JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakati Serikali na wadau mbalimbali wakisisitiza umuhimu wa jamii kuwa na vyoo bora ambavyo vinaweza kuepusha baadhi ya magonjwa yakiwemo ya milipuko, upande wa ofisi nyingi za Serikali za Mitaa hazina vyoo kabisa huku kati ya ofisi zenye huduma hizo baadhi vyoo vyake hivipo katika hali ya kuridhisha hali ambayo inahatarisha afya za watumiaji.
Hapa Dar nimeshuhudia hali hiyo katika ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Jogoo, ofisi ya Serikali ya Mtaa Ndumbwi, Mbezi juu Sakuveda, Mbezi Mtoni Wilayani Kinondoni.
Nimeona hivyo pia katika Ofisi nyingi za Serikali za Mitaa zilizoko Wilaya nyingine zikiwemo Temeke na Kigamboni, wahusika hawana huduma ya vyoo.
Wanaofika kwenye ofisi hizo au waliopo wanalazimika kutafuta njia mbadala kwa ajili ya kumaliza haja zao.
Njia mbadala zinazotumika ni kutumi vyoo vya watu binafsi maeneo ya karibu na ofisi, wanaoteseka zaidi ni Wamama wenye Watoto, wakati mwingine wanamaliza haja zao kwenye maeneo yasiyo rasmi.
Hali hiyo inachangia baadhi ya viongozi kutotimiza majukumu yao kwa umakini unaotakiwa au wakati mwingine kuendesha majukumu ya kiofisi wakiwa majumbani kwao au maeneo mengine yasiyo rasmi.
Tukumbuke imebakia miezi michache Nchi kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika udadisi wangu nimebaini changamoto ya miundombinu ya vyoo inaweza kusababisha kuwakosa viongozi bora, kwa kuwa kukosekana kwa huduma za vyoo inaweza kuwa kikwazo kwa wengine kutaka dhamana ya kuongoza.
Serikali inaweza kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kila baada ya miaka mitano, basi hiyo ni ishara ya kutambua umuhimu wa mamlaka hizo.
Hivi nini kinashindikana kuratibu ujenzi wa vyoo bora kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa hususani kwenye Jiji la Dar ambapo idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi.
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ni kweli imeshindwa kubaini changamoto hiyo na kuratibu kampeni maalum ya uboreshaji wa miundombinu ya ofisi za Serikali za Mitaa hususani kujenga na kuboresha vyoo?
Serikali za Mitaa ni msingi wa awali wa utatuzi wa changamoto za kijamii, hivyo haina budi kuboresha miundombinu ya vyoo kwenye ofisi hizo, ili ziweze kuwa kikocheo cha wananchi kufika na kupata huduma.
Hata hivyo katika udadisi wangu licha ya suala la vyoo imebainika uwepo wa Serikali za Mitaa ambazo ofisi zake hazina ubora, hali ambayo inaweka hatarini nyaraka muhimu za umma.
Serikali inaweza kutenga fungu kwenye mapato ya ndani ambayo yanasimamiwa na wakurugezi kwa lengo la kuboresha ofisi za Serikali za Mitaa hata Vijiji.