Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa yoteWewe unaijua kwa lipi?
Maneno ya RC yafanye ndiyo ya Rais kwa wale wanaopinga bandari isiendelezwe.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo August 17, 2023 amevunja uongozi wa Soko la Mabibo na kukabidhi soko hilo kwa Manispaa ya Ubungo.
Soko hilo lililokuwa likimilikiwa na kikundi cha watu wachache nakupelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali ambazo Mkuu wa Wilaya Mhe. Hashim Komba alizibaini kama, miundombinu mibovu iliyo pelekea kuwepo kwa tope wakati wa mvua, chemba kuziba, mazingira machafu sokoni hapo, kutokuwepo kwa taarifa sahihi za mapato na matumizi, kutokuwepo kwa maboresho yoyote sokoni hapo huku kikundi cha watu wachache wakinufaika.
Katika mkutano huo, Mhe. Chalamila alianza kwa kuukemea vikali uongozi huo kwa mambo yaliyokuwa yanaendelea sokoni hapo ikiwemo kuwafukuza watumishi wa Serikali na hata kufikia hatua ya kutaka kuchoma moto gari la kubeba taka linalomilikiwa na Serikali.
"Hawawezi kutupanda kichwani, nimechukizwa na vitendo hivyo," alisisitiza Chalamila.
Aidha, Chalamila aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakaye kuja kusumbuliwa wakati serikali ikifanya shughuli zake katika soko hilo kama ukusanyaji wa ushuru na uendeshaji wa soko hilo kiujumla.
Soko litakuwa chini ya Manispaa na kuhakikisha hakuna mfanyabiashara atakaye sumbuliwa na mtu yeyote, taratibu zote zitaendelea kama kawaida, aliwaagiza wafanyabiashara sokoni hapo kulipa ushuru kwa Manispaa.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara sokoni hapo wamepongeza hatua hiyo ya serikali ya kuchukuwa soko wakiamini soko hilo ninakwenda kuwa bora zaidi kama masoko mengine.
Halikadhalika, Soko hilo limetengewa kiasi cha shilingi milioni 600 kwaajili ya kuliboresha na katika uboreshwaji huo hakuna mfanyabiashara yeyote atakaye ondolewa wakati uboreshaji unaendelea
Pia soma - Hali ya soko la Mabibo wakati wa mvua ni mbaya sana
Haya sasa kuwa msemaji wa mabibo badala ya chato.Haijui mabibo huyo.Mwacheni
Hujanisoma?Fanya basi
Manispaa ya Ubungo ndiyo yenye dhamana ya kuanzisha, kuunda na kuendesha Masoko na Magulio. Hii ni kwa mujibu wa Sheria Ndogo (Masoko na Magulio) ya Manispaa ya Ubungo ya mwaka 2019Hili swali lijibiwe na huyu anayesapoti uhuni wa RC. Soko liliwmzishwa na wafanyabiashara wenyewe na lilikuwa linamilikiwa na wao 100% isipokuwa ushuru wa Halmashauri ulikuwa unatozwa kama kawaida. Sasa RC kijanja anakabidhi soko Kwa Halmashauri na soon tutaona watu wanaanza kulipa Kodi za vibanda Kwa hicho kisingizio cha m600 hewa zitakazowekezwa.