milangomitatu
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 1,469
- 1,166
Nlikuwa napaki gari akaniambia (tusi) nlikuwa naenda ATM kisa anaona eti nimepaki karibu na kibanda chao badala ya kuniambia kistaarabu maana nlikuwa sijui tena ni madogo sema lugha hata mimi nlimwambia sababu una sare zako nakuacha ila ungekuwa kitaa ningekifumua nkasepaulikutana nao kwenye escot au ulikutana nao wapi mkuu???
tunachozungumza ni maeneo hatari mfano katika kusindikiza pesa kama hizo...
wewe UKnaleta matukio ya wapi mkuu??
Ipo haja ya polisi kuchukuliwa kutoka sumajktNlikuwa napaki gari akaniambia (tusi) nlikuwa naenda ATM kisa anaona eti nimepaki karibu na kibanda chao badala ya kuniambia kistaarabu maana nlikuwa sijui tena ni madogo sema lugha hata mimi nlimwambia sababu una sare zako nakuacha ila ungekuwa kitaa ningekifumua nkasepa
Mkuu kwa mara ya kwanza leo naomba kutofautiana na wewe!!Ni kwamba hao polisi wamemkuta hapo mwanajeshi akiwa anatoa pesa. Sidhani kama kuna mtu anaweza kukuta maafisa wa bank na polisi wanaweka pesa akalazimisha kuingia. Mbona hata wanajeshi wakikuta kuna mtu ndani anachukua fedha wana simama kwenye foleni kusubiri? Labda huwajui polisi na mikwala yao ya hovyo
Nakubaliana nawe kabisa, lakini sio kufika na kumtoa mtu ndani kama mhalifu huku umemuelekezea bunduki. Kumbuka huyo mwanajeshi ni train soldier na anaelewa madhara ya kuelekezewa bunduki na reaction yake ni pap hadi ikamshangaza mshika bundukiMkuu kwa mara ya kwanza leo naomba kutofautiana na wewe!!
Mwanajeshi hayuko juu ya sheria... Wakati wa kuweka hizo pesa hatakiwi kuwepo mtu pale. Kazi hiyo ni ya hatari hivyo inatakiwa kufanyika kwa haraka, inaweza kuwa kuna majambazi yanafanya timing tu msimame pale yalenge shabaha na kuondoka na fedha, hivyo hawawezi kumsubiria mtu mpaka amalize kazi zake ndipo waweke. Huyo mwanajeshi alitakiwa kucancel transaction na kuondoka pale haraka na sio kutaka abembelezwe kama alivyodai... Pale kuondoka ni amri sio ombi.
By the way mkuu, wengi humu mnatetea mwanajeshi kwa kudhani kuwa ndio friendly na raia, si kweli... Kwa nchi ya Tanzania polisi na wanajeshi ni walewale tu, ukitaka kuamini, watu waandamane tarehe 26, polisi wazidiwe uone kama wanajeshi hawajaingia barabarani kupiga r
Askari wetu lishe ndogo hawana mazoezi.duuu, hapo ndo ujue kuwa weled ktk jeshi letu la polisi hamna kabisa, pia ata mwanajeshi hakuwa na hekima hata kidogo na anatakiwa kuadhibiwa vikali, haiwezekan umeshapewa tahadhali ya kutoka eneo hilo na unaona kabisa kitu kinachoendelea kwa mjibu wa sheria na kiusalama, halafu ww unadinda eti kisa ww ni mwanajeshi yaan alishindwa kutambua kwamba hapo kuna tukio linalohitaji usalama zaid, na alikosea zaid alipoishika silaha ya afande kama ni kweli, hapa polisi walitakiwa wamkamate kwa nguvu then wampe kichapo cha mbwamwitu ili ajue kuwa kaingia cha kike, askali aliyerusha risasi hakutumia weled wa kazi.
Hilo la maandamano tuliache hapa, ila kumbuka Misri walifanyajeMkuu kwa mara ya kwanza leo naomba kutofautiana na wewe!!
Mwanajeshi hayuko juu ya sheria... Wakati wa kuweka hizo pesa hatakiwi kuwepo mtu pale. Kazi hiyo ni ya hatari hivyo inatakiwa kufanyika kwa haraka, inaweza kuwa kuna majambazi yanafanya timing tu msimame pale yalenge shabaha na kuondoka na fedha, hivyo hawawezi kumsubiria mtu mpaka amalize kazi zake ndipo waweke. Huyo mwanajeshi alitakiwa kucancel transaction na kuondoka pale haraka na sio kutaka abembelezwe kama alivyodai... Pale kuondoka ni amri sio ombi.
