Dar: Mganga wa kienyeji akutwa na watoto wawili wa familia moja walioibwa na msaidizi wa kazi

Dar: Mganga wa kienyeji akutwa na watoto wawili wa familia moja walioibwa na msaidizi wa kazi

Binadamu bhana,hawataki kumwamini Mungu ila wanaamini ushirikina🙌
 
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili wakiume na wakike nyumbani kwa mganga wa kienyeji anayefahamima kwa jina la Abdulikarim mkazi wa Kimara baruti.

“January 12,2025 tulipata taarifa za kuibwa watoto wawili wadogo mmoja wa kike mwingine wakiume, mmoja Miaka mitano mwingine minne, dada wa kazi kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji Kimara walishirikiana kufanya kitendo cha kihalifu kuiba watoto”

Aidha Watoto wote wamefanyiwa vipimo Afya zao ni njema na wamekabidhiwa kwa wazazi wao wakati shauri la watuhumiwa likisubiriwa kukamilika ili kufikishwa Mahakamani.
Aisee!
“Wamefanyiwa vipimo na afya zao ni njema”

Je, kwa upande wa vipimo visivyoonekana Hosp.? Ama Serikali haiamini ushirikina.
 
Aisee!
“Wamefanyiwa vipimo na afya zao ni njema”

Je, kwa upande wa vipimo visivyoonekana Hosp.? Ama Serikali haiamini ushirikina.
Kwa hiyo vipimo visivyoonekana huwa ni vya kishirikina? Hivyo vipimo huchukuliwa kwa mitambo inayoonekana k.v kumkata kuku kichwa na kumuachia ghafla kisha kuangalia anavyotapatapa na kumtumbua ili kutoa maini yake na kumtafuta mchawi! Tawile! tawile! mchawi ni yule Bibi kizee aishiye nyumba ileee!
 
Mkuu, nimetumia lugha laini ya “Vipimo visivyoonekana kwa vifaa vya hosp”.
Lakini bila shaka umenielewa.
 
Polisi wakiamua kufanya kazi na kutowasikilia wanasiasa, kazi wanaiweza.
Hongera IGP na vijana wako.
Mganga alazimishwe amtaje mteja wake hata kama ni mtu mzito huko serekalini ili tupate kuwajua mashetani yalio jificha kwenye ngozi ya kondoo!!
 
Huyo mganga ilitakiwa achapwe risasi hadharani iwe mfano kwa wengine sema ndio hivyo hatuna hiyo sheria..
 
Msichana hakukutwa?, maana atasaidia kujua lengo la kuwachukua na kuwaacha hapo.
 
Huyo Mganga atakua keshaua watoto wengi mpaka kufikia hatua ya kukamatwa
 
Huyo mganga ilitakiwa achapwe risasi hadharani iwe mfano kwa wengine sema ndio hivyo hatuna hiyo sheria..
Pengine huyo mganga ahusiki kwa lolote, anaweza kuwa amedanganywa na huyo msichana " nawaacha kwa muda nitawafuata kesho"...... huyo msichana atasaidia sana uchunguzi .
 
Safi sana Jeshi la polisi.

Ila CID wengine wana "jicho"la tatu,wamejiweka vzr,wamejiongeza...wana uwezo wa kutambua mharifu alipo.

Nina Rafiki mmoja ni kazi yake.
Unasifia kitu ambacho hata kwenye maandishi na tamko la jeshi la polisi hakipo

Inakuaje kama raia wema ndo wametoa taarifa kwa polisi?

Wauaji wa Mzwe kibao na kutekwa kwa Soka hao Polisi hawana unoma siyo?
 
Hivi kwanini kuwa Mganga kienyeji lazima uwe muislam au upewe Jina la kiislam?
 
Wafanyakazi ni kuwanao makini sana, ndio maana waarabu wanakuwaga makini sana kwa watoto wao, sio kama waswahili wengi wao wanaviachia tu vitoto vyao mara viingie mitaani mara mabarabarani end of the day vinagongwa au kuibiwa.
 
Hivi kwanini kuwa Mganga kienyeji lazima uwe muislam au upewe Jina la kiislam?

Ng'wanamalundi alikua muislamu? N.k wengi tu. So Uisilamu hauna mahusiano na hicho ulichouliza.

Ukiona Mganga ni muislamu basi huyo yupo mbali na mafundisho ya dini yetu, kwa maana ni muislamu JINA huyo.
 
Back
Top Bottom