DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

shekhe amekutana na chizi ambae amerogwa siku nyingi sana hahahahahahahaaa.....shekhe anatia huruma Mungu wangu anazidi kuvuliwa nguo tu inabidi asome leo hili kesho afariki chizi ambae kesharogwa tayari....kumbe ustadh anaudhuria sana tigo fiestaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.............
 
Kweli sheikh kujibu hoja kwa kutishia bado hujasimama katika msingi wa kiisilam nilijua ungejieleza tu na uendelee na yako hadi kutishia kushitaki kuna nini kimekugusa hapo au kuna ukweli kuwa umepiga kampeni? Maana sio mara moja wala mbili mashehe wameshawahi kupiga kampeni za kisiasa misikitini nami nikiwemo mungu anawaona manaposimami na anajua ukweli kamili, Siungi mkono matusi ya mange lakini kwenye tuhuma kunaweza mukawa na ukweli mashehe fanyeni mambo ya mungu acheni kujiingiza kwenye siasa mnatugawa waumini wenu mungu anawaona
 
Reputation ya sheikh inaweza ikashuka ghafla, nadhani hakunaga mtu ambae aligombana na Mange akabaki salama,.kakosea sana kumjibu.Mange ana source nyingi sana za info,wadangaji wote wa
Mjini wapo kule kwa mange,so yeye akilianzisha tu bhasi info zinakuwa zina flow tu. He has to learn from mh.Paul makonda
 
Unamaanisha huyo shehe mpenda ubwabwa yupo karibu na Mungu ??[emoji23][emoji23]

Kuwa katika position kama yake sio kitu cha mchezo mchezo tu

Maana ingekuwa ni rahisi hata wewe ungekuwa hapo
Lakini ana kipawa ambacho Mwenye Enzi Mungu anemtunuku!

Ndiyo maana kwenye Biblia Takatifu Mfalme Daudi hakuthubutu kumwuua Mfalme Sauli, tena alimwita mpakwa mafuta wa Mola, akamwambia Mwenye Enzi Mungu pekee ndiyo atakaye kuhukumu!

Hivi viti wanavyo kalia wakuu wa dini sio vya mchezo, ni watu wanao shika roho za watu yaani ni IMANI!

Tuwe wasngalifu sana kwenye maswala haya!

Tusiwafanye wakakunja roho zao!

Kweli nawaambia mwisho wake huwa sio mzuri hata!
 
Rudia lalamiko la mange kuhusu kauli ya shekhe kukemea kuchanganya dini na siasa baada ya maaskofu Fulani kuonekana kukosoa,halafu ujijibu mwwnyewe
Oh! Kumbe Mange...!! Yaani kwavile Mange kasema ndo basi tena unashindwa kutumia uelewa wako mwenyewe kupima?!

Kwanza nini maana ya kuchanganya dini na siasa?! Huyo Sheikh alikuwa anaongea mambo ya siasa msikitini hadi useme anachanganya dini na siasa?!

Isitoshe, picha ambayo uliisema wewe ni hii hapa:
Al Had.png


Hapo juu unaona maelezo yanasema " Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu Akimkarisbisha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam"

Hivi sasa Mbunge wa Temeke ni Abbas Mtemvu?!

Maelezo zaidi ya hiyo picha yanasema:
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkaribisha Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alipowasili kwenye ukumbi, baada ya kuwalikwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo hilo, ambao uliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jimbo na Katibu ambapo katika jumla ya kura 54 zilizopigwa Ahmad Mnamala alipata kura 50 za ndiyo na tatu za hapana na hivyo kuibuka mshindi, huku kwa jumla ya kura hizo hizo zilizopigwa, Kasim Kiame akiibuka kuwa Katibu wa jimbo kwa kupata kura zote 54 za ndiyo.
Kumbe kulikuwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo la Temeke... lakini kwa kuwa mnameza kila mnacholishwa na Mange, mkakubali tu kwamba alikuwa kwenye kampeni za Ubunge Kinondoni!!!

