Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Serikali inakosea sana kutoa vibali vya kufungua makanisa, ninaona ni bora iwe inashirikiana na taasisi zote za kikristo kusajili au kutoa kibali chochote e.g Tec,na umoja wa makanisa ya kipentekoste, kwa sababu kuna makanisa mengi sana ya kihuni yanaanzishwa.

Lazima kuandaliwe vigezo hata 100 vya kulisajili kanisa ili kuepukana na makanisa fake yenye mafundisho fake na maombi fake. Na hivyo vigezo viwe ni mchanganyiko vya umoja wa makanisa na serikali. La sivyo mpaka waganga wa kienyeji watafungua makanisa.

Huyo Suguye anajiita eti chief prophet, sijui alipatia wapi hicho cheo cha kujimwambafy, lazima kuwe na filter makini dhidi ya makanisa mapya, siku hizi hadi watu wachafu kama lgbt nao husajili makanisa yao ya geresha na haramu lazima kuwe na mchujo ili wasije nao tukawaona Tanzania
Kuna uhakiki wa taasisi zote za kidini unaendelea, kama hujakamlisha usajajili unastopishwa kwanza
 
Uyu si ndo aliekuwa anatuma kucha na nywele sas kanisa au kilinge kile
 
Udini awamu ya sita inatisha sana
Sio udini! Wanatakiwa wafunge yote Haya. Kutoka kucha na kunyoa nywele ndio nini? Kama kweli Wana neno la Mungu waende Ulaya ambapo Kuna pesa nyingi zaidi na makanisa yanafungwa. Waende wakawaokoe!
 
Ulimjua huyo dada kabla ama ulimuonea hapo hapo kanisani/kwenye runinga ?

Ndugu yangu usihadaike. Hawa ni wahuni tu Kama wahuni wengine. Huyo dada alikuwa kipofu wamchongo!!
Siandiki hapa kumfurahisha mtu au kujifurahisha, ninamjuwa fika huyo Dada amekuwa kipofu kwa miaka kadhaa amepata uponyaji kwa Suguye, ila Mimi binafsi namuona Suguye ni muhuni Fulani tu, lakini kuhusu uponyaji huu unaweza kulishuhudia hilo.

Namuongelea mtu ambaye nimesoma naye darasa moja.
 
HAKUNA KUSAJILI KANISA AU HUDUMA YOYOTE. NI USANII NA UAPELI MTUPU. PALE KWA MZEE WA UPAKO KWEKA PICHA KUBWA YA MH RAIS,. KAZI IENDELEE. WANAJIWEKA KARIBU NA WATAWALA, WANA AGENDA YAO. KINA GWAJIMA NAO....mhh
 
Kama hajakamilisha usajili, sioni kama kuna udini hapo..!!
Serikali haina dini na katiba ya nchi inatamka wazi mambo ya dini ni mambo binafsi ya nje ya serikali

Serikali kwa hiyo imeanza kusajili dini? Waabudu mizimu nnso wamewasajili?

Tatizo liko kwa watoa usajili pia wagumu sana kutoa hizo hati za kudumu

Mtu miaka yote hiyo ana operate kanisa kafungua hadi Television inaingiza pesa TCRA ,katoa ajira kibao kwa watu wasio na ajira kwenye huduma yake ikiwemo tele

Pili wageni kutoka nje kualikwa kuns shida gani si sawa tu na Royal tour kuvutia wageni waje waache pesa zao za kigeni nchini.Hizo ni faith tourism lakini huingiza pesa kwenye nchi kama ilivyo kwa waenda kuhiji Roma au Israel au Maka

Mzee wa Mwasapile wa Kikombe cha babu alikuwa hana usajili wowote na anachofanya anakijua mwenyewe lakini alibadilisha kabisa hali ya uchumi wa lolilondo.Watu walifurika kwa maelfu toka nje ya nchi na ndani .Nchi ikaingiza mapato makubwa mno

Halmashauri ya ngorongoro ikapaa kimapato ,magari ,ndege, nk biashara zikaamka mno

Hakuna aliyemfungia Mzee yule kufanya huduma

Nadhani labda yako mengine lakini kusingizia tu usajili sioni kama ni sababu yenye uzito wowote kufungia watu wasiendelee kuabudu kwa jinsi waonavyo wenyewe sawa

Hekima mara ingine itumike.
 
