Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Mie nitasema kitu kimoja kwa Askari Polisi wetu, waache ubabe.. Magwanda wanayovaa na silaha wanazoshika zisiwape kiburi na kuacha kutumia hekima na busara.. Wawe wanaongea na kuelekeza bila ya kuwawekea raia kibesi.. Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, marehemu hakutumia kauli ya kibusara katika kumuelekeza huyo askari wa JWTZ.. Naamini angetumia kauli ya busara, basi angekuwa bado yupo hai.. Nimeshaona na mwenyewe kukutana na kauli za kibabe na kutisha toka kwa hawa Askari wetu..
 
duuu, hapo ndo ujue kuwa weled ktk jeshi letu la polisi hamna kabisa, pia ata mwanajeshi hakuwa na hekima hata kidogo na anatakiwa kuadhibiwa vikali, haiwezekan umeshapewa tahadhali ya kutoka eneo hilo na unaona kabisa kitu kinachoendelea kwa mjibu wa sheria na kiusalama, halafu ww unadinda eti kisa ww ni mwanajeshi yaan alishindwa kutambua kwamba hapo kuna tukio linalohitaji usalama zaid, na alikosea zaid alipoishika silaha ya afande kama ni kweli, hapa polisi walitakiwa wamkamate kwa nguvu then wampe kichapo cha mbwamwitu ili ajue kuwa kaingia cha kike, askali aliyerusha risasi hakutumia weled wa kazi.
Nadhani utakuwa umechanganya vitu au ni mmoja wa kundi lile.

Dereva wa treni akipita kwenye barabara haina tabu, ila akiamua kuipitisha treni barabara ya magari itakuwa ajabu.

Huwezi kuelekeza silaha ya moto kwa mtu asiye na silaha hata silaha baridi. Yuko mmoja, mko wengi, maneno yakufanye uoneshe nia ya kutumia silaha?

Zaidi, kwakuwa mjeda alijua kuwa jamaa akili zao huwa wanaziacha nyumbani baada ya kuvaa yunifomu, aliamua kuokoa nafsi yake na raia wengine kwa kuelekeze silaha juu.

Na askari gani unashindwa kulenga tageti? Au ndo mambo ya ilikata kona na kumpiga wa kwake?

Si ajabu yuke mwanafunzi kwenda na moto, akili zenu si ndo hizi!
 
Kifo cha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Konstebo Kulwa Gilbert, aliyepigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake, kimezua mshtuko kwa ndugu, jamaa, askari wenzake na majirani aliokuwa akiishi nao nyumbani kwake, Ukonga-Mazizini jijini Dar, Gazeti la Uwazi pekee ndilo lenye mkasa mzima wa tukio hilo.

NI SINZA JIJINI DAR
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea Jumanne ya wiki iliyopita, majira ya jioni wakati afande Kulwa na FFU wenzake wakiwa na askari wa kampuni binafsi ya ulinzi wakishusha pesa kwa ajili ya kuziweka kwenye mashine ya ATM ya Benki ya CRDB iliyopo Sinza-Mori pembezoni mwa Kituo cha Mafuta cha Big Bon, jijini Dar.

Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia Uwazi kuwa, wakati maafande hao wakiwa kwenye harakati za kushusha pesa hizo karibu na mashine hiyo, kulikuwa na askari wa JWTZ aliyekuwa akitaka kutoa pesa kwenye mashine hiyo hivyo afande Kulwa na wenzake walimuamrisha aondoke haraka eneo hilo kwa sababu za kiusalama.

MASHUHUDA WASIMULIA
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda hao, Jimmy Kaishozi, mkazi wa Sinza-Meeda, mwanajeshi huyo, baada ya kupewa amri ya kuondoka haraka eneo hilo, aliona kama amedharauliwa na askari hao hivyo aliwataka wamwambie kistaarabu na siyo kumwamrisha.

Kaishozi alisimulia kuwa, hali hiyo ilizua malumbano kati ya askari hao na mwanajeshi huyo ambapo Kulwa alimfuata jamaa huyo akiwa na bunduki mkononi huku akimuelekezea ambapo mwanajeshi huyo aliikamata na kuelekezea mtutu juu, jambo lililoonekana kuwa alikuwa na utaalam wa masuala ya silaha.

“Kitendo hicho kilizidisha taharuki ambapo askari mwingine wa FFU naye alitoka kwenye gari lililokuwa limebeba pesa na bunduki nyingine na kumlenga mwanajeshi huyo, lakini katika hali iliyoonekana kama bahati mbaya, risasi hizo zilimpata afande Kulwa na nyingine ilimlenga mwanajeshi huyo.

“Hapo mapambano yalizidi kukolea kama sinema ya kivita ambapo askari aliyekuwa akilenga shabaha, alipoona amempiga mwenzake, aliikoki tena bunduki na kumpiga risasi nyingine mwanajeshi huyo ambapo afande Kulwa na mwanajeshi huyo, wote walianguka chini na kuanza kutapatapa huku wakitokwa na damu nyingi.

