Mimi ninawalaumu hao wananchi. Kuna jamaa anaitwa Massawe, yeye amehamisha mto fulani huku Madale na mto ukaenda mbali bila kuathiri nyumba na shamba.
Hapohapo, kuna ''mswahili' ambaye shamba limesombwa na mto kwa sababu ameshindwa kupanda miti na majani ili kuuzuia mto kama alivyofanya Massawe.
Niniwalaumu wananchi wa Kibo kwa sababu, wao ndiyo wazembe. Wangepanda miti na magugu, huo mto Gide usingefanya uharibifu.
Waswahili hawapendi kutunza mazingira bali wanataka mazingira yawatunze. Haiwezekani mazingira yawe bora Kama mwanadamu hachukui hatua.
Watu wa Kibo na Kibangu wamevuna walichopanda.
Huwa ninachukia sana tabia ya kutokutunza mazingira.
Huko Kilimanjaro Kuna mito na miinuko mikali lakini huwezi kusikia upuuzi wa mito kufuata watu na kusomba ardhi, kwa sababu watu wanapanda miti na magugu ili kulinda ardhi.