DAR: TANESCO mnachotufanyia mtatuunguzia vitu

DAR: TANESCO mnachotufanyia mtatuunguzia vitu

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Sijui kuna tatizo gani, lakini leo Ijumaa Septemba 8, 2023, huku ninakoishi maeneo ya Kilungule A, Kimara, Dar es Salaam, umeme umekatika zaidi ya mara nane.

Tangu asubuhi Tanesco wanafanya zoezi la kukata na kuwasha umeme, sijui wana mpango wa kutuunguzia vitu vyetu ambavyo tumenunua kwa kukopa.

Kama kuna tatizo tuambiwe lakini hili la umeme unakatika, unakaa nusu saa au dakika kumi unarudi, kisha baada ya saa tatu au nne unakatika tena, si sawa.

Hebu fikiria, kama usiku huu pekee kuanzia saa 1 hadi saa 3, umeme umekatika mara tatu na kurudi si chini ya dakika kumi.

Pia, soma Kero: TANESCO Mtwara wanakata kata umeme ovyo!
 
ingekua Makamba bado yuko pale, angekula mvua za matusi
 
Sijui kuna tatizo gani, lakini leo Ijumaa Septemba 8, 2023, huku ninakoishi maeneo ya Kilungule A, Kimara, Dar es Salaam, umeme umekatika zaidi ya mara nane...
Mkuu tanesco hawakati na kurudisha umeme ni mfumo
 
Makamba anachekelea tu huko aliko,huku akim-DM Martin Maranja Masese.
 
TANESCO wapumbavu Mbezi mwisho wamekata toka saa 11 jioni mpaka mda hawajarudisha pumbavu zao
 
TANESCO wapumbavu Mbezi mwisho wamekata toka saa 11 jioni mpaka mda hawajarudisha pumbavu zao
bora huko mkuu ni masaa tu... Shinyanga ni siku 3 mpaka 4... Au wanakata saa 3 asubuh wanawasha saa 7 usiku... Wenye biashara zinazotegemea umeme tutashika majembe mwezi wa 9 huu...
 
dah! Pole sana mkuu... Nakushaur tafuna tuu huo mchele kuliko umwage alaf njaa iume uanze kuokota tena...
Kinachosikitisha ni kuwa mboga ipo tayari ilibaki wali tu yan aah afu bado haujarudi hadi saiv dah[emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom