Kwamba wameajiriwa watu kujiunga kwenye makundi hayo yote?
Hao watu uliowasema wapo lakini ni wachache sana, kuanzia leo nikupe taarifa simu yako ikidukuliwa basi mdukuaji anaona na kusikia kila kitu kama wewe unavyoona na kusikia kupitia simu yako. Ni kama vile simu yako ipo mikononi mwake pia.
Hiyo End-To-End Encryption inasaidia mawasiliano yanayodakwa au kuchotwa juu kwa juu wakati ujumbe unasafirishwa toka kwa mtumaji hadi kwa mpokeaji, lakini upande wowote wa mtumaji na mpokeaji ujumbe unakuwa umefunguliwa code yani unakuwa decoded au deciphered unakuwa plain text ili mwenye kifaa(simu) aweze kuusoma au kusikia au kuona.
Kwa hivyo kama kadukuliwa mtumaji au mpokeaji basi kila kitu kinasomeka au kuonekana wazi kwa mdukuaji.