#COVID19 Dar: Mkuu wa Mkoa awataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa CORONA

#COVID19 Dar: Mkuu wa Mkoa awataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa CORONA

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI DHIDI YA CORONA.

Kufuatia kuwepo kwa Viashiria vya Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla* amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari* na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za Maji na Miundombinu ya Maji tiririka.

Akitoa tamko la tahadhari dhiri ya Corona RC Makalla amesema kutokana na Mwingiliano wa watu kutoka Nchi jirani na Nchi mbalimbali na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa Wananchi.

Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na :-

1.Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya.

2. Kunawa Mikono kwa Maji tiririka kwa sabuni Mara kwa Mara.

3.Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua Makali, kikohozi, uchovu na nyingine.

4. Kufanya Mazoezi ili kuimarisha Kinga ya Mwili.

5. Kula mlo kamili.

6. Uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara wakiwemo Wazee na Wenye Magonjwa sugu.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.

IMG-20210624-WA0063.jpg

IMG-20210624-WA0066.jpg

IMG-20210624-WA0067.jpg

IMG-20210624-WA0068.jpg

IMG-20210624-WA0064.jpg

IMG-20210624-WA0062.jpg
 
Elimu iendelee kutolewa maaana sisi watanzania ni wagumu sana kuelewa,
tuchukue tahadhari, tuhakikishe tinavaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko, kama vile kwenye daladala n.k
 
Kuna ambaye hana elimu kuhusu korona? Elimu itatolewa na tutakuwa hivi hivi
Tatizo letu ss watanzania wajuaji hadi kwenye kifo tunajifanya wajuaji!!!

Mhe. Rais amesha tuambia wazi wazi kuwa tuchukue tahadhari, tuvae barakoa, tuepuke misongamano.
au tuanze kuchapana viboko?
 
Tunakwenda vizuri:

"Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo."

Matumizi ya ka minimum force hakajawahi kuwafanya waungwana wakasikitika.

Kama kawaida waumini wazalendo wa awamu ile habari ndiyo hiyo.
 
Tatizo letu ss watanzania wajuaji hadi kwenye kifo tunajifanya wajuaji!!!

Mhe. Rais amesha tuambia wazi wazi kuwa tuchukue tahadhari, tuvae barakoa, tuepuke misongamano.
au tuanze kuchapana viboko?
Sasa elimu ipi zaidi unataka itolewe. Hii ni wave ya tatu ya korona, watu wanajua kutofautisha usanii na uhalisia.
Korona ipo lakini si kwa kiasi cha kutishana kiasi hiki
 
Tatizo letu ss watanzania wajuaji hadi kwenye kifo tunajifanya wajuaji!!!

Mhe. Rais amesha tuambia wazi wazi kuwa tuchukue tahadhari, tuvae barakoa, tuepuke misongamano.
au tuanze kuchapana viboko?

Tunakoelekea sasa ni kwenye bakora. Na iwe hivyo kwani bila kiboko punda hawezi kwenda.
 
Kila siku kututia hofu tu, ndiyo kazi tuliyowatuma? Kama wameshindwa kutuongoza waache kazi.
Kuongoza ni kuwa wakweli Watanzania hawataki mtu wa kuwadanganya hasa pale maisha yanapokuwa hatarini. Wimbi hili mpya limeingia na leo baba wa Rafiki yangu kapoteza maisha Musoma. Kanda ya ziwa imeshaingia kutokea Uganda. Viongozi wanao puuzuia magojwa yanaweza kuwaondoa hata wenyewe na tumeshaona hili.
 
Kwanini unachukulia ni kutiwa hofu?

Kutakiwa kuchukua tahadhari kabla ya hatari ni kutiwa hofu?

Tafakari kwa usahihi ndugu.
 
Makanisani sijui kama watasikia hayo. Kuna makanisa hayana maji tiririka, ibada hadi masaa 2, kupeana amnai tena padre anasema peananeni mikono ya amani.
La ajabu watu wanapeana mikono ya amani halafu wanaenda kukomunika kwa mikono!
 
RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI DHIDI YA CORONA.

Kufuatia kuwepo kwa Viashiria vya Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla* amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari* na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za Maji na Miundombinu ya Maji tiririka.

Akitoa tamko la tahadhari dhiri ya Corona RC Makalla amesema Kutokana na Mwingiliano wa watu kutoka Nchi jirani na Nchi mbalimbali na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa Wananchi.

Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na :-

1.Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya.

2. Kunawa Mikono kwa Maji tiririka kwa sabuni Mara kwa Mara.

3.Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua Makali, kikohozi, uchovu na nyingine.

4. Kufanya Mazoezi ili kuimarisha Kinga ya Mwili.

5. Kula mlo kamili.

6. Uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara wakiwemo Wazee na Wenye Magonjwa sugu.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.

View attachment 1828681

View attachment 1828682

View attachment 1828683

View attachment 1828684

View attachment 1828685

View attachment 1828686
Yule mzee mlimdanganya hakuna colona. Mungu anawaona
 
Kila siku kututia hofu tu, ndiyo kazi tuliyowatuma? Kama wameshindwa kutuongoza waache kazi.
Unaowalaumu hapa wametokana na serikali inayoongozwa na chama gani?siyo hao hao unaokata mauno humu kuwashangilia?

Subiri bado hujapewa limit ya kutembea mitaani!

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Kwani si chanjo inakuja, ileteni msiotaka kufa na Corona mchomwe halafu mtuache sisi tunaotaka kufa tuendelee kufa na Corona kwa kuendelea kuishi maisha tuliyoyazoea ya kutojibanabana.

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
 
Makanisani sijui kama watasikia hayo. Kuna makanisa hayana maji tiririka, ibada hadi masaa 2, kupeana amnai tena padre anasema peananeni mikono ya amani.
La ajabu watu wanapeana mikono ya amani halafu wanaenda kukomunika kwa mikono!
Mkuu si vizuri kutoa taarifa ya kupotosha!

Kanisa Katoliki liliondoa utaratibu wa kutakiana amani kwa kushikana mikono siku nyingi sana zilizopita.

Utaratibu unaotumika kwa sasa ni kuinamisha kichwa kidogo kwa mtu unayemtakia amani; na yeye akifanya hivyo hivyo.

Huku niliko makanisa yote yana maji tiririka kwa ajili ya waumini kunawa mikono.
 
Kiongozi mzuri ni Yule anayependa na kulinda wananchi wake. Asante Sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Mkuu wetu wa mkoa. Tulipoteza viongozi wetu, ndugu, majiraji na marafiki Kwa uzembe. Nikimkumbuka wale shangazi zangu wawili mmoja 2020 na mwingine 2021 sina hamu kabisa. Yaani nikisikia mtu anakejeli Corona ninasikia nachefuka. Siku ikikufika ndiyo utashika adabu. Endeleeni kubeza.
 
Ningeshangaa msaliti kulipwa hela. Kwa kazi ipi aliyofanya? Kwa kuzunguka nchi za ulaya akiitukana Tanzania na watanzania?
Tutashitakiwa MIGA?

UJINGA MTUPU
Inahusiana vipi hii katika suala la Covid-19?
 
Back
Top Bottom