Ndugu zangu wa Yanga ndio tunapambana na timu inafanya vizuri kipindi hiki lakini kuna haja ya mageuzi makubwa kufanyika hasa suala la uwekezaji wa maana. Mafanikio ya Mikia yawe somo kwenda kwamba siku zote utavuna ulichopanda. Nakataa kukubali kwamba Simba yeye ndio anayaweza haya mashindano. Jiulize toka mwaka 2002 leo ndio anafanikiwa kutinga hatua ya makundi. Ni nguvu ya usajili, nguvu ya pesa. Vilabu vikubwa vyote vimewekeza pesa nyingi sana kwa ajili ya haya mashindano na ni ngumu sana kuchuana nao kama una kikosi dhaifu.
Rejea kipindi Manji bado yupo na timu, tulitinga hatua ya Makundi mara mbili. Sio kwamba tulibahatisha bali tulistahili kutokana na uwekezaji uliofanyika.
Mwisho naiombea Mikia ipewe kundi jepesi ili iendelee kutuwakilisha Watanzania.
Kundi A :
Esperence
Tp Mazembe
Al Ahly
Simba