Kilbark
JF-Expert Member
- Feb 25, 2008
- 572
- 168
Kila nikisikia hili la mlimani city huwa nakasirika lakini nifanyeje. Unaweza kujionea hali halisi ya msongamano wa wanafunzi chuo kikuu madarasani na vyumbani. Hawa viongozi wetu wakaamua wahodhi ardhi kwa miaka 100 ili iwe kituo cha biashara badala ya kujenga vitengo vya utafiti, madarasa, nyumba za walimu , wafanyakazi na hata wanafunzi. Jiulize hao jamaa wanapata faida gani hapo. Huu (Mlimani city )ni uoza mwingine ambao utakuja kuwekwa hewani muda sio mrefu