Acha kupotosha. Quran siyo kitabu cha wachawi.Msichezee imani za watu, subirini muone. Kuna visomo kaka wewe au sijui dada wewe au ndio mange mwenyewe. Usicheze na Qur’an! Huyo Mange Sio kama atakufa ila ataacha kutukana Watu.
Hivi wafahamu kitu kiitwacho CHARACTER DEFAMATION? ...Kwa sentensi chache niseme nionavyo mimi kuhusu hii "vita mpya" kati ya dada Mange na Sheikh mkuu Dar, Alhad Mussa Salum. Kwanza nieleze tu kuwa nauheshimu sana Uislamu kama navyoheshimu imani za watu wengine. Pia nawaheshimu viongozi wa kiislamu wakiwemo masheikh kama navyoheshimu viongozi wa imani na madhehebu mengine.
Lakini nadhani Sheikh Salum hakuwa na sababu ya kumjibu Mange. Kuna mambo ambayo tunategemea kuona Sheikh Mkuu wa mkoa akifanya, sio kufuatilia mambo ya instagram na kujibu. Tunategemea kuona akipambana kupigania haki za waislamu ktk namna itakayoleta matokeo chanya kwa waislamu na taifa kwa ujumla.
Tunategemea kumuona akiwasemea masheikh waliokamatwa miaka zaidi ya mitano iliyopita na mpaka leo wapo tu mahabusu bila kujua hatma yao. Aombe kesi zao zisikilizwe haraka (JPM anasema chapchap) ili kama wana hatia wahukumiwe, na kama hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani basi waachiwe HURU, kuliko kuendelea kuteseka tu mahabusu miaka zaidi ya mitano kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.
Hivi wakikaa mahabusu miaka 10 halafu bado ushahidi wa kuwatia hatiani usipatikane itakuaje? Au wakakaa mahabusu miaka 30 halafu wakaja kuachiwa huru kwa kuonekana hawana hatia itakuaje? Sheikh Salum haoni kama wenzake watakua wameteseka bila sababu? Sasa kwanini asiwasemee? Wanasheria wanasema "Justice delayed is justice denied", yani haki inayocheleweshwa ni haki iliyopotezwa.
Hawa masheikh wakiendelea kukaa mahabusu kwa miaka mingine zaidi na wakaja kukosekana na hatia it is justice denied. Ndio maana nilimpongeza Rais JPM alipomwambia Jaji Mkuu kwamba anapenda kuona kesi zikisikilizwa chapchap. Naamini na hii ya Masheikh itasikilizwa "chapchap" kama alivyoshauri Rais JPM (japo wameshasota miaka mingi sana ndani).
Je Sheikh Salum anajua kuna wenzie wanaoteseka huko magerezani? Wapo wanaodaiwa kudhoofika sana kiafya, wakiwemo akina Sheikh Fareed, Mselem na wengine. Nilitegemea kuona Sheikh Salum akipambana kwa ajili ya HAKI na USAWA kwa watanzania wote (wakiwemo masheikh walioko gerezani) na sio kupambana na Mange Kimambi. I stand to be corrected.!!
Malisa GJ
I second your opinionNadhani lengo la mtoa uzi,ni kuhusu masheikh waloko rumande.sasa unataka sheikh aingilie mahakama au aipaingie mahakama nn cha kufanya.
Acha kupotosha. Quran siyo kitabu cha wachawi.
Hata kama mtu akisomewa ili adhurike huwa hawasomi kwenye Quran. Vipo vitabu maarufu kwa kazi hiyo.Sio wachawi, ni kitabu kitakatifu. Subirini Kisomwe.
Ningedhan mngemshaur huyo Mange aache MATUSI lingekuwa jambo la BUSARA ... badala yake naona mwazidi kumpa "promo" ili azidi kuendeleza MATUSI ... and you enjoy it ..Sheikh amevuliwa nguo amebaki uchii km alivozaliwaa, ni hatari sana, asipowahi kumuomba msamaha Mange basi atazidi kuumbuka na huenda yy Ndio hataumaliza huu mwaka atakufa kwa depression!
Hata kama mtu akisomewa ili adhurike huwa hawasomi kwenye Quran. Vipo vitabu maarufu kwa kazi hiyo.
Na huo ndio wasifu mdogo wa sheikh alhadNi kweli mkuu hayo uliyoyazungumza ni ndoto na tamaa ya kila muislamu kuskia kesi ya mashekh wazanzibar sio tu inasikilizwa lakini wanaachiwa huru kwa kutokutwa na hatia.
Ima hilo la kumsikia Alhad akizungumza juu ya mateso wanayokutaana nayo wenzie, miaka miambili hutomsikia hata siku moja, na wala sio katika matarajio ya wengi kulisikia hilo.
Alhad ni katika wanufaika wajuu kabisa wa mfumo huu wa tawala za CCM hapo ndipo mkate wake wa kila siku ulipo, huwezi kuskia akienda kinyume na wanaompa mkate wake.
Mwache awatie adabu hawa waharibifu aisee, tunawaamini kuwa ni watu wa Mungu kumbe ni mafirauni tu!Ningedhan mngemshaur huyo Mange aache MATUSI lingekuwa jambo la BUSARA ... badala yake naona mwazidi kumpa "promo" ili azidi kuendeleza MATUSI ... and you enjoy it ..
Naelewa vijembe unavyotaka kumaanisha. Lakini pamoja na sayansi yote kjwa kwenye Quran imepiga marufuku uchawi.Ndio lkn ni Quran. Quran ina elimu pana sana, uumbaji wote wa dunia upo ndani ya Quran. Sayansi yote ya dunia ipo kwenye Quran.
Naelewa vijembe unavyotaka kumaanisha. Lakini pamoja na sayansi yote kjwa kwenye Quran imepiga marufuku uchawi.