Mkuu,
Kule ndani kulikuwa pia kuna vile vitoto vinakuja kuvizia mikate iliyoachwa mle ndani. Watu wakawa wanaviita vindege. Siku moja kitoto cha Kahurananga kikaingia na chenyewe kuwa ndege "tukakitoa mbio hadi kwa baba yake". Tukakipa heavy warning na kipande cha mkate kuwa akitaka basi awe anatusubiri chumbani kwetu.
Kahuranganga alikuwa ni Big Brother wetu kweli kweli. Jamaa alikuwa mtu mmoja safi sana na ndiyo maana kesi ya mwanae tuliifanya kama ni kesi yetu na hatukusubiri baba aone. Kwa kupenda mziki, tulikuwa tunapata Good time akituazima ile Radio Cassete yake aliyonunua German (Telefunken). Hilo readio lilikuwa na uwezo wa kudaka waves za Microphone wireless. Ilipokuja kwaya ya Kanisa kuu la Kilutheri pale TCA kwenye mashindano ya kuimba, waliimba nyimbo mpya kabisa ambazo hata hawajazirekodi. Kumbe Kahuranga anawarekodi kwa kutumia Mic iliyokuwa imewekwa mbele yao. Wakati wa chakula cha mchana, akaanza kuipiga ile miziki ambayo ilikuwa almost Studio Quality. Jamaa waliogopa sana na kumuomba asiuze wala kugawia watu maana ndiyo Investment yao.......
Mwaka jana nilikuwa nataka cheti changu. Baada ya pilika za hapa na pale, Sambayuka akakubali na kumpatia dada yangu aliyekuwa Arusha anitumie. Nilipokipata nikampigia simu kumshukuru.
Yule Mpishi mwenye Matusiiii, aitwaye Mama Hamza (kibonge cha mama) alikuja kumuokoa maisha rafki yangu. Kijana aliuguwa homa ya Matumbo na akienda hospital wanampa aspirin. Mama akampa kadi yake Familia na kwenda hospital fulani barabara ya Uhuru karibu na kanisa la Walokole, kama sikosei ni private (na aghali) na kijana akafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa. Kijana alipona na gharama zote alilipa mama Hamza na mumewe. Yule mama milele sintamsahau. Ukimuona huwezi kudhani ni mtu mkarimu namna hiyo. MUNGU AMBARIKI KOKOTE ALIPO yeye na familia yake.