KERO Dar: Usalama duni wa watoto wanaoenda kuogelea Jangwani Sea Breeze Beach, nani anawajibika?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Siku ya sikukuu ya Idd, watoto waliniomba niwapeleke eneo la kuogelea. Nilishauriana na mke wangu, naye akapendekeza tuwapeleke Jangwani Sea Breeze, kwani ni sehemu iliyo karibu, na pia watoto wamekuwa wakisikia ikitajwa na wenzao shuleni.

Nilikubali. Nikawasha gari, mimi na mke wangu tukaelekea eneo hilo lililopo Mbezi Beach, Dar es Salaam. Tulipofika, tulilipa kiingilio. Hata hivyo, tulipokuwa tunaulizia sehemu maalum ya watoto kuogelea, niliona watoto wadogo wamechangamana na watu wazima wakiogelea pamoja. Kwa kweli nilipigwa butwaa.

Katika bwawa la kuogelea (Swimming Pool), watoto walikuwa pamoja na watu wazima huku wanaume na Binti wakiwa hata wamekumbatiana na kuchezeana bila staha. Yote haya yalikuwa yanaendelea huku watoto wakishuhudia mubashara.

Baada ya kuona hali hiyo, nilimwambia mke wangu kuwa ni bora tuhesabu gharama ya kiingilio kama hasara. Nikawachukua watoto na kuelekea hoteli nyingine ya jirani ili waweze kuogelea katika mazingira salama.

Hata hivyo, nilibaki na maswali mengi na sikuamini nilichokiona. Hivyo, niliamua kutenga muda tena siku ya Pasaka, Aprili 5, 2026, ili kujiridhisha kama hali ile ilikuwa ya siku moja tu. Kwa bahati mbaya, nilichokiona mara ya pili kilikuwa kibaya zaidi bwawa lilikuwa limejaa kupita kiasi; haikujulikana mtoto ni nani wala mtu mzima ni nani. Inaonekana wasimamizi wanachojali zaidi ni kukusanya fedha, huku masuala ya usalama yakiachwa mikononi mwa wateja pekee bila kuzingatia uwepo wa watoto.

Niliondoka nikiwa na masikitiko makubwa hadi leo. Inasikitisha kuona baadhi ya wazazi wanawatuma watoto wao kwenda na wasaidizi wa kazi za nyumbani, ambao wakati mwingine baadhi yao huwatelekeza watoto hao waogelee peke yao huku wao wakijishughulisha na mambo yao. Hali hii inaongeza hatari kwa usalama wa watoto katika maeneo kama hayo. Hapo ndipo uzito wa hoja yangu kuwa wamiliki nao wanatakiwa kuwajibika na suala la usalama hasa wa watoto.

Aidha, mazingira hayo yalinifanya nitafakari juu ya hatari za kiafya kwa watoto hata watu wazima. Bwawa lilikuwa linatumiwa na watu wengi kwa wakati mmoja bila usafi wa maji kudumishwa ipasavyo. Hii inaweza kusababisha hatari ya magonjwa mbalimbali, hasa ya ngozi, kutokana na msongamano mkubwa niliouona.

Nitoe wito

Kwa kuwa ushahidi upo na tatizo hili linaonekana kujirudia mara kwa mara, naomba kutoa wito kwa mamlaka husika, ikiwemo Wizara inayosimamia ustawi wa watoto, chini ya Waziri Dorothy Gwajima, kulifuatilia kwa kina na kuchukua hatua stahiki.

Vilevile, mamlaka nyingine zikiwemo zinazotoa vibali, zinapaswa kufuatilia kwa makini hali hii na kuwachukulia hatua wahusika ili kulinda ustawi wa jamii, hususan watoto. Bila hatua madhubuti, tutaendelea kuhatarisha usalama wa watoto na afya za wananchi kwa ujumla.

Mamlaka waasimamie viwango madhubuti vya uendeshaji wa maeneo ya kuogelea, hasa yanayotumiwa na watoto. Lakini ni muhimu kuhakikisha uwepo wa walinzi na wasimamizi waliopata mafunzo ya usalama wa maji pamoja la uangalizi wa watoto kwenye maeneo yanayotoa huduma hizo.
 
Duh sasa hapo wanaogelea au mateso 😄
Kwa tz sijaogelea kwenye swimming pool miaka mingi sana sana
Pool zangu zilikuwa ile ya kilimanjaro hotel(pool side)
Na swimming pool ya udsm
Ila ya udsm kwa sasa sijui ina hali gani nayo 😄

Ova
 
View attachment 3572923

View attachment 3572924

Hapo full UTI 😄

Ova
 
Duh sasa hapo wanaogelea au mateso 😄
Kwa tz sijaogelea kwenye swimming pool miaka mingi sana sana
Pool zangu zilikuwa ile ya kilimanjaro hotel(pool side)
Na swimming pool ya udsm
Ila ya udsm kwa sasa sijui ina hali gani nayo 😄

Ova
Ziko kama Golden Tulip huwa nawapeleka watoto, sio mbaya sana lakini sio weekend kunajaa sana
Hata White Sands sio mbaya sana, ila tu kuna malaya wengi wanakaa pale kwenye viti vya swimming pool kutafuta madanga ya kichina.
 
Ndugu njoo Zenji ufurahi ww na familia yako dereva wa tours nipo
 
Sehemu wamepangilia vizuri ni funcity kigamboni...wao kuna sehemu ya kuogelea ya watoto na ya wakubwa.....angalau kule pamekaa vizuri...jPo siku za sikukuu pia watoto tu wanamuwa wengi sana japo huwezi kukuta msongamano na watu wazima kama hvyo....
 
Back
Top Bottom