Dar: Rais Samia ashiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC Februari 8, 2025

Dar: Rais Samia ashiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC Februari 8, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC Februari 8, 2025.

Rais Samia amewataka viongozi wenzake wa Kikanda kuchukua hatua madhubuti kuhusu hali inayoendelea kuzorota katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akionya kwamba historia itawahukumu vikali endapo watafumbia macho mgogoro kati ya Serikali ya DRC na Vikosi vya M23 ambao unatajwa kusababisha vifo vya takriban raia 700 huko Goma

Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, alizungumza hayo akitoa hotuba ya ukaribisho kwa Wakuu wa Nchi waliohudhuria Mkutano wa Pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam, Tanzania, ukiwa na lengo la kutafuta mwafaka wa mgogoro huo

Katika Mkutano huo, Viongozi Wakuu wa Kikanda, akiwemo Rais Samia na Rais wa Kenya, William Ruto, wamehimiza umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja, wakionya kutokuchukua hatua kutazidi kudhoofisha utulivu wa DRC



Pia soma:
=====

Maazimio ya mkutano huu soma hapa: Mkutano wa SADC na EAC waazimia kuondoa vikosi vya kigeni visivyoalikwa katika ardhi ya DRC
 
Back
Top Bottom