Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Jeshi la Polisi Kinondoni limesema limefanikiwa kuwakamata Wafanyakazi wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communication-Kitengo cha Matangazo kwa tuhuma za kutuma taarifa za uongo na uzushi kuhusu #COVID19
Limesema waliokamatwa ni Hidari Hakimu (27), Afisa Biashara kwenye Kampuni hiyo ambaye ni mkazi wa Kigamboni pamoja na Alona Tarimo (42), Afisa Biashara ambaye ni mkazi wa Masaki
Hidari anadaiwa kuandika katika WhatsApp “Za chinichini kuna Padri wa Peramiho amefariki na Ugonjwa wa Corona. Alitokea Italia, akakaa Dar kidogo kisha akaelekea Mbeya kwa kutumia ndege na baadaye akatumia ‘private’ kuelekea Songea. Akazidiwa akawa ICU kule Peramiho na sasa amefariki. Waliomuhudumia wamewekwa katantini.”
Polisi wameeleza kuwa ujumbe huo uliotumwa Aprili 5, 2020 uliungwa mkono siku hiyo hiyo na Alona aliyeposti katika kundi hilo hilo la WhatsApp kuwa “Hizi Kigogo hajazipata ili aposti, then Serikali waweke wazi.”
Alona naye kwa kutumia simu yake Aprili 29, 2020 anadaiwa kutuma ujumbe katika mtandao wa WhatsApp unaosema “Mbezi Beach karibu na Kanisa la Mloganzila kuna Mzee kaondoka na Corona. Sorry Mloganzila Katoliki nimedata yaani."
Polisi wamefafanua kuwa Watuhumiwa hawa walituma taarifa hizo katika mitandao huku wakifahamu fika taarifa hizo ni za uzushi na uongo na hazina ukweli wowote