By the way mkuu, wengi humu mnatetea mwanajeshi kwa kudhani kuwa ndio friendly na raia, si kweli... Kwa nchi ya Tanzania polisi na wanajeshi ni walewale tu, ukitaka kuamini, watu waandamane tarehe 26, polisi wazidiwe uone kama wanajeshi hawajaingia barabarani kupiga r
Hilo la maandamano tuliache hapa, ila kumbuka Misri walifanyajeMkuu kwa mara ya kwanza leo naomba kutofautiana na wewe!!
Mwanajeshi hayuko juu ya sheria... Wakati wa kuweka hizo pesa hatakiwi kuwepo mtu pale. Kazi hiyo ni ya hatari hivyo inatakiwa kufanyika kwa haraka, inaweza kuwa kuna majambazi yanafanya timing tu msimame pale yalenge shabaha na kuondoka na fedha, hivyo hawawezi kumsubiria mtu mpaka amalize kazi zake ndipo waweke. Huyo mwanajeshi alitakiwa kucancel transaction na kuondoka pale haraka na sio kutaka abembelezwe kama alivyodai... Pale kuondoka ni amri sio ombi.
By the way mkuu, wengi humu mnatetea mwanajeshi kwa kudhani kuwa ndio friendly na raia, si kweli... Kwa nchi ya Tanzania polisi na wanajeshi ni walewale tu, ukitaka kuamini, watu waandamane tarehe 26, polisi wazidiwe uone kama wanajeshi hawajaingia barabarani kupiga r
Nashangaa wanaowatetea sana hawa wanajeshi, nao ni waonevu tu kwa raia sawa tu na hao polisi, wanajeshi hawachelewi kupiga raia kwenye mtaa flani kisa tu mwenzao kaporwa demu...@cc@Chakaza.Ila yeye wanajeshi anaweza kumwambia na kumfanya mtu upuuzi....
Kisa nini?
Hilo ni funzo kuwa wanavyowaonea raia mtaani wajuwe kuwa wanaumia vile vile
Walikutana mwenye lugha mbovu na mwenye vitendo viovu!
Sawa, turudi kwenye mada, alitakiwa kucancel transaction na kuondoka haraka, ni amri, sio ombi..Hilo la maandamano tuliache hapa, ila kumbuka Misri walifanyaje
Hapana, aliambiwa atoweke, yeye akadinda na kudai aambiwe "kistaarabu", Ndipo wakamuelekezea mtutu...Nakubaliana nawe kabisa, lakini sio kufika na kumtoa mtu ndani kama mhalifu huku umemuelekezea bunduki. Kumbuka huyo mwanajeshi ni train soldier na anaelewa madhara ya kuelekezewa bunduki na reaction yake ni pap hadi ikamshangaza mshika bunduki
Kifo cha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Konstebo Kulwa Gilbert, aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake, kimezua mshtuko kwa ndugu, jamaa, askari wenzake na majirani aliokuwa akiishi nao nyumbani kwake, Ukonga-Mazizini jijini Dar, Gazeti la Uwazi pekee ndilo lenye mkasa mzima wa tukio hilo.
NI SINZA JIJINI DAR
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea Jumanne ya wiki iliyopita, majira ya jioni wakati afande Kulwa na FFU wenzake wakiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi wakishusha pesa kwa ajili ya kuziweka kwenye mashine ya ATM ya Benki ya CRDB iliyopo Sinza-Mori pembezoni mwa Kituo cha Mafuta cha Big Bon, jijini Dar.
Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Uwazi kuwa, wakati maafande hao wakiwa kwenye harakati za kushusha pesa hizo karibu na mashine hiyo, kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine hiyo hivyo afande Kulwa na wenzake walimuamrisha aondoke haraka eneo hilo kwa sababu za kiusalama.
MASHUHUDA WASIMULIA
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda hao, Jimmy Kaishozi, mkazi wa Sinza-Meeda, mwanajeshi huyo, baada ya kupewa amri ya kuondoka haraka eneo hilo, aliona kama amedharauliwa na askari hao hivyo aliwataka wamwambie kistaarabu na siyo kumwamrisha.
Kaishozi alisimulia kuwa, hali hiyo ilizua malumbano kati ya askari hao na mwanajeshi huyo ambapo Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea ambapo mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuwa alikuwa na utaalam wa masuala ya silaha.
