Dar: Rais Samia atembelea eneo la ajali ya ghorofa Kariakoo, asema vifo vimefikia Watu 20

Dar: Rais Samia atembelea eneo la ajali ya ghorofa Kariakoo, asema vifo vimefikia Watu 20

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili hivi punde Kariakoo, Dar es Salaam, ambapo jengo la Gorofa liliporomoka Jumamosi na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.

Kuhusu ajali hiyo, soma LIVE - Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 16 wafariki 77 waokolewa

Alipofika eneo la tukio, Mkuu wa Nchi alikagua jengo lililoporomoka kabla ya kuhutubia wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa nchini Brazil kwenye Mkutano wa G20 ametua jijini Dar es Salaam leo na moja kwa moja kuelekea eneo lilipoporomoka jengo Kariakoo. Amesema taarifa aliyopewa, Watu 20 wamepoteza maisha kwenye jengo hilo

Amesema

“Jitihada zetu kubwa katika tukio hili ilikuwa kuwaokoa wenzetu walionasa ndani ya jengo hili wakiwa hai, ndilo lengo letu lililokuwa kubwa, lakini kama tunavyoambiwa jitihada haiondoshi kudra ya Mungu au kadara ya Mungu, pamoja na jitihada iliyofanywa na serikali na waokoaji hawa walioko hapa lakini bado kuna wenzetu ambao tumewapoteza na taarifa niliyopewa leo ni kwamba mpaka saa tatu asubuhi tumepoteza wenzetu 20 ambao serikali imeshirikiana na familia kuwasitiri wenzetu ipasavyo, lakini wenzetu majeruhi ambao walikuwa wamepelekwa hospitali naambiwa kuna watu watatu tu na nikitoka hapa nitakwenda niwaone niwasalimie.”

“Hili sio pigo kwa Familia zilizopoteza Watu wao pekee yao ni pigo letu kama Watanzania na tunaguswa pia, ni kumbukumbu ya kutisha kwa wenzetu waliookoka hapa, kwa jinsi jengo lilivyo Mtu akitoka hai bila shaka hawapo sawa (kisaikolojia), niombe wasifadhaike, wajipe moyo na tuendelee na shughuli zetu za kawaida bado Mungu ana kazi nao”

“Tukio hili ukiangalia kwa macho tu lina viashiria vya kuwepo kwa mapungufu ya kiutendaji hivyo nitoe wito kila Mtu atimize wajibu wake ipasavyo, ukiangalia jengo lile lilipewa vibali kutoka Serikalini vya ujenzi lakini jengo lile halikutazamwa ubora wake wakati wa ujenzi, niwaombe wote tunaohusika Serikali Kuu, Halmashauri na Wananchi wote kwa ujumla tuseme kwa pamoja kwamba matukio ya aina hii yasijirudie”




PIA SOMA
- Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi

- ZIMAMOTO: Watano wamefariki, zaidi ya watu 40 wameokolewa ajali ya ghorofa Kariakoo

- Waziri Mkuu Majaliwa awasili lilipoporomoka jengo Kariakoo, uokoaji waendelea

- Ghorofa laendelea kushuka, zoezi la uokoaji lasimama, mwananchi watawanywa

- Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"

- Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Polisi kumtafuta mmiliki wa Jengo lililoporomoka Kariakoo
 
Siku ya 5, jengo la ghorofa 4 bado wanahangaika nalo, badala ya kujifunza hapa, ikatolewa pesa vifaa vikanunuliwa ili siku zijazo tusifedheheke, katoa milioni 700 kwa taifa stars.

Jana watu walikuwa wanajadili humu kitanda muhimbili ni 50 elfu kwa siku.
Bado kuna shoga anatoka anasema wanamsapot, yaan wanasapot nini? Bora hata watu binafsi wakichangisha michango wanaweza saidia wenzao
 
Siku ya 5, jengo la ghorofa 4 bado wanahangaika nalo, badala ya kujifunza hapa, ikatolewa pesa vifaa vikanunuliwa ili siku zijazo tusifedheheke, katoa milioni 700 kwa taifa stars.

Jana watu walikuwa wanajadili humu kitanda muhimbili ni 50 elfu kwa siku.
sasa yeye vinamuhusu nini. Hana uchungu wowote na bara. Ingekuwa imetokea Zanzibar kungeitwa waokoaji hata kutoka nje ya nchi.

Katika akili ya kawaida kwa mtu mwenye uchungu angetoa hiyo Mil 700 kwa wahanga na waokoaji ila kaona kipaumbele ni Taifa Stars.
 
Ningemuona wa maana sana kama angefanya hivyo
ili kufanya hivyo ilipaswa awe na uchungu, ila hana uchungu wowote. Ingekuwa mtu mwenye busara angeghairisha safari na kutuma mwakilishi, badala yake kaendelea na mambo yake tu.

Huyu mama akapumzike tu, maana hata kiakili hayupo kiuongozi, ni kama mtu aliejichokea tayari.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili hivi punde Kariakoo, Dar es Salaam, ambapo jengo la Gorofa liliporomoka Jumamosi na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.

Alipofika eneo la tukio, Mkuu wa Nchi alikagua jengo lililoporomoka kabla ya kuhutubia wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa nchini Brazil kwenye Mkutano wa G20 ametua jijini Dar es Salaam leo na moja kwa moja kuelekea eneo lilipoporomoka jengo la Kariakoo. Amesema taarifa aliyopewa, Waru 20 wamepoteza maisha kwenye jengo hilo


View: https://www.youtube.com/watch?v=LxRylvve7ao

kwani alikuwa wapi?anajua term hii kuna form ya Urais zaidi ya moja
 
Hivi waathirika hawawezi kumshtaki mwenye jengo, pamoja na serikali, kutokana na ajali hii? Raisi, kwa maana serikali, amekiri kuwepo na uzembe kwa upande wao.
 
Watu wachache sana wamesababisha msaafa, mpaka sasa wapo uraiani wanapiga mvinyo huku wanasubiri sakata lipoe waanzishe dili lipya. Kumbuka bila madili mjini hakuishiki
 
Back
Top Bottom