DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Huyo shehe angetubu tu ili yaishe maana yule dada atamuabisha sana
 
Nadhani hakutakiwa kutoa tamko kama alilotoa hadharani..Tatizo alikuja kwa pupa mno..Alitakiwa kuwauliza hao wapambe wa chama kabla ya kutoa tamko la ku mu attack mrembo wa kule Amerika

Alitakiwa kumuuliza RC nini kilimkuta alipo jaribu kupambana na yule dada

Halafu angekuja kwa super brand a.k.a the nation pia angemuuliza pia..

Sasa kwa kashfa hizi zote sidhani kama waumuni watamuelewa..Ni vema akajivua gamba tuu..

Tatizo hachelewi kutuwekea video za dhambi alizokuwa anafanya…

Yule mrembo wa kule Amerika anaita kitu cha “HIROSHIMA”
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hivi nani anamuelewa Al hadi huyu ni toothless kama vile mrema kwenye siasa

Mm nashangaa chadema wanaogopa huyu jamaa kushiriki kampeni wakati hakubaliki kwa waislamu hakuna shehe wa bakwata mwenye ushawishi kwa waislamu tena haswa huyu wengi wanajua cheo chake cha shehe wa mkoa ni wa kisiasa tu ila Alhadi hana ushawishi wowote na ukifanya research na Fanya sampling 99% utaambiwa hawamuelewi na hawamkubali ..nashangaa hii tension iliyo rise saizi wkt 2012 watu walilalamika na kupigwa virungu sabb ya huyu lkn alikuwa backed na govt ..

Saizi mtapambana naye chadema huyu kazi kwenu ila suala la uaminifu kitambo haaminiwi na waislamu wa tz
 
Shehe mkuu, wa mkoa wa dsm, mji kuu wa nchi, kualika wandishi kuelezea mambo ya binti na mitandao, na vitisho vya maombi, si hadhi yake. Ni kudhalirisha cheo hicho.
 
Nilidhan huna INFO kamili juu kilichotokea ... cause you have the FULL INFO ya kilichotokea .... Swali: Ni nani aloanza kumtukana mwenzie kati ya Mange na Shekhe? ... Ukipata jibu rejea msg yangu ya awali ...
Chizi akichukua nguo zako wakati unaoga busara nikuachutama na kuangalia namna ya kujistiri sio kumkimbiza, ukimkimbiza utaonekana wewe ndio chizi yeye mzima, ndicho ninachokiona hapa.. huyu Shekh sio wakwanza kutukanwa na Mange, na wote tunamjua Mange ni mtu wa aina gani.. Kuna wakati kunyamaza ni jibu jema sana kwa mtu aliyekosa hekima
 
Kwa upeo wetu tunaendelea kuamini eti wenye vyeo ndio wenye akili kumbe mambo yalishaharibika kitambo baada ya waliokuwa na vyeo kuanza kuwashika watoto wao na wajomba mikono kuwaingiza makazini hadi kuwapa hata nafasi za maamuzi makubwa.
Matokeo yake yanaanza kuonekana sasa kuwa walio ndani hawawezi kuelewa kuwa walioko nje vijiweni wana upeo kuwazidi! Kwa vile yeye ndio kaanzisha kujibu udakuu wa insta kwa press conferences na aje sasa akanushe yote yaliyosemwa ili kunusuru kanafasi kake!
 
Daah, nimeona mahali fulani, mashuhuda wanatiririka kashfa hadi aibu
 
Jamiiforums tafadhali jitengeni kabisa na huu upuuzi wa kina Mange na kuchafua viongozi wa dini na taasisi......si jambo jema na si lengo la mtandao huuu
 


Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, walijiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Angekuwa kweli kiongozi wa kiroho roho wa Mungu angempa maarifa ya kunyamaza!
 
Mmeshindwa kusoma albadir kwa watu wanaouwawa kila kukicha mnakuja kukomalia jambo la kipuuzi mmemgeuza Mungu shemeji yenu eti!!!
 
Back
Top Bottom