“Ilichukua muda wakigaragara chini hadi walipofika askari wa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) na kuwachukua, sijui walipelekwa wapi,” alisimulia Kaishozi.

KITUO CHA MABATINI
Hata hivyo, habari kutoka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ambapo mwandishi wetu alifika, baadhi ya polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, wakisema kuwa majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wakiwa njiani afande Kulwa aliaga dunia.

MAKAO MAKUU FFU
Mwandishi wetu pia alikwenda Makao Makuu ya Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), Ukonga-Madafu jijini Dar ambapo aliwakuta askari wenzake marehemu ambao walionesha hisia za majonzi wakati wakizungumzia kifo cha mwenzao huyo.

Askari hao hawakuwa tayari kuandikwa majina kwa maelezo kuwa hawaruhusiwi ambapo walimwelekeza mwandishi wetu nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mazizini jijini Dar.

NYUMBANI KWA MAREHEMU
Mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa marehemu, lakini alikuta chumba chake kimefungwa ambapo mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema kuwa, msiba ulihamishiwa Tazara-Mchicha kwa dada yake aitwae Doto ambaye ndiye pacha wake.

Mwandishi wetu alizungumza na majirani aliowakuta eneo hilo ambao walisema kuwa, kifo hicho kilisababisha mshtuko mkubwa mtaani hapo na kuibua majonzi makubwa.
Kutokana na afande huyo kuishi vizuri na majirani zake, mwandishi wetu aliwakuta wakiendelea kuchangisha pesa za rambirambi huku wakiwa na picha ya marehemu.
ACP Muliro Jumanne Muliro.

UJIJI, KIGOMA KWA MAZISHI
Mwanahabari wetu pia alifika alipoelekezwa ulipokuwa msiba huo, lakini alipofika alikuta tayari mwili wa marehemu ulishasafirishwa kupelekwa kijijini kwao, Ujiji mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

MWANAJESHI MUHIMBILI
Habari kutoka Muhimbili zilidai kuwa mwanajeshi aliyepata kisanga hicho yeye anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo japokuwa hakuna afisa habari yeyote katika hospitali hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo.

“Ni kweli huyo mwanajeshi yupo, lakini chini ya ulinzi mkali, itakuwa vigumu ninyi kumuona,” alisema mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini hospitalini hapo.

KAMANDA MAMBOSASA
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema angempigia mwandishi baadaye.

KAMANDA MULIRO
Mwandishi aliamua kumpigia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Muliro Jumanne Muliro na alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema ni vema kuzungumza na Kamanda wa Kanda Maalum.

“Ndugu yangu si unajua kuwa kuna Kamanda wa Kanda Maalum? Mpigie yeye,” alisema Kamanda Muliro.

Alipoambiwa amepigiwa hajajibu swali ndiyo maana akapigiwa yeye RPC, Muliro alisema atampigia yeye Mambosasa.

Mwandishi alimpigia simu tena Kamanda Mambosasa na kumueleza kuhusiana na tukio hilo ndipo akasema yupo chumba cha daktari na akaahidi kumpigia mwandishi baadaye.

MSEMAJI WA POLISI
Hata hivyo, ili kupata undani wa tukio hilo, pia Uwazi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Barnabasi Mwakalukwa na kumuuliza juu ya taarifa za tukio hilo ambapo aliomba atafutwe Kamanda Mambosasa.

“Hilo jambo anayepaswa kulizungumzia ni Kamanda Mambosasa, mtafuteni huyo,” alisema Kamanda Mwakalukwa.

UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.

Haikujulikana mara moja kama polisi aliyempiga risasi mwenzake pamoja na mwanajeshi huyo kama amekamatwa au la.

KUMRADHI
Jina la Konstebo Justine Mtesigwa, ambalo awali lilitumika kwenye habari hii kwenye gazeti la Uwazi leo kwamba ndiye aliyeuawa lilikosewa, jina sahihi ya aliyeuawa ni konstebo Kulwa Gilbert. Justine na Kulwa walikuwa ni marafafiki na walikuwa wakifanyakazi pamoja Ukonga. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa Justine, ndugu, jamaa, marafiki na wafanayakazi wenzake – Mhariri.

Stori: Richard Bukos, Dar.

