pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 692
- 880
Deiwaka World chini ya Joseph Mbilinyi “SUGU” kwa kushirikiana na Alliance Francaise (Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa), imeandaa “Bongo Flava Honors” Concerts ambalo ni Jukwaa mahsusi kwa Wakongwe wa Bongo Flava.
Concerts hizi zitafanyika Alliance Francaise, Upanga, Dar Es Salaam.
Kila mwezi kutakuwa na Concert moja kwa ajili ya Mkongwe mmoja, ambapo Mkongwe huyo atafanya Show live kwa kupigiwa na band ya Swahili Blues na usiku wote utakuwa ni maalum (dedicated) kwa ajili yake.
Madhumuni ya BongoFlava Honors ni kuweza kuwa na Jukwaa litakalotumika kutambua na kuheshimisha muziki wa Wakongwe wa Bongoflava, na pia kuwapa fursa mashabiki wa enzi hizo (Golden Era) za muziki huu kujikumbusha na kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu na wanaitamani .
Na pia Bongo Flava Honors zitasaidia kuondoa gap kati ya zamani na sasa, Mashabiki wa zama mpya wanatapata nafasi ya kuona Wakongwe mbalimbali na kuweza kufuatilia historia ya muziki wetu kupitia ratiba hizi za kila mwezi.
Mwezi huu tarehe Februari 24, 2023 siku ya Ijumaa kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 6 usiku. Tutakuwa na Mkongwe TID.
Host wa Concerts hizi za kila mwezi atakuwa ni Msanii mkongwe Sugu, na pia atakuwepo Dj Mkongwe Boni Luv kwa burudani zaidi.
KARIBUNI NYOTE!
#HeshimaKwaWakongwe