Tafadhari, msije mkamfanya kama kaka mkubwa LIMUTUZ NATION.Tena alhadi akae kimyaa mnaafiki haswaa
Hana usheikh wwt mchumia tumbo tu!
Au tumpe ishu zake da mange tumharibiee?tunamsitiri tu
Nafikiri shehe ndo anatakiwa kutubu.Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya Mungu.Aache vitishohahahaha albadil inamuhusu akiendeleaa
kinywa kichafu siku zote hunena mabaya na si mema.mange kimambi dada yetu [HASHTAG]#ukatubu[/HASHTAG]
Unamaanisha huyo shehe mpenda ubwabwa yupo karibu na Mungu ??[emoji23][emoji23]
Oh! Kumbe Mange...!! Yaani kwavile Mange kasema ndo basi tena unashindwa kutumia uelewa wako mwenyewe kupima?!Rudia lalamiko la mange kuhusu kauli ya shekhe kukemea kuchanganya dini na siasa baada ya maaskofu Fulani kuonekana kukosoa,halafu ujijibu mwwnyewe
Kumbe kulikuwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo la Temeke... lakini kwa kuwa mnameza kila mnacholishwa na Mange, mkakubali tu kwamba alikuwa kwenye kampeni za Ubunge Kinondoni!!!Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkaribisha Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alipowasili kwenye ukumbi, baada ya kuwalikwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo hilo, ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jimbo na Katibu ambapo katika jumla ya kura 54 zilizopigwa Ahmad Mnamala alipata kura 50 za ndiyo na tatu za hapana na hivyo kuibuka mshindi, huku kwa jumla ya kura hizo hizo zilizopigwa, Kasim Kiame akiibuka kuwa Katibu wa jimbo kwa kupata kura zote 54 za ndiyo.
Yeyote anayejaribu kusaliti maslahi ya mungu kwa watu wake kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe hatakuwa salama. Kumbuka ya yuda na vipande thelathini. Shekhe wa mkoa wa dar jitafakari upya. Watu wa mungu hawawi hivi, wewe ni tofauti
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.
=====
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.
Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.
Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).
Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.
Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi
Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.
Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.
Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.
Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.
Si kila kiongozi ni mtu wa Mungu kuna wengine ni watu wa Ibilisi sasa jiulize walifikaje huko juu soma hapaKuwa katika position kama yake sio kitu cha mchezo mchezo tu
Maana ingekuwa ni rahisi hata wewe ungekuwa hapo
Lakini ana kipawa ambacho Mwenye Enzi Mungu anemtunuku!
Ndiyo maana kwenye Biblia Takatifu Mfalme Daudi hakuthubutu kumwuua Mfalme Sauli, tena alimwita mpakwa mafuta wa Mola, akamwambia Mwenye Enzi Mungu pekee ndiyo atakaye kuhukumu!
Hivi viti wanavyo kalia wakuu wa dini sio vya mchezo, ni watu wanao shika roho za watu yaani ni IMANI!
Tuwe wasngalifu sana kwenye maswala haya!
Tusiwafanye wakakunja roho zao!
Kweli nawaambia mwisho wake huwa sio mzuri hata!
Jamiiforums where we dare to talk OPEN!Siku hizi jf nayo imekosa udhibiti. Sioni sababu ya kumshambulia hivi huyu Shehe kwa alichosema