Dar Technical na Technical College Arusha Mpo !!

Wale wa TCA mnakumbuka kumwaga sumu cafetaria? hasa kwa wale waliokuwa wameoa jengo fupi, ingawa siku hizi nalo limerefushwa. halafu mnamkumbuka marehemu Mzee Bukwimba? alikuwa anapenda totos sana. Nawakumbuka sana kina Chris Konga, Teddy Mwanambilimbi huyu alikuwa anapenda sana watoto hadi mwendo wake ulibadilika as if yuko shughulini muda wote, alikuwa akiwapiga korido wenzie sana.

Na wale waliokuwa wameoa mnakumbuka ile bar ya west kilimanjaro? maana huko ndo ilikuwa sehemu ya kubadilisha dayat hasa Jumatatu kama sikosei ilikuwa Ugali maharage.
 

Mkuu ina maana siku hizi jengo fupi limerefushwa? Ishu ya kumwaga sumu hata usinikumbushe. Nakumbuka nilikuwa mimewekeza jengo fupi, basi nilikuwa namwaga sumu vibaya sana, bahati mbaya niliyemwekeza marehemu Bukwimba akaingiza gia zake nikatoswa. Nami kwa hasira nikakamata rafiki yake. Kuwapiga watu korido ilikuwa jadi yetu chumba namba tisa, scaba scuba.

Kulikuwa na mpishi mmoja tulikuwa tunamwita form six. alikuwa hamalizi shule. Tukicheza disko na totoz alikuwa anajifanya denti na darasa alilokuwa anasoma daima ilikuwa form six. Nimeingia pale akiwa form six na nimeondoka akiwa form six bado.
 


Leta mambo ya Korogwe, Bagamoyo, Tanga na kaka yake na huyo Teddy Mwanambilimbi, waambie nawasalimia sana
 
Tupo kamanda. pale mie 1992 mpaka 1996. mechanical engineering. namkumbuka sana marehemu mwl. Flowin Sapula. Dr. Zakaria Mganilwa yupo SUA sasa hivi. kuu alikuwa Mr. Msoma


RIP Sapula, nimesoma naye 84-87 DTC japo tulikuwa fani tofauti namkumbuka sana alishika madaraka ya uongozi wa wanafunzi pale DTC miaka hiyo.sikujua haya asante jamii forums
 

Mkuu, sumu kama kazi. Ila unakumbuka msemo "ameyamwaga?"

Teddy nilimuacha mwaka 1989 kama sikosei akiwa mwaka ya 2. Nikiwa mwaka wa 1 kulikuwa na kaka yake kifamilia akiondoka kwa jina Bob Venny. Jamaa alishawahi fanya varangati huyu jengo fupi kama saa tisa usiku. Mwenyewe anarudi zake Disco usiku, kufika jengo fupi anasikia kule juu kicheko na akina dada wakimjadili. Mmoja huyo naona alikuwa akimsema sana, basi akaingia jengo refu, akavuta JANI lake swafi na kwenda chini ya dirisha, basi alikuwa akifoka kwa nguvu kiasi kwamba jengo refu na fupi wanasikia.............

Dooo, RIP Bukimbwa. Huyu jamaa alikuwa wakati mwingine akijifanya Mpelelezi. Sikujua kuwa alikuwa mtu wa totoz. By the way kuna kijana mmoja wa Kichaga alikuwa akikata PUNKY za nguvu sana na kama sikosei alikuwa akiitwa Bathoromew. Huyu kijana akimdaka mtoto wako getini kwa bahati mbaya kaja bila taarifa, alikuwa mkarimu sana na kumpeleka hadi kwake. Akifika chumbani alikuwa akiomba amege hadi ANALIA>... 🙂 Wakati mwingine alikuwa akifanikiwa.....

Pale TCA walikuwepo watoto wawili vichaa, mmoja akiitwa Mambo Mambo na mwingine alikuwa akichukuliwa na kijana mmoja akiitwa Kaswalala. Hawa walikuwa wakikutana na Marehemu Sonda, ndiyo utajua USWAHILINI kukoje maana unakuwa kama upo LOVE PARADE ya Berlin. Lugha na vitendo vyao hasa kama ni GIZA, kwa kweli yalikuwa matendo ya GIZA.

Ehhh, namkumbuka yule CHURA walikuwa wakimuita TUM TUM. Ila Vyura wengine walikuwa wakali sana. Nakumbuka kimoja kilikuja hadi kuolewa na Boss wao.