Amefanya tofauti na usajiri wake unavyotaka
 
Kama hajakamilisha usajili, sioni kama kuna udini hapo..!!
Kukamilisha ni kitu kidogo walitakiwa tu wamwambie akamilishe Kwisha.Kwa nini nguvu kubwa itumike kulifunga badala tu ya kwenda politely kumwambia kamilisha hiki na hiki na kama kuna la kurekebisha aambiwe rekebisha hiki na hiki
Simple.Alichofanyiwa hakiko sahihi kabisa

Unless serikali imeamua sasa kuwa na dini wakati katiba inatamka wazi kuwa haina
dini.Kufunga dini na kuwaambia watu wakatafute sehemu ingine ya kuabudu ni udini.Sio kazi ya serikali kumuambia mtu akaabudu wapi na aabudu vipi kwa staili ipi na aabudu nini kuku ng'ombe au mtu.Ni maswala binafsi
 
Siyo utaratibu mpya. Makanisa yote yanasajiliwa
Ni kinyume cha katiba ya nchi

Katiba ya nchi inatamka wazi serikali haina na kuwa mambo ya dini ni mambo binafsi
Kama kweli serikali inasajili dini imevunja katiba

Na kama kweli imefunga kanisa na huduma za kidini imevunja katiba
 
Hakuna makanisa ya makanjanja
Wakusanya sadaka,wauza mafuta,maji ya upako huko

Ova
Watu wanatumia pesa zao wewe kinakuuma nini? Mtu akipata pesa yake yuko huru kutumia apendavyo aweza honga wanawake au wanaume aweza kulewea pombe ,kutoa sadaka au kununua mafuta ya upako mikojo ya upako hata mavi ya upako ya kiongozi wake wa kidini .Ni pesa yake wewe yanakuhusu nini ?

Pesa zako nani anahangaika nazo kuhoji unakopeleka
 
Mfano wa Kagame, anaetaka kuanzisha kanisa ni lazima awe na degree ya Theology kutoka chuo kinachotambulika na serikali. Nami niongezee, awe na degree ya falsafa kutoka chuo kinachojulikana.
Katiba ya Rwanda tofauti na ya Tanzania
Rwanda Raisi ndie kila kitu sidi tunsongozwa na katiba.

Katiba Inatamka wazi kuwa Serikali haina dini na mambo ya dini ni ya mtu binafsi

Tanzania kuna waabudu mizimu unataka wawe na degree ya falsafa ya wapi?

Kuna waislamu unataka wawe na digrii ya wapi? Kuna waabudu ng'ombe wahindu unataka wawe na degree ipi? Huwezi.kuwa na Sheria inayo discriminate watu wa imani tofauti tofauti kuwa ohh huyu awe na digrii ya falsafa kuwa kiongozi wa dini huyo mwingine sio lazima nk ujinga mtupu

Yesu na mitume hawakuwa na hizo digrii za falsafa

Binadamu ndio ujiibukie kuweka vigezo ambavyo hata Yesu mwenyewe hakuweka
 
Wangefukuza wote tu wahuni yabakie makanisa ambayo hayafundishi umbea umbea na kutabiriana uongo
Sio kazi ya serikali kuangalia kanisa lipi la kweli na lipi sio hiyo ni kazi ya Mungu na muumini mwenyrwe tu anayesali sehemu husika
 
Ni kinyume cha katiba ya nchi

Katiba ya nchi inatamka wazi serikali haina na kuwa mambo ya dini ni mambo binafsi
Kama kweli serikali inasajili dini imevunja katiba

Na kama kweli imefunga kanisa na huduma za kidini imevunja katiba
Kwani wanaposajiri mabasi ya abiria, serikali inakuwa na mabasi?
 
Siku za mwisho wataibuka manabii wa uongo Jamii ya kikristo haishangai kuibuka kwa matapeli kwa sababu unabii unatimia. Wakristo thabiti hawalaghaiwi na hayo matapeli
 
Back
Top Bottom