My Take;
Polisi wawili kupambana na Mwanajeshi mmoja asiye na silaha na kuishia kuuana wenyewe ni picha kuwa hawa wanahitaji mafunzo ya uhakika ili unyonge wao wasiutumie kuwaonea raia wasio hatia
Wana Jamvi,
Katika Utaratibu wa aina yoyote Kiutendaji intendaji lazima discipline izingatiwe.
Mwanajeshi ni Mtu alipewa dhamana ya nchi hii, hivyo anapaswa kuwa mwadilifu na mwenue adabu katika kila jambo.
Aliona wale wakiwa katika utendaji na anajua wazi ubebaji na usafirishaji wa pesa ni kitu cha hatari isipokuwa tu kwa sababu mwanajeshi ni mkaidi mjinga asiejua mchango wake kwa taiga haya yote yametokea kwa ajili yake.
Kama lilikuea no swala la kudharauliwa angetii amri FFU wamalize kazi yao kisha awaulize madai take.
Anastaili kushtakiwa. Charge 1distortion or causing commotion to a working team causing them fail to render their services as carriage and preventive officers 2 causing death kama sheria zipo Tanzania na wanasheria wapo, Huyo! Wapeleke ukonga.
 
TUNASHUKURU KAMA HUYO Mwanajeshi yuko salama

Polisi, alishndwaje kuvumilia jamaa atoe hela kwa sababu ni kitendo cha dakika moja tu

Halafu sheria ya bunduki, usikwoneshe mtu ambaye huna nia ya kumpiga risasi
Utawezaje kutoa pesa ATM wakati wanaweka ,,, Elimu muhimu sana si kwa majeshi tu Bali kwa jamii nzima .
 
Huwezi kuwa na Busara kama huna elimu. Tuangalie wapi kuna makosa parekebishwe na siyo kutoa kawama.

Pole sana mwanajeshi
 
Huyu mwanajeshi ni hodari wa kujikinga.
Nahisi aliona mfyatua risasi anamlenga kisha akamuweka polisi kama kinga.
Polisi haruhusiwi kufyatua risasi kwa mtu ambaye hana silaha.
Ingetokea mwanajeshi amemnyang'anya polisi silaha na kutaka kuitumia kupiga, polisi angekuwa na haki ya
kutumia silaha yake.
Kuna mapungufu makubwa sana kwa polisi wetu katika kanuni za kutumia silaha za moto wakati wa matukio madogo.
 
Siwezi kumlaumu polisi au mwanajeshi kwakuwa sijashuhudia tukio.

Lakini nakumbuka wiki iliyopita nilienda kwenye ATM moja pale makumbusho sikujua kama ndani wanaweka hela, ile nasogea tu nikaambiwa na askari "toka, pita kule usisogee hapa" kwa ukali na lugha nyingine zisizoelezeka huku ameninyooshea bunduki.
Kila mteja aliyekuja pale alipatwa na kadhia hyo.

Tunaomba askari wetu wawe na lugha nzuri kwa raia, utanitukanaje wakati sijajua kama ndani wanaweka hela, si uniambie tu kwa kawaida?
Na je unavyoninyooshea bunduki risasi ikitoka ikanipata utasema ni bahati mbaya au Mimi ni jambazi? Mjitafakari nyie polisi.
 
Muandishi wa mada ameandika vizuri sana na mada inaeleweka,nimeupenda uandishi wake,

Pole kwa wafiwa na majeruhi Mungu awasaidie wapone majeraha yao,pia uchunguzi ufanyike ili kujua kilichotokea ni nini hasa ili kujaribu kuzuwia kitendo kama hicho kisije kujirudia tena.
Amekopi gazetini
 
maelekezo ya kipuuzi na ya kibabe ndio chanzo cha yote haya.walioendelea wanatenda kama hii mipuuzi yetu ? sio wote namaanisha baadhi ya mipuuzi yetu !!
 
duuu, hapo ndo ujue kuwa weled ktk jeshi letu la polisi hamna kabisa, pia ata mwanajeshi hakuwa na hekima hata kidogo na anatakiwa kuadhibiwa vikali, haiwezekan umeshapewa tahadhali ya kutoka eneo hilo na unaona kabisa kitu kinachoendelea kwa mjibu wa sheria na kiusalama, halafu ww unadinda eti kisa ww ni mwanajeshi yaan alishindwa kutambua kwamba hapo kuna tukio linalohitaji usalama zaid, na alikosea zaid alipoishika silaha ya afande kama ni kweli, hapa polisi walitakiwa wamkamate kwa nguvu then wampe kichapo cha mbwamwitu ili ajue kuwa kaingia cha kike, askali aliyerusha risasi hakutumia weled wa kazi.
Wewe ni Polisi?
 
Mie nitasema kitu kimoja kwa Askari Polisi wetu, waache ubabe.. Magwanda wanayovaa na silaha wanazoshika zisiwape kiburi na kuacha kutumia hekima na busara.. Wawe wanaongea na kuelekeza bila ya kuwawekea raia kibesi.. Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, marehemu hakutumia kauli ya kibusara katika kumuelekeza huyo askari wa JWTZ.. Naamini angetumia kauli ya busara, basi angekuwa bado yupo hai.. Nimeshaona na mwenyewe kukutana na kauli za kibabe na kutisha toka kwa hawa Askari wetu..
Hawa ndo wale walikuwa kwenye lile kundi lililotembeza kichapo kwa raia maeneo ya ukonga
 
Back
Top Bottom