Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 5,168
- 8,982
Ukifika Dar kwanza jihesabu wewe ni miongoni wa wateule wenye bahati, hivyo usiichezee nafasi hiyo.
Bila kujali umeenda huko kwa njia gani iwe umeletwa kwa kudandia gari ya msiba, ama umeenda kama shamba boi, dada wa kazi, umeenda kama saidia fundi au umeletwa mara moja kubarizi na kupunga upepo au kusalimia ndugu vyovyote iwavyo usikubali kurudishwa kijijini kwenu kizembe hasa kama ramani zako bado hazijakaa sawa.
Ukifika Dar utagundua watu wake hawalali, kutwa kucha vijiwe na masoko yamejaa watu wakijumua na kuuza vitu mbalimbali. Saa tisa usiku ukishuka pale Kariakoo/Karume/Tandale/Tandika na senta zingine kubwakubwa utakuta watu kibao unaweza kuzani ni mchana. Hao watu wote wanapambana watoboe kimaisha. Maisha ya Dar yanaweza kuwa magumu hasa unapoanza lakini ukikomaa na ukapata kampani sahihi na kumwomba mola wako maisha yanasonga.
Tatizo vijana wengi wanakuja Dar na kuishia kukaa kizembe kama kuku wa kizungu au kama kuna katv hapo home basi yeye muda wote anamalizia hapo. Sasa ukiwa wa hivi lazima upaone Dar pachungu na hapakufai.
Dar ni jiji kubwa sana na limetanuka kila upande, shughuli za kuingiza pesa ni chungu mbovu cha msingi ni wewe kukaa sehemu sahihi na watu sahihi. Usibakie apo ndani kwenu kama utumbo!
Kuna watu nawafahamu wameenda Dar wakiwa hawana chochote lakini leo hii wana miji yao pale Dar. Wengine hadi kuna mitaa inaitwa majina yao. Kinachoibeba Dar ni mzunguko mkubwa wa pesa uliopo pale. Almradi unajichanganya unachapa kazi lazima utaona kesho yako.
Najua kuna watu watasema mbona kuna umaskini mkubwa sana Dar? mbona kuna watu wanaishi ktk hali ngumu sana pale Dar. Hiyo sio uongo ni kweli kabisa. Kuna wengi tu wanaishi pale lakini hawajaweza kumiliki hata kijiko au sufuria! na unaweza kukuta wamekuwa wakaazi wa hapo wa miaka nenda rudi. Kinachotofautisha watu ni jitihada na kudra, hamna kingine. Siku zote ukifanya jitihada na ukatia nia mola ya mafanikio, mola wako atakulipia.
Cha muhimu jichanganye kwa walio sahihi na kwa yaliyo mema utafanikiwa. Kingine Dar hakuna wa kusema anakufatilia eti akuroge. kila mtu anapambana kivyake watu wanatoka nyumbani usiku wanarudi usiku, unaweza kukuta miezi 6 haujaonana na jirani yako wa nyumba ya pili.
Kwahiyo ukigusa ardhi ya Dar wewe komaa adi kielewe na ukiona sponsa wako aliyekupeleka uko anang'ang'ana akurudishe kijijini kwenu, wewe chimba potelea huko kitaa jimix katafute ramani zingine usikubali kurudishwa kwenu kizembe. pambana ujenge hatima bora kwako na vizazi vyako vijavyo.