Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Screenshot_2018-10-11-10-30-47-909_com.instagram.android.jpeg
 
System at work, ameonywa tu aache figisu anazozifanya chini kwa chini..

Utaona kama hao watekaji watajulikana..
Huyu si ni cooporate. Wanaweza wakamuita ofisini au wakamfuata ofisini kwake wakamueleza bwana tunalo file lako sasa tunakuagiza uache. Usipoacha tutadeal na wewe. Ya nini kutuhusisha na sie na kutuletea hofu isiyo na sababu maana hata hayo hawatatueleza na kuwaletea stress wanasimba.

Mambo mengine ni ovyo kama yanafanywa na mgambo.
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

Hii sio taarifa nzuri sana kwa Collosium gym itapoteza watu maarufu wateja, pia kwa wawekezaji, huyu MTU amegusa maisha ya watu wengi sio kitu cha kuchekea , Mh Rais hawezi kulifumbia macho hili hatari kubwa.
 
Kama ni kick kwahilo lilifanyika,najiuliza nikwafaida ya nani?ili iweje?
 
Ana upako mkuu wa mkoa wangu kujua wanaotekwa.. Tusubiri Mambosasa akifanya tukio live LA kututangazia watekaji wa tajiri wetu Kama watataka kutuonyesha kwanza maana hawakawii kusema wataharibu uchunguzi wakituonyesha watekaji
Halafu tunazidi kujijengea sifa mbaya kila kukicha. Ile sifa yetu ya Tz ni nchi ya Amani inapotea kila kuchwao.

Polisi wawe tayari kutupa mrejesho wa kilichotokea, ni nani waliomteka, kwa kosa gani, ili iweje?

Makonda anao wajibu wa kuwatoa wananchi wake ktk hali ya hofu kuhusu watu wasiojulikana.
 
Nimemsikiliza Kamanda Mambosasa anadai kuwa ametekwa na Wageni kwa vile ni wazungu!! ........... Hivi kwani hakuna Wazungu watanzania!!?

Anyway, kama walikuwa wameficha usoni hivi kweli kwa tukio la haraka kama utekaji utawatofautishaje wazungu, wahindi au waarabu!!
 
Back
Top Bottom