Mimi natokea Kitunda mkuu, huwezi amini hii barabara ni kama mwaka wa 2 sasa toka tuanze kusikia kuna wakandarasi wameshapewa tenda lkn cha ajabu hatuoni chochote kinachoendelea
Hii barabara ni kero kubwa sana kiongozi, Kwanza ni ya vumbi, Pili ina mashimo vbaya sana ukipanda Bajaji tu mpaka ufike kwako Mgongo wote unauma kwa kurushwa rushwa kwenye mashimo.
Tatu ni kwamba haina madaraja ya kuaminika hii barabara hivyo kipindi cha mvua kama hivi ni janga usafiri unakwama hadi kulazimika watu kuvuka kwa miguu[emoji22]
Hawa wakandarasi Wanastahili kabisa kuwekwa ndani maana naona kabisa hawana nia njema na wananchi
Daraja la hapa Kitunda tu wamemaliza miaka 2 na bado hawajakamilisha, yaani kuweka level tu Daraja lianze kutumika wameshindwa hiiii hiiiiii [emoji3].... sasa hawa wasipowekwa Ndani watajifunza Lini??
Wakandarasi Wazawa ni Jipu sana bora mara 10 Tenda hizi wapewe wakandarasi wa nje tu mana wako serous na Kazi.