Yegomasika
JF-Expert Member
- Mar 21, 2009
- 13,164
- 61,255
wenzio wanapiga nyundo kwenye internet hawapatikani mzee,si mafundi?na wakimaliza kazi wapo hoi so i think humu hakuna DIT kabisaaaaa!mwenyewe shahidi since jana hajatokea mtu?au wewe ulibadilisha fani?
Yeah, enzi akina Prof. Mwadosya na Luhanga walipokuwa wanasoma pale !... Anamaanisha enzi zileee za mwaaalim
Yeah, enzi akina Prof. Mwadosya na Luhanga walipokuwa wanasoma pale !
Yegomasika,
Mie nilikuwa Tech. College Arusha...... Je ulitokea shule gani kuja Dar Tech?
Washikaji zangu hapo walikuwepo kibao. Akina Mgongo, Kasanga, Msaka, marehemu Mfwangavo, Godfrey M. Ntille (kwa sasa yuko Sumbawanga), Kyebala (mshikaji wa JKT, Mhaya wa maneno meeengi!!). Haya lete habari zaidi maana Dar tech na TCA walikuwa ni MAPACHA ambao ukichokoza mmoja, unaangukiwa na wengine......
Du Kasanga na Msaka nilikuwa nao class moja pale Dar Tech, kwa hiyo utakuwa unamfahamu jamaa mmoja alikuwa hapo TCA miaka hiyo anaitwa Kayungilo?. Huyu tulikuwa nae Oljoro JKT.Yegomasika,
Mie nilikuwa Tech. College Arusha...... Je ulitokea shule gani kuja Dar Tech?
Washikaji zangu hapo walikuwepo kibao. Akina Mgongo, Kasanga, Msaka, marehemu Mfwangavo, Godfrey M. Ntille (kwa sasa yuko Sumbawanga), Kyebala (mshikaji wa JKT, Mhaya wa maneno meeengi!!). Haya lete habari zaidi maana Dar tech na TCA walikuwa ni MAPACHA ambao ukichokoza mmoja, unaangukiwa na wengine......
Du Kasanga na Msaka nilikuwa nao class moja pale Dar Tech, kwa hiyo utakuwa unamfahamu jamaa mmoja alikuwa hapo TCA miaka hiyo anaitwa Kayungilo?. Huyu tulikuwa nae Oljoro JKT.
Umenikumbusha mbaaaali sana. Kina Lugundi (mzee wa misosi) Mwamafupa, Belela, Mbosoli, Mollel kina marehemu Method Mogella, Mh. George Simbachawene.(Mb) nakadhalika. Nakumbuka tulikuwa tunaenda kambi ya fisi kupata machozi ya simba kwa mama Seberee afu tunamalizia na kabia kamoja pale kwa anti kutoa harufu. TCA, kweli tumetoka mbaaali sana!
Mkuu Chrispin,
Mie nilikuwa mwaka mmoja na marehemu Method Mogella na marehemu Saleh Sonda. Sonda alikuwa na shabaha kwenye miguu yule mtu ni hatari. Mzee Lugundi na misosi yake alikuwa hana noma. Tulikuwa tunawahi mapema kupata Top Layer na "ng'ombe". Ng'ombe ilikuwa linyama likubwa na mifupa..... ukiondoka nalo watu wanaanza kupiga makelele, buuuuu....
Nimepata habari juzijuzi kuwa kijana mmoja wa Makelele sana akienda kwa jina la Cathbert Busumano amefariki. Sina habari zaidi ya amefariki.
Mungu Awalaze mahali pema peponi wale wote waliotutangulia mbele ya haki,AMINA.
Ndugu tukumbushe ulikuwa intake ipi hapo TCA,kwenye Vimbosoli,
Ila kaka Crispini noma unasingizia kuumwa ili uwapate wapishi,umalize?Aibu hiyo kwa mhandisi mtarajiwa,sitashangaa nikisikia umerudia form one ili uwapate mabinti wa form one!Ila kwa Technics uko juu mkuu!
Mkuu umenikumbusha mbali. Nakumbuka utaalamu wangu wa kuvizia ng'ombe na kuvizia Top Layer. Na vile vimkate "vimbosoli". Unawakumbuka na 'vyura'? Wale wafanya usafi ambao mzee mzima ukizidiwa unakacha klasi unawavizia wakija kudeki unamvuta mmoja chumbani unafanya vitu vyako. Au tule tupishi tuliokuwa tunaleta msosi bwenini kama unaumwa. Mzee nilikuwa nazuga kuumwa ili niletewe msosi, then namaliza kazi. Hahahahahah!
Mkuu,
Kule ndani kulikuwa pia kuna vile vitoto vinakuja kuvizia mikate iliyoachwa mle ndani. Watu wakawa wanaviita vindege. Siku moja kitoto cha Kahurananga kikaingia na chenyewe kuwa ndege "tukakitoa mbio hadi kwa baba yake". Tukakipa heavy warning na kipande cha mkate kuwa akitaka basi awe anatusubiri chumbani kwetu.
Kahuranganga alikuwa ni Big Brother wetu kweli kweli. Jamaa alikuwa mtu mmoja safi sana na ndiyo maana kesi ya mwanae tuliifanya kama ni kesi yetu na hatukusubiri baba aone. Kwa kupenda mziki, tulikuwa tunapata Good time akituazima ile Radio Cassete yake aliyonunua German (Telefunken). Hilo readio lilikuwa na uwezo wa kudaka waves za Microphone wireless. Ilipokuja kwaya ya Kanisa kuu la Kilutheri pale TCA kwenye mashindano ya kuimba, waliimba nyimbo mpya kabisa ambazo hata hawajazirekodi. Kumbe Kahuranga anawarekodi kwa kutumia Mic iliyokuwa imewekwa mbele yao. Wakati wa chakula cha mchana, akaanza kuipiga ile miziki ambayo ilikuwa almost Studio Quality. Jamaa waliogopa sana na kumuomba asiuze wala kugawia watu maana ndiyo Investment yao.......
Mwaka jana nilikuwa nataka cheti changu. Baada ya pilika za hapa na pale, Sambayuka akakubali na kumpatia dada yangu aliyekuwa Arusha anitumie. Nilipokipata nikampigia simu kumshukuru.
Yule Mpishi mwenye Matusiiii, aitwaye Mama Hamza (kibonge cha mama) alikuja kumuokoa maisha rafki yangu. Kijana aliuguwa homa ya Matumbo na akienda hospital wanampa aspirin. Mama akampa kadi yake Familia na kwenda hospital fulani barabara ya Uhuru karibu na kanisa la Walokole, kama sikosei ni private (na aghali) na kijana akafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa. Kijana alipona na gharama zote alilipa mama Hamza na mumewe. Yule mama milele sintamsahau. Ukimuona huwezi kudhani ni mtu mkarimu namna hiyo. MUNGU AMBARIKI KOKOTE ALIPO yeye na familia yake.
Mkuu,duh!!!!!!!!! huyo kayungilo tulisoma nae mazengo technical sec school