Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Leo Rais hawezi kuingilia mchakato wa mahakama? Kwani walioko Magerezani na mahabusu walipitishwa hata mahakama. kama wangepata hata fursa za mahakamni ingekuwa nafuu. wengi walifungwa kwa maagizo kutoka juu.
 
Jifanyeni kuidanganya Dunia ila sisi tunajua kuna Mamia ya Wafungwa wa kisiasa waliolundikwa kwenye Magereza na kubambikiwa Kesi

Nasema ni Mamia.
 
Mama alisema kesi ambazo hazina ushahidi zitafutwa,hata kama ni ya kisiasa haina ushahidi itafutwa.

Ni kweli mkuu mfano kesi iliyoamuliwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu ktk Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

5 May 2021

HALIMA MDEE NA WENZAKE WAFUTIWA KESI KISUTU, ILE YA KUVUNJA GETI LA SEGEREA "NINA WAACHIA HURU WOTE"





Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru viongozi na wafuasi 27 wa CHADEMA waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko na kuvunja geti la gereza la Segerea. Kesi hiyo imefutwa leo Mei 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Upande wa Mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamani. Kesi hiyo iliitwa leo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wakili wa Serikali, Ester Martin kudai mahakamani hapo kuwa kuwa kwa leo hawana shaidi hivyo wameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine ya kusikilizwa. Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala na Edson Kilatu walipinga kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuiomba mahakama kuifuta kwa kuwa upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi kwa muda mrefu. Katika uamuzi wake Hakimu Shaidi amesema; "Kesi hii imeshakuwa na maahirisho kwa muda mrefu hivyo ninawaachia huru washtakiwa wote chini ya kifungu cha 225(5)". Hata hivyo kifungo hicho kinawapa mamlaka jeshi la polisi kuwakamata tena washtakiwa pale wanapokamilisha ushahidi. Walioachiwa ni Wabunge Halima Mdee(41), Ester Bulaya(40) na Jesca Kishoa( 36). Boniface Jacob, Patrick Assenga, Henry Kilewo,Yohana Kaunya,Kedmony Mhembo, Mshewa Karua, Khadija Mwago, Pendo Raphael maarufu kama Mwasomola na mkazi wa Bonyokwa, Cesilia Michael, Happy Abdalla; Stephen Kitomali na Paul Makali, Edgar Adelinj na Reginald Masawe Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kutoa lugha ya kuudhi kuharibu Mali; kufanya mkusanyiko usio kuwa wa halali na kutokutii amri halali iliyowekwa na Jeshi la Magereza na shambulio. Inadaiwa, Machi 13, 2020 , eneo la gereza la Segerea, lililopo wilaya ya Ilala, kwa makusudi washtakiwa walikaidi amri halali ya kuondoka eneo la gereza kwa amani ili eneo hilo libaki wazi, amri hiyo iliyotolewa na askari mwenye namba B 3648, Sajenti John ambaye ni mlinzi wa Geti la gereza hilo. Katika shtaka pili ambalo ni la kufanya mkusanyiko, washtakiwa wanadaiwa kukusanyika isivyo halali kwenye geti la Gereza la Segerea na kusababisha hofu iliyokuwa inapelekea uvunjifu wa amani na utulivu. Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuharibu geti kuu la kuingilia na kutokea katika gereza la Segerea mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia huku Mdee, Bulaya na Jacob wakidaiwa kutoa lugha ya matusi kwa askari Magereza mwenye namba B 3648, Sajent John.
 

4 May 2021​

Haki Africa appeals to Pres. Samia Suluhu Hassan to release activists arrested in Tanzania​


Source : Kenya CitizenzTv
Haki Africa appeals to Pres. Suluhu to release activists arrested in Tanzania Lobby group claims activists have been held for long without charges
Civil society actors drawn from Kenya, Uganda and Tanzania have implored Tanzania’s President Samia Suluhu Hassan to release more than 100 human rights activists, journalists and political prisoners incarcerated by the previous regime for criticising the 2020 general election.

The Haki Africa human rights group that made the statement on behalf of their colleagues in the region acknowledged the move by President Suluhu to pardon 5,000 prisoners last week, stating that notable human rights defenders are still languishing in correctional facilities.

“We acknowledge your stature as a progressive leader to the People of Tanzania, East Africa and Africa at large. As civil society organizations, we have confidence and faith in your leadership and the good example you continue to set. Your Excellency, we African civil society actors from all walks of life, view the citizens of the United Republic of Tanzania as our brothers and sisters,” read the statement released on Tuesday.

“We affirm that any concern arising from your country is our collective concern. From the interactions, reports and media highlights, we have come to learn and appreciate your recent move to release over 5,000 prisoners from prison, some of who were detained during the recently concluded electoral process in Tanzania. Indeed, you have shown the way for other African leaders to follow.”

According to Haki Africa, there are at least 100 known human rights defenders, journalists and political activists still being detained over the last election.

“…from our partners in Tanzania, we have come to learn that, there may still be others including human rights defenders, journalists and political activists, who may still be incarcerated in prisons across Tanzania. It is our belief that they too were arrested in relation to Tanzania’s 2020 general elections. Attached is a list of about 100 who we fear may still be held in prisons,” they stated.


“Through this statement, we appeal to you, first as a mother, secondly as a civil society colleague and thirdly as the President of the United Republic of Tanzania, to consider releasing and or pardoning them. This request is keeping in-line with your government’s commitment to fulfill its obligations under international laws and statutes guarding human rights, rule of law and democracy.”
 
Kwa hiyo kaongopa kwa niaba ya kipenzi chako?

..ulitegemea msemaji wa serikali akiri kwamba Mama Samia ameamuru waliokamatwa kwa sababu za kisiasa waachiwe?

..its about time ccm iache kutumia vyombo vya ulinzi na mahakama kisiasa. Waache vyombo hivyo vitekeleze majukumu yake bila upendeleo.
 
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amekana taarifa inayosambaa kwamba Rais Samia kawaachia huru Wafungwa 23 wa Kisiasa. Kadai Tanzania haina mfungwa wa kisiasa na kusema Rais hawezi kuingilia mchakato wowote wa Mahakama.

Awali chombo cha habari cha Kenya kiliripoti Rais Samia kuachilia wafungwa 23 wa kisiasa nchini.


Pia, soma: Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?
Ila ina wakimbizi wa kisiasa...!!!
Hivi wahanga kama kina Ben Saanane waliposhikiliwa kabla ya kupotezwa walipaswa kuitwaje?
 
Back
Top Bottom