Dar: Wabunge 19 wa Viti Maalum waliovuliwa uwanachama na CHADEMA, Kuongea na Wanahabari

Status
Not open for further replies.
Kama Ni suala la maadili mabovu basi lianze na Mbowe..ni kwanini alikuwa anawapa kibali kila hatua...na barua ikapelekwa NEC..Sasa hapa imekuwa shida
 
Dada Halima, mtoto akijinyea, kama anaufahamu kidogo, atabaki bila kugaragara mpaka hausigeli aje kumnasua na kumtakasa. Kwa kadiri anavyokukulika kitandani ndivyo anavyozidi kujipaka mavi. Mimi nakushauri kwa sasa usingeongea chochote na yeyote. Tulia kwanza upime upepo unavyokwenda na upate hekima ya nini cha kuongea kwa wakati huu na jinsi ya kukiongea huku ukijua audience yako. Ukimuuliza mzee Jemsi atakueleza hivyohivyo!
 

Mkuu hii inaitwa maji kuzidi unga. Hapo ni mwendo wa uji tu. Ugali hausongeki tena!
 
Mdee utambana na cdm lkn kamwe hutashinda. Mungu atakuadhibu tu, cdm wewe Ni Kama mzazi wako maana imekulea. Amin laana itakuja kukuangukia tu. Amin hata ccm wewe hawakuamini Sana wanajua we Ni mtoto halali wa cdm. Sio wa kuasili Kama bulaya.
 
MODS NAOMBA MSIUUNGANISHE HUU UZI. Huu uzi ni wa kipekee kabisa wenye mapenzi mema kwa Mdee na wenzake 18 na CHADEMA. Binafsi mimi naipenda sana chadema japo sio mwanachama. Halima Mdee na wenzake waliamua kubeti na bahati mbaya mkeka umechanika. Hivyo nawaomba wajishushe, waombe radhi na chedema pamoja na wapenzi wake tutawasamehe. Hela tamu jamani, hata mimi ningekuwa kwenye nafasi yake ningesaliti tu. Bahati mbaya amesaliti na ameshindwa kuyapata matunda ya usaliti, hivyo ni bora atubu na atasamehewa. Halima umelala jela kwa sababu ya chadema, umepigwa, umeumizwa na kudhalilishwa kwa ajili ya chadema, hivyo kosa lako moja haliwezi kuyafuta mema yote uliyokifanyia chama. Hakuna aliye mkamilifu chini ya jua. Hata Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha sembuse wewe! Halima tumekuelewa shida sio kwamba huna mapenzi na chadema, shida ni tamaa ya fedha hivyo tafadhali dada angu omba msamaha na hakika utasamehewa. Ni hayo tu dada angu.
 
Yaani na ule mzigo auachie..aaahh acha masihara..!!
 
waliobaki chadema wenyewe wanatamani asubuhi na usiku zali la kina mdee

lingewaangukia wao,watu wanajikaza tu pale ila mioyo ina tamani mengi sana
 
Ninauhakika uko anakoelekea atafutika mapema mno kwenye ulimwengu wa siasa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…