Dar: Wahalifu wavamia mtaa, wapora mali & fedha, wapiga watu mapanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WATU watano wamejeruhiwa huku mmoja akiwa mahututi baada ya kundi la vijana kuvamia mtaa wa Tagusako, Tabata jijini Dar es Salaam, kupora mali na fedha taslimu."

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, mashuhuda na viongozi wa mtaa huo, walisema vijana hao wakiwa na silaha za jadi waliwakata kwa mapanga waendesha bodaboda watatu na wananchi wawili, huku wengine wakikatwa vidole.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, Peter Joakimu, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 28, mwaka huu, majira ya saa tano usiku na kundi hilo la vijana lililokuwa limebeba silaha kama visu na mapanga.

Alisema wanamshikilia mtu mmoja ambaye alionekana na watuhumiwa hao.

"Kweli vijana hao walifanya uhalifu huo, waliwaumiza wananchi watatu pamoja na vijana wawili wa bodaboda ambao kati yao mmoja anafahamika kwa jina la Nelson Aruya (30), ambaye mpaka sasa hali yake sio nzuri amelazwa Hospitali ya Amana,” alisema Joakimu.

Mwenyekiti huyo alisema kundi hilo la wahalifu lilivamia maduka na kupora fedha na kuwanyang’anya simu za kiganjani wananchi.

"Wahalifu hao walivamia wateja waliokuwa kwenye baa ya Shooters Pub, na kuanza kuwakata mapanga kichwani na kuwakatakata viungo vya mwili wateja waliokuwapo na kuwaamuru walale chini,” alisimulia.

Alisema walishirikiana na Kituo cha Polisi Tabata na kumpata mhusika mmoja ambaye majira ya mchana siku ya tukio, alionekana na watuhumiwa wengine nyumbani kwake.

Hata hivyo, alipofikishwa kituoni alibainika kuwa sio mkazi wa eneo hilo.

Mjumbe wa eneo hilo, Saida Mashine (60), alisema vijana hao walivamia eneo hilo mapema wakati baadhi ya wananchi wakiwa hawajafunga biashara zao.

"Nilikuwa nipo ndani nikasikia kelele nje nilipotoka nikamkuta kijana mmoja wa bodaboda anatoka damu nyingi kichwani na mkononi, huku akiwa anapiga kelele anakimbia ikanilazimu nifanye utaratibu apelekwe hospitali huku nikiwa nimeishikilia pikipiki yake,” alisema Mashine.

Tukio hilo alidai limeathiri uchumi wa eneo hilo baada ya kuwapora wananchi fedha na mali zilizokuwa kwenye biashara zao.

Mmoja wa majeruhi, aliyekatwa mapanga kichwani na kukatwa kidole cha mkono Abduli Salum Maketa (35), alisema vijana hao walimvamia akiwa anashusha abiria na kupora simu na fedha alizokuwa nazo.

"Nilikuwa nimesimama nasubiri abiria anilipe pesa nikaona kundi la watu linakuja nikidhani ni ulinzi shirikishi waliponikaribia wakatoa mapanga wakaniambia nitoe simu pamoja na pesa nilizokuwa nazo hapo tayari wamenipiga panga la kichwa nikawa sijitambui nikakimbizwa hospitali,” alisema Maketa.

Naye dada wa majeruhi, Sara Aruya, alisema hali ya mdogo wake sio nzuri anaendelea na matibabu Hospitali ya Amana.

"Nelson hali yake sio nzuri alikatwa mapanga mawili kichwani vile vile alikatwa kidole cha mkono ninavyokