Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Hii inaonyesha askari Polisi hawana mafunzo ya kutosha ya matumizi ya silaha. Ndio maana ni vituko tuu kama tulivyoona kwa Malima, kule Morogoro au hata kwa Akwilina
Una smg unamsogelea adui kiasi cha kukamata silaha yako? Kabla ya kumfuata kwanini hakumtaarifu mwenzie?
 
Hahahaaa...never happen hiyo mkuu, mtu hata kumlenga adui kashindwa kaishia kuua mwenzake!
Unaona police na mjeda wamekwidana si angemwita soja kishikaji halo braza mwachie tu
 
UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.

Mkuu kabisa kanda maalum anaongea hiyo kauli,,, hivi unawezaje kudhani ni jambazi? kwa ishara gani aliyoionesha huyo mwanajeshi?
 
Maaskari wawili wenye silaha wameshindwa kumthibiti mwanajeshi na kupelekea askari mmoja kupoteza maisha

Maafande watofautishe mafunzo ya ccp na monduli
Haya mambo ya kuleta ujuaji mwisho unaishia pabaya...huyo mjeda anajifanya mwamba usikute hapo atm alikuwa anatoa buku 10 tu
Nimesikitishwa sana na michango ya watu wengi kuhusu hili suala, hata baadhi ya watu ninaowaheshimu kabisa hapa jamvini.. Wengi wanampendelea mwanajeshi na kumponda polisi, labda ni kwa sababu ya kuwachukia tu polisi, uhalisia unawekwa pembeni, ni hivi wakuu, wakati huo wa kuweka pesa, hakuna mtu anaruhusiwa kuwepo eneo hilo, hata kama ni mwanajeshi, kwani mwanajeshi sio binadamu? Hawezi kupora pesa na kutokomea nazo? Wakati wa tukio hilo amri ni moja tu, anaekaidi anatakiwa kuchukuliwa hatua mapema, maana anaweza akawa jambazi, majambazi wengi wamefanya uharifu wakiwa na uniform...

Hata hivyo, ninakubali hoja moja, polisi hawana weledi mzuri, hakutakiwa kumsogolea katika kiasi cha yeye kuishika silaha, alitakiwa amtandike risasi akiwa mbali... Huyo mwanajeshi anatakiwa afukuzwe kazi na apelekwe mahamani.
 
Mimi naona jeshi la polisi niamie kwenye kusaidia trafk light tu silaha wanaona kumnyooshea mtu ni sifa au kumtisha sasa mjeshi mlinda amani anaendelea poa Afande kadanja kumbe kifo chake kilikuwa kinatafuta sababu tu. Pole kamanda mjeshi.
 
we nae ndo hamna kitu kabisa... ungeonekana wa maana sana kama ungetoa ushauri kwa chuo cha mafunzo polisi warekebishe masomo yao hasa nidhamu,silaha na utambuzi.
 
Upo sshihi mkuu
 
Maisha ni ya ajabu sana! Yaani "vitu" vimekua na thamani kubwa kuliko uhai wa binadamu!
 

Yote haya chanzo ni mhutu !

Viburi na utumiaji wa mabavu wa askari ni kutokujua mipaka yao na ujinga wa wananchi
 
Mwanajeshi alikuwa na sare au la? hata hivyo alipaswa kutii amri iliyotolewa! nasikia aliesababisha hayo anashitakiwa kwa kusababisha kifo!! jamani hizi kazi busara muhimu!!
Kutii amri kuna style tofauti kwa mfano:
"Wewe toka hapo ilo sio eneo la kusimama"
Na.
Habari yako ! Hapa haparuhusiwi kusimama ni eneo la benk.
Hapo wewe unatii ipi mkuu ?
 
we nae ndo hamna kitu kabisa... ungeonekana wa maana sana kama ungetoa ushauri kwa chuo cha mafunzo polisi warekebishe masomo yao hasa nidhamu,silaha na utambuzi.
Niwashauri chuo cha polisi au jeshi?! Aliyetakiwa kuwa na nidhamu na utambuzi hapo ni nani kati ya polisi na mwanajeshi?
 
Pole nyingi zikufikie mwanajeshi...
Hao wapuuzi wanafikiri kila mtu ni Nape.
Mola akujalie wepesi kwenye majeraha uliyo pata.
NB:Wanajeshi naomba muwashughulikie hao wahuni wanao tumia vibaya bunduki zao.
 
Ndo maana UN walisema kuna mapungufu katika mafunzo na vijana wa jwtz hili swala inatakiwa liangaliwe kwa jicho pevu sana

Hili tukio limitufumbua macho nidhamu ya vijana wetu wa jwtz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…