JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amesema zaidi ya wagonjwa 160 wameshapatiwa huduma katika maabara hiyo toka ilipoanza kazi mwaka 2021. Maabara hiyo imejengwa na Serikali kwa zaidi ya Tsh Bilioni 7.9.
“Hivi karibuni tulianzisha ushirikiano na wenzetu hawa Hospitali ya Ramaiah India ili tushirikane katika kuboresha huduma zetu za uchunguzi na tiba ya Ubongo hapa nchini, sasa ndio wamekuja na wamewahudumia wagonjwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu wetu ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kisasa za upasuaji,” alisema Dkt. Boniface.
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo kutoka Hospitali ya Ramaia India, Dkt. Sunil Valentine Furtado amesema ujio wao umetokana na majadiliano ambayo yalifanyika baina yao na uongozi wa MOI ambapo ushirikiano baina ya Taasisi hizi unalenga kuboresha huduma kwa wagonjwa, kubadilishana uzoefu na mafunzo.
Source: Matukio na Maisha