Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Uchaguzi 2020 Dar: Tundu Lissu akamatwa na Polisi, aachiwa bila masharti

Makumbele

Member
Joined
May 9, 2009
Posts
77
Reaction score
431
Taarifa za hivi punde ni kuwa Vyombo vya Dola jijini Dar vinamshikilia Ndg. Tundu A. Lissu.

Lissu amekamatwa muda mchache uliopita jijini Dar akiwa ameenda Ubalozi wa Ujerumani (amekamatiwa mbele Jengo la Umoja House).

Huu ni mwendelezo wa kukamata viongozi wa CHADEMA na ACT Wazalendo.

======
UPDATE: 1950hrs

Lissu ameachiwa bila masharti yoyote

=====

TAARIFA ZAIDI KUTOKA KWA MENEJA WA KAMPENI WA LISSU

Lissu akiwa na Katibu wake pamoja walinzi wake wawili alikamatwa akiwa nje ya Ubalozi wa Ujerumani ambapo alikuwa akisubiri kuonana na Balozi wa Ujerumani, Regine Hess aliyekuwa na miadi naye.

Taarifa zinaeleza kuwa Balozi alikuwa akiendelea kufanya some foreign clearance ili aweze kuonana na Lissu.

Lissu alishikiliwa kwa sababu zile zile za kuhamasisha na kuchochea maandamano ambayo yangesababisha uvunjifu wa amani.

Akiwa ameshikiliwa, inadaiwa kuwa Balozi wa Ujerumani alienda Central pia.

Lissu amehojiwa na kuachiwa na muda huu (saa mbili usiku) yuko nyumbani kwa Balozi wa Ujerumani.
 
Aliyekua mgombea urais wa CHADEMA Tundu Lissu akamatwa na jeshi la polisi.

Huu ni mwendelezo wa udhalimu wa serikali dhidi ya vyama vya upinzani na viongozi wake Tunaziomba jumuiya za kimataifa kuingilia Kati ili kuepusha maafa zaidi.
 
Aliyekua mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu akamatwa na jeshi la polisi akiwa nyumbani kwake Tegeta Dar es Salaam.

Huu Ni muwndeleza wa udharim wa serikali dhidi ya vyama vya upinzani na viongozi wake Tunaziomba jumuiya za kimataifa kuingilia Kati ili kuepusha maafa zaidi
Naona ulikua unawahi kuanzisha uzi kwa haraka mpaka ukafanya typing error ukajikuta uzi umeangukia kwenye comment.
 
Back
Top Bottom