“Kitendo hicho kilizidisha taharuki ambapo askari mwingine wa FFU naye alitoka kwenye gari lililokuwa limebeba pesa na bunduki nyingine na kumlenga mwanajeshi huyo, lakini katika hali iliyoonekana kama bahati mbaya, risasi hizo zilimpata afande Kulwa na nyingine ilimlenga mwanajeshi huyo.
“Hapo mapambano yalizidi kukolea kama sinema ya kivita ambapo askari aliyekuwa akilenga shabaha, alipoona amempiga mwenzake, aliikoki tena bunduki na kumpiga risasi nyingine mwanajeshi huyo ambapo afande Kulwa na mwanajeshi huyo, wote walianguka chini na kuanza kutapatapa huku wakitokwa na damu nyingi.
“Ilichukua muda wakigaragara chini hadi walipofika askari wa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) na kuwachukua, sijui walipelekwa wapi,” alisimulia Kaishozi.
KITUO CHA MABATINI
Hata hivyo, habari kutoka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ambapo mwandishi wetu alifika, baadhi ya polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakisema kuwa majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wakiwa njiani afande Kulwa aliaga dunia.
MAKAO MAKUU FFU
Mwandishi wetu pia alikwenda Makao Makuu ya Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga-Madafu jijini Dar ambapo aliwakuta askari wenzake marehemu ambao walionesha hisia za majonzi wakati wakizungumzia kifo cha mwenzao huyo.
Askari hao hawakuwa tayari kuandikwa majina kwa maelezo kuwa hawaruhusiwi ambapo walimwelekeza mwandishi wetu nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mazizini jijini Dar.
NYUMBANI KWA MAREHEMU
Mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa marehemu, lakini alikuta chumba chake kimefungwa ambapo mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema kuwa, msiba ulihamishiwa Tazara-Mchicha kwa dada yake aitwae Doto ambaye ndiye pacha wake.
Mwandishi wetu alizungumza na majirani aliowakuta eneo hilo ambao walisema kuwa, kifo hicho kilisababisha mshtuko mkubwa mtaani hapo na kuibua majonzi makubwa.
Kutokana na afande huyo kuishi vizuri na majirani zake, mwandishi wetu aliwakuta wakiendelea kuchangisha pesa za rambirambi huku wakiwa na picha ya marehemu.
ACP Muliro Jumanne Muliro.
UJIJI, KIGOMA KWA MAZISHI
Mwanahabari wetu pia alifika alipoelekezwa ulipokuwa msiba huo, lakini alipofika alikuta tayari mwili wa marehemu ulishasafirishwa kupelekwa kijijini kwao, Ujiji mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.
MWANAJESHI MUHIMBILI
Habari kutoka Muhimbili zilidai kuwa mwanajeshi aliyepata kisanga hicho yeye anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo japokuwa hakuna afisa habari yeyote katika hospitali hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.
“Ni kweli huyo mwanajeshi yupo, lakini chini ya ulinzi mkali, itakuwa vigumu ninyi kumuona,” alisema mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini hospitalini hapo.
KAMANDA MAMBOSASA
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema angempigia mwandishi baadaye.
KAMANDA MULIRO
Mwandishi aliamua kumpigia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro na alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema ni vema kuzungumza na Kamanda wa Kanda Maalum.
“Ndugu yangu si unajua kuwa kuna Kamanda wa Kanda Maalum? Mpigie yeye,” alisema Kamanda Muliro.
Alipoambiwa amepigiwa hajajibu swali ndiyo maana akapigiwa yeye RPC, Muliro alisema atampigia yeye Mambosasa.
Mwandishi alimpigia simu tena Kamanda Mambosasa na kumueleza kuhusiana na tukio hilo ndipo akasema yupo chumba cha daktari na akaahidi kumpigia mwandishi baadaye.
MSEMAJI WA POLISI
Hata hivyo, ili kupata undani wa tukio hilo, pia Uwazi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Barnabasi Mwakalukwa na kumuuliza juu ya taarifa za tukio hilo ambapo aliomba atafutwe Kamanda Mambosasa.
“Hilo jambo anayepaswa kulizungumzia ni Kamanda Mambosasa, mtafuteni huyo,” alisema Kamanda Mwakalukwa.
UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.
Haikujulikana mara moja kama polisi aliyempiga risasi mwenzake pamoja na mwanajeshi huyo kama amekamatwa au la.
