Dar: Mganga wa kienyeji akutwa na watoto wawili wa familia moja walioibwa na msaidizi wa kazi

Dar: Mganga wa kienyeji akutwa na watoto wawili wa familia moja walioibwa na msaidizi wa kazi

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili wakiume na wakike nyumbani kwa mganga wa kienyeji anayefahamima kwa jina la Abdulikarim mkazi wa Kimara baruti.

“January 12,2025 tulipata taarifa za kuibwa watoto wawili wadogo mmoja wa kike mwingine wakiume, mmoja Miaka mitano mwingine minne, dada wa kazi kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji Kimara walishirikiana kufanya kitendo cha kihalifu kuiba watoto”

Soma: Dada wa kazi atoweka na watoto wawili mara baada ya kwenda dukani

Aidha Watoto wote wamefanyiwa vipimo Afya zao ni njema na wamekabidhiwa kwa wazazi wao wakati shauri la watuhumiwa likisubiriwa kukamilika ili kufikishwa Mahakamani.
 
Hawa wapuuzi kitanzi ndo kinacho wafaa.
 
Back
Top Bottom