Dar: Polisi yazima maandamano, yakiri kumshikiliwa Sheikh Ponda kwa mahojiano

Dar: Polisi yazima maandamano, yakiri kumshikiliwa Sheikh Ponda kwa mahojiano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Novemba 10, 2023 Dar es Salaam, pia amewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo.

=====

Polisi Dar wazima maandamano, Sheikh Ponda akamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Mwananchi Digital ilifika Mnazimmoja na kukuta umati wa watu, huku askari Polisi wenye sare wakiwa wameimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo.
Chanzo: Mwananchi

===========

UPDATES: TAARIFA YA JESHI LA POLISI

Akizungumza na JamiiForums kuhusu taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema:

"Tulimueleza taarifa zinazohusiana na mikutano au makusanyiko, taarifa zake anatakiwa kupeleka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, na Mkuu wa Polisi wa Wilaya anatakiwa kutoa mwongozo wa kiusalama, yeye (Ponda) hakufanya hivyo.

"Baada ya kuelezwa hivyo, hakufanya chochote, akawa anahamasisha kwenye mitandao kuhusu, akaanza kukusanya watu, hakufuata utaratibu kama anakubaliwa au la.

"Kinachofanyika anahojiwa, tunataka kujua kuna nini kinachoendelea kuhusu mipango iliyopo.

"Baadaye tutaangalia mazingira, tutaangalia hiki kinachochunguzwa kama kinadhaminika au tofauti, baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria na anatoa ushirikiano mzuri katika mahojiano."
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Novemba 10, 2023 Dar es Salaam, pia amewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo.

Kwa nini wananchi wawe wanapnywa kutekeleza entitlements za kisheria? Katiba na sheria vinaruhusu maandamano. Polisi wanazuia. Nani wa kumpuuza?
 
Kwa nini wananchi wawe wanapnywa kutekeleza entitlements za kisheria? Katiba na sheria vinaruhusu maandamano. Polisi wanazuia. Nani wa kumpuuza?
Lakini wapuuzi wakisema wanaandamana kumpokea yule vuvuzela Bashite ziro brain ni ruksa!
Kweli mtu akikuambia akili zako kama manjagu wa TZ jifungie ndani ulie maana ni dharau kubwa
 
Acha waseme maana tutatii sababu wanajua tutatii.
Opposition hakuna so acha waendelee kutugeuza kama chapati mpaka siku tukijitambua.
 
Poleni sana Wapalestina wa Bongo.

Walioandaa Maandamano hawana weledi,wangetumia kigezo Cha Kuandamana Ili Hamas Wawaachie Wale Watoto Wetu ,harafu mbele huko inageuka kuwa Takbiir na kulaani Mazayuni.

Bure kabisa 😁😁
---
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Mwananchi Digital ilifika Mnazimmoja na kukuta umati wa watu, huku askari Polisi wenye sare wakiwa wameimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo.

Mwananchi
 
Safi Sasa kuzua taharuki kwa Mambo ya kipumbavu et oooh ndugu zetu wanaonewa pumbavu kabisa hawa

Kongo ndugu zetu wa Afrika wenzetu jilani zetu weusi wenzetu Ila Kila MTU yupo kimya Leo uandamane ufunge barabara kisa mwalabu ambae hakusaidi chochote

Bibi yetu mfia dini Faiza hakua uko kwenye maandamano?
 
Back
Top Bottom