KUMRADHI
Jina la Konstebo Justine Mtesigwa, ambalo awali lilitumika kwenye habari hii kwenye gazeti la Uwazi leo kwamba ndiye aliyeuawa lilikosewa, jina sahihi ya aliyeuawa ni konstebo Kulwa Gilbert. Justine na Kulwa walikuwa ni marafafiki na walikuwa wakifanyakazi pamoja Ukonga. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa Justine, ndugu, jamaa, marafiki na wafanayakazi wenzake – Mhariri.
Stori: Richard Bukos, Dar.
My Take;
Polisi wawili kupambana na Mwanajeshi mmoja asiye na silaha na kuishia kuuana wenyewe ni picha kuwa hawa wanahitaji mafunzo ya uhakika ili unyonge wao wasiutumie kuwaonea raia wasio hatia
Siku utatukaniwa mama yako mzazi na jamaa ndo utakuja kurudi kuanzisha thread humu mimi yamenikutaga hata kama unatoa amri si kwa maneno machafu na hapa yote yametokea haya sababu ya lugha chafu na mimi nawajua jamaa wakiwa na sare na bunduki huwaambii kituSawa, turudi kwenye mada, alitakiwa kucancel transaction na kuondoka haraka, ni amri, sio ombi..
Je, ni kweli kwamba askari akipeleka fedha kwenye ATM analazimika kumfukuza mteja anayemkuta kwenye ATM husika au ndiyo kiherehere cha Jungle Green kufanya kazi zisizowahusu...
So far wenye pesa zao (i mean banks) wao huwa wanaamini kwamba fedha siyo muhimu kama uhai maana fedha zao zimekatiwa bima lakini hawa wanausalama wetu kwa kutaka masifa sometimes wana-exaggerate sana security issues wanaposafirisha fedha na kuzichukulia kiujiko ujiko sana. Sioni logic ya kumsogelea adui kiasi kile, kama alikuwa mwanajeshi chambo kuna uwezekano hata fedha zingeondoka na wakora pia na uhai wa wanausalama wetu wote ungekuwa mashakani.
Pole kwa wafiwa, ila kwa waliobaki hapo FFU Ukonga wajifunze kupitia kosa la mwenzao, unless otherwise death was calling him but the policemen did was wrong.
Unayedhani mjinga yupo hai.Hao wenye akili mmoja kalazwa chini.Wana Jamvi,
Katika Utaratibu wa aina yoyote Kiutendaji intendaji lazima discipline izingatiwe.
Mwanajeshi ni Mtu alipewa dhamana ya nchi hii, hivyo anapaswa kuwa mwadilifu na mwenue adabu katika kila jambo.
Aliona wale wakiwa katika utendaji na anajua wazi ubebaji na usafirishaji wa pesa ni kitu cha hatari isipokuwa tu kwa sababu mwanajeshi ni mkaidi mjinga asiejua mchango wake kwa taiga haya yote yametokea kwa ajili yake.
Kama lilikuea no swala la kudharauliwa angetii amri FFU wamalize kazi yao kisha awaulize madai take.
Anastaili kushtakiwa. Charge 1distortion or causing commotion to a working team causing them fail to render their services as carriage and preventive officers 2 causing death kama sheria zipo Tanzania na wanasheria wapo, Huyo! Wapeleke ukonga.
Hilo la kutukaniwa mama yako siyo sahihi, ila wakiwa na sare na bunduki ni kweli hutakiwi 'kuwaambia kitu', na wala hutakiwi kuwasogelea.. Ukikaidi amri katika maeneo ya hatari kama wakati wa kusindikiza pesa au kuweka pesa anashauriwa akutandike shaba, kwa ajili ya usalama wa maisha yake.. Kulwa alichelewa kumtandika shaba huyo mwanajeshi, matokeo yake kapoteza maisha yeye!Siku utatukaniwa mama yako mzazi na jamaa ndo utakuja kurudi kuanzisha thread humu mimi yamenikutaga hata kama unatoa amri si kwa maneno machafu na hapa yote yametokea haya sababu ya lugha chafu na mimi nawajua jamaa wakiwa na sare na bunduki huwaambii kitu
Hilo la mjinga na mwenye akili tuliache kwanza, ila alichofanya askari wa JWTZ ni aibu kwa jeshi, anatakiwa achukuliwe hatua, ila kulindana pia bado kupo, inaweza ikapotezewa kimya kimya au jeshi likamkana kuwa siyo mtu wetu, na kumficha mahali..Unayedhani mjinga yupo hai.Hao wenye akili mmoja kalazwa chini.