Mkuu, unaweza kumuona Sambayuka hapa ila picha zi nzuri sana na ukurasa wafunguka taratibu:

http://eol.habari.co.tz/tca.htm
 

Kwani huyu Chrispin hapa nu yule aliemaliza TCA mwaka 94 na kina Sumo? Mimi Robert Moshi, nilimaliza 94 lakini nikiwa Automotive Engineering, napenda pia kuwafahamisha kuwa mwenyezi Mungu aliwachukua pia kina Mzee Lugundi, na Mzee Mkongwe aliekuwa Automotive
 
RIP Mzee Lugundi. Alitulisha na kututunza wengi sana pale TCA. Asprin upo hapo?

Kikubwa kwa huyu Mzee ilikuwa ni Busara ua utu. Ukiacha kuwa ni Mpishi, pia alikuwa na Mzazi kwelikweli.

Utamfahamu mara kukitokea matatizo na wapishi wengine au kijana akiuguwa. Hata ukipata Mgeni, ukienda kumuona na kuongea naye, siku zote alikuwa akisikiliza na kukuambia nini ufanye. Ila mwisho wa siku unakuwa umeridhika na msaada wake.

Miaka ya 80 mwishoni kulikuwa na Mushi mwingine na kama sikosei na yeye alikuwa Robert na alitokea Mazengo. Mwanzo nilifikiri ndiye ila ulivyosema ni miaka ya 90 basi nikajua siyo.
Nafikiria siku moja tuanze mpango wa kuwakusanya Watanzania waliosema hapo na kuwa tunafanya michango ili kukisaidia kile chuo chetu kipendwa. Nategemea Mhandisi Robert Masika anafanya kazi nzuri hapo kwa sasa.

AGAIN: RIP Mzee Lugundi.
 
Last edited by a moderator:
OMG!

Imetokea lini hii makitu kwa mzee wetu??

RIP Mzee Lugundi.

Mkuu MoshiR, naam mie ndo yuleyule nlokuwa na kina Sumo. Majuzi kati hapa nimekutana na room mate wako Wiranga Mwisawa a.k.a ngozi. Wako wapi kina MT??
 
Last edited by a moderator:
Babu Asprin ni mkali duh!

 
Last edited by a moderator:
ah ah ah! umenichekesha sana.. kumbee eeh! babu wajukuu wako wasikurithi huo ujanja wako

 
ah ah ! eti korido

 
''Top layer'' has always been in my memory,sitaisahau ile siku paka alivyoibuka toka kwenye sufuria,,,nimemaliza 1990 i miss those moments,,
abdu hapa
Hahahahaah That paka LOL. Na watu wakapiga msosi kama kawa..!

Hahahaha manoah njoo upate story mpya.

Mkuu Sikonge, kuna siku nyau aliibuka kwa sufuria kwa Lugundi. Watu wakajifanya hawajaona wakapiga ubwabwa kama kawa! Hahahahahah dah!!
 
Last edited by a moderator:
Duu!!!! Sasa huyu Paka Nyau alikuwa bado hai au Marehemu? Damn.

Watu mkala wali na Top Layer yake bila kumjali Mzoga Paka na yeye alikuwa kapikwa?

Hebu huyu jamaa afafanue zaidi hii story ya Paka ...
 
Hebu funguka zaidi kuhusu PAKA kwenye Chungu. Kama umemaliza 90 basi wewe utakuwa Mzee mwenzangu maana nilikuacha mwaka wa Pili, 1989. Enzi hizo shida ilikuwa Maharage na zile Spinach, nilikuwa sizipendi kabisa.
''Top layer'' has always been in my memory,sitaisahau ile siku paka alivyoibuka toka kwenye sufuria,,,nimemaliza 1990 i miss those moments,,
abdu hapa
 
Hebu funguka zaidi kuhusu PAKA kwenye Chungu. Kama umemaliza 90 basi wewe utakuwa Mzee mwenzangu maana nilikuacha mwaka wa Pili, 1989. Enzi hizo shida ilikuwa Maharage na zile Spinach, nilikuwa sizipendi kabisa.

kama kawaida watu tulikuwa tunaenda kula jioni,,sa wazee wa top layer wakawa wanawahi kitu cha harage,kipindi mchuzi unakorogwa na yule mpishi nimemsahau jina,si paka akaibuka kwa juu,jamaa alichofanya ni kumtoa paka na kuendelea kukoroga,huko watu hawana mbavu kwani kuna raia wengine walikuwa wameshakua chakula,,yaani ilikuwa kelele 'top layer' 'top layer'
its true mkuu,,,,itabidi tufahamiane zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…