Mnondwe
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 4,013
- 3,679
Kamtandika kisawasawa,akiendeleanae anaweza kumfikisha pabaya.Nimeona Majibu ya Mange Kimambi kwa sheikh! Aiseew! Kuna tatizo kubwa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kamtandika kisawasawa,akiendeleanae anaweza kumfikisha pabaya.Nimeona Majibu ya Mange Kimambi kwa sheikh! Aiseew! Kuna tatizo kubwa!
Huyu Mungu wetu si wa visasi. Yeye hufanya njia pasipo na njia, kama Lisu walishindwa kumuua huku CCTV zikiwa zimeximwa kwa watu wasiojulikana na bunduki za kivita zilindima kwenye makao makuu ya nchi yenye ulinzi wa nchi bila mafanikio yeye atatumia nini? Labda awasiliana na Rais Kim wa Northern KoreaHicho anachokieleza kwamba Mange "ataondoka" ni kuwazia mambo yasiyowezekana! Katika nyakati zetu ni lazima kuacha kutumia matisho kama zamani kwamba ukimfanya hivi dhidi ya dini utadhurika. Kama anamaanisha kuwa Yeye Sheikh na viongozi wenzie watamuomba Mungu ili "amupumzishe" Kimange hilo ni jambo ambalo Mungu hawezi kufanya kabisa! Labda kama kuna Mungu tofauti na tunayemjua wengine. Ningeelewa zaidi ikiwa angemuombea Mange maisha marefu na kujaliwa moyo Wa kutambua makosa yake na kutubu.
Rudia lalamiko la mange kuhusu kauli ya shekhe kukemea kuchanganya dini na siasa baada ya maaskofu Fulani kuonekana kukosoa,halafu ujijibu mwwnyeweKwahiyo ni dhambi au ukiukwaji wa sheria kwake kuwepo kwenye hicho kikao?
Hatari sana. Na kwa huyo binti watawekana makovu ya kucha usoniAnamjibu Mange, angetumia Instagram tu asiwachoshe wanahabari
Biblia inasema msikae barazani kwa wenye mizaha!Utofauti wa viongozi wa kislam na kikatoliki unauona hapa.
Ingekuwa ni askofu katukanwa hivyo wala asinge hangaika kujibu.
Kusoma falsafa na theoloji inasaidia kutoshiriki kwenye ujinga
Atamweza mange insta?Anamjibu Mange, angetumia Instagram tu asiwachoshe wanahabari
Kwanza kiongozi wa dini uliye na ujazo wa busara na hekima wapata wapi muda wa kusubscribe account ya mange kama sio umbea kitu gani !!?najua matusi hayafai,ila dhulma wanazofanyiwa wengine mbona sijawahi msikia akiongelea.
Allah atusamehe.
hilo neno lako LA mwisho pigia mstari ..tena usije kushangaa pindi atkpoitwa white house na kupewa bahasha ya kaki kama pongezi ya hiki alichokifnyaMtumishi Wa mungu anamtisha mtu badala kumwombea abadilike jamani au ni Mtumishi Wa ccm
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.
=====
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.
Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.
Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).
Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.
Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi
Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.
Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.
Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.
Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, wajiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.
Na wengine ni wabaya kuliko hata watu wabkawaidambona viongozi w dini wanalawiti, wanatembea na wake za watu, wanIba sadaka, etc acha kuwakweza. Ni watu kama yeyote