Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Keshapatikana na wahalifu wako rupango... Heko za kipekee zimuendelee mkuu wa mkoa kijana na mahiri wa Dar na kamanda mambo sasa ... Dar iko salama
 
Yule mfanyabiashara kule Tarime yeye aliwapiga Risasi bila msaada wa bodyguard iweje yeye ashindwe kujihami?
Mkuu, si unajua mambo ya gym, huenda alikua kavaa bukta so huwezi weka bastola; anyway, maadamu na wana ccm nao wameanza kutekwa, labda tutatia akili maanake mwanzoni ilikuaga either wapinzani au wanao amini katika upinzani
 
Duh!Watu wasioujulikana hao bila shaka!

Hii nchi sasa!!

Walitekwa na kupotea watu wa kawaida, tukaona ni mambo madogo.Leo wanatekwa matajjri na watu maarufu labda sasa ndio tutashituka.

Nakumbuka pia yaliompata Lissu na mfanyabiashara wa Tarime bwana Zakaria.

Wacha tusubiri tuone nini kinaendelea tutapata picha kamili.

Kwa sasa wanaweza kuwa wanapima upepo.Pressure ikiwa kubwa,wanaweza kumwachia ikiwa mpaka sasa bado yuko salama.

Hii update kuwa katekwa na wazungu,inanipa maswali mengi sana na mojawapo ni wazungu gani hao wa kumteka mtu tajiri kama huyo tena wakiwa katika nchi ya watu?

Wanajiamini nini?
Wanajulikana si wamesema wazungu
 
Watanzania wengi hamjielewi, hili ni jukumu la Polisi kumpata Mo na kuwakamata watekaji.

Kazi ya Tiss ni kutowa information kabla ya tukio kutokea, Tiss hawana power of arrest

By the way Makonda ndio mwenye uwezo wa kumpata Mo alipo, narudia Makonda akamatwe mara moja kama kweli jeshi la Polisi linajitambuwa.
Kwani madaladala ana bifu nae ?
 
Hii issue tatizo linachukuliwa kisiasa zaidi....
Kwa kweli ili kuepusha mengi matajiri wanatakiwa wawe makini maana wanaangaliwa na watu wengi sana wema kwa wabaya.

Yule ni tajiri na mfanyabiashara yawezakuwa ni utekaji wa kawaida tu lengo la watekaji wapate pesa au ni kwenye mambo yao ya kibiashara.

Nilijua kwa sababu jamaa ni mwanachama wa CCM watu watasema ni utekaji wa kawaida...ila mpaka sasa kuna stori zimeanza kuundwa.
Nimekuelewaaa

Muhimu sisi Yambwa eti yambwa ...Yanga tusihusishweee
 
Mo Kapatikana.
IMG_20181011_100835_026.JPG
 
Back
Top Bottom