Dar: Simba yafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC 3-1 Nkana FC

Dar: Simba yafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC 3-1 Nkana FC

Ni mechi ya kupindua matokeo na kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, leo kwa wawakilishi wa Tanzania, Simba SC watakapokuwa wakikwaruzana na Nkana FC kutoka nchini Zambia katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kaa pamoja na Timu ya JF kukuletea mtanange huu wa kukata na shoka kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukaambiwa.View attachment 975408View attachment 975410
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Taifa ni dakika 90 za mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika

Naam mpira umeanza uwanja wa Taifa

Simba wameanza kwa kulishambulia lango la Nkana FC..ambapo shuti la Bocco linadakwa na golikipa wa Nkana FC

10' Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna timu imepata bao

Simba 0-0 Nkana FC

17' Gooooooooaaal W. Bwalya anaipatia Nkana FC bao la kwanza kwa kichwa kufuatia krosi iliyopigwa

Simba SC 0-1 Nkana FC

Nyoni anajaribu kupiga shuti kali goo laaaa..Mpira unagonga mwamba na kurudi uwanjani.

Pamoja na kuwa nyuma ya bao moja bado Simba wanaliandama lango la Nkana FC

29' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal..Jonas Mkude anaisawazishia Simba bao kwa shuti la umbali mrefu

Simba SC 1-1 Nkana FC

Nkana wanajaribu kutumia mashambulizi ya kushtukiza hapa uwanja wa Taifa.

40' Ligi ya mabingwa Afrika uwanja wa Taifa

Simba 1-1 Nkana FC

45+2 kuelekea kuwa mapumziko Simba wanaliandama lango la Nkana huku Nkana wakijaribu kuzuia

45+1' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal Mk14 Mfumba Jicho Meddie Kagere anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa safi kufuatia mpira wa Krosi

Simba SC 2-1 Nkana FC

Naaaaaaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wanatoka uwanjani wakiwa mbele ya mabao mawili dhidi Ya bao moja la Nkana FC


Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Taifa na hakuna mabadilko kwa pande zote mbili

Simba SC 2-1 Nkana FC

49' Simba wanapanga mashambulizi kuelekea lango la Nkana FC

Wanachukua Nkana sasa..Lakini wanapoteza anachukua Wawa upande wa Simba

Kona kuelekea lango la Nkana FC..Bocco gooo laaa, ilikuwa hatari lango la Nkana

53' Anatoka Nicholas Gyan anaingia Juuko upande wa Simba

57' mpira ni mkali kwa pande zote mbili..huku Simba wakihitaji goli moja tu kuweza kufuzu michuano hii ya mabingwa afrika.

87' Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga..ilikuwa ni hatari sana

Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal
Mwamba wa Lusaka anaipatia Simba bao la tatu hivyo kuihakikishia Simba inafuzu michuano hii Ligi ya Mabingwa ya Afrika

90' Naaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa. Simba wanaibuka kwa ushindi wa mabao matatu dhidi ya moja la Nkana FC

Kwa matokeo hayo Simba imefuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao manne kwa matatu kufuatia mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Zambia ambapo Nkana FC waliibuka mabao mawili kwa moja dhidi ya Simba SC

Simba SC 4-3 Nkana FC

Asante sana wote mlioshiriki hapa JF

Ghazwat...
View attachment 975519
SIMBA YAFUZU KUCHEZA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

Klabu ya Simba imefuzu kuingia hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga klabu ya Nkana FC ya Zambia goli 3-1

Magoli ya Simba yamefungwa na Mkude 29', Kagere 45+1' na Chama 88' huku goli la Nkana likifungwa na Bwalya 17'. Hivyo Simba inasonga kwa jumla ya magli 4-3

Timu kutoka Tanzania inafuzu kucheza Klabu Bingwa Afrika ikiwa ni baada ya miaka 15
Nawapongeza sana wachezaji wote benchi la ufundi na wapenzi wote,haikuwa kazi rahisi pamoja na kuwa nyuma walijituma sana......hongereeni
 
Mnyamaaaaa kafanya yake Leo, wale wenye chuki, husda na roho mbaya kwa Mnyama wajinyonge Leo.

FB_IMG_1545581287014.jpg
 
Back
Top Bottom