Lakini mbaya zaidi, ni wakati Mbunge wa Temeke ni Abbas Mtemvu ambae hakurudi tena bungeni kwenye uchaguzi wa 2015. Kumbe kwa maana nyingine, mmelishwa matango pori kwa kuwekewa picha za zamani!!!

Picha zingine za hilo tukio ni hii hapa:
Al Had02.png


Mange.png


Na hili usidhani kwamba ni photoshop, tukio zima lipo hapa!

Au ni picha zipi hizo unazosema kwamba alikuwa anachanganya dini na siasa?!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Albadili mpaka ipate e-passport ikapate viza ya states of america si jambo dogo akiulizwa sabb ya kupeleka marekan??? Na hapo kunamawili kama haijawah kupanda ndege itagoma ndege masikhara ingekua hapa hapa bongo labda
 
CCM wameitumia fursa ya Sheikh wa mkoa wa Dar-es-Salaam kupiga propaganda ktk uchaguzi mdogo wa Kinondoni.

Wito kwa sheikh wetu wa Mkoa BAKWATA Dar-es-Salaam kuwa mwaangalifu kuhudhuria hafla ambazo CCM au viongozi wateuliwa wa awamu hii ya tano watamualika au kuwepo mahali hapo.

Jamiiforums haihusiki kwa namna yeyote na sakata la Shehe wetu Alhad Mussa Salim kukaangwa na jamii ya watanzania "kisiasa".
 
Hakuna dua ya mwovu inayoweza kumshika huyo dada maana matusi ni sehemu ndogo tu ya maisha yake hivyo huyo sheikh atavuliwa nguo tu hadi akome maana hana akili timamu kusimama kama kiongozi wa kidini.

Watu wanaomwombea huyo Mange ni wengi si tu raia wa kawaida bali hata baadhi ya viongozi wanafurahia uwepo wake 100%
 


Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Yeyote anayejaribu kusaliti maslahi ya mungu kwa watu wake kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe hatakuwa salama. Kumbuka ya yuda na vipande thelathini. Shekhe wa mkoa wa dar jitafakari upya. Watu wa mungu hawawi hivi, wewe ni tofauti
 
Huyu shekhe nae
Hahahhahaha et atamshtaki mahakama ya mbiguni kwakwakwkwa,,,tz kuna vituko
 
Viongozi wa dini wanapaswa kuwa na subira wao ni viongozi. Kumnuizia mtu jambo baya kwa sababu yeyote ile si halali, hii ni dalili ya kushindwa kuwa na subira. Ukiona umeshindwa kuwa na subira mbele ya Mwenyezi Mungu chukuwa hatua. Mungu tujalie heri na subira, tuvumiliane kwani hi dunia imejaa wanaadamu wa tabia tofauti na wote wapo chini ya viongozi wa kiroho.
 
Kuwa katika position kama yake sio kitu cha mchezo mchezo tu
Maana ingekuwa ni rahisi hata wewe ungekuwa hapo
Lakini ana kipawa ambacho Mwenye Enzi Mungu anemtunuku!
Ndiyo maana kwenye Biblia Takatifu Mfalme Daudi hakuthubutu kumwuua Mfalme Sauli, tena alimwita mpakwa mafuta wa Mola, akamwambia Mwenye Enzi Mungu pekee ndiyo atakaye kuhukumu!
Hivi viti wanavyo kalia wakuu wa dini sio vya mchezo, ni watu wanao shika roho za watu yaani ni IMANI!
Tuwe wasngalifu sana kwenye maswala haya!
Tusiwafanye wakakunja roho zao!
Kweli nawaambia mwisho wake huwa sio mzuri hata!
Si kila kiongozi ni mtu wa Mungu kuna wengine ni watu wa Ibilisi sasa jiulize walifikaje huko juu soma hapa
[emoji116]
16 Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.
Isaya 9 :16

Mara ngapi tumesikia masheikh, mapadri na hata maaskofu wamefumwa wakizini na hata kulawiti?

Hivi unajua kuwa kuna viongozi wa kidini walifika hapo kwa hongo? [emoji23] [emoji23] [emoji23] tulia kabisa viongozi wengine ni takataka kabisa
 
Back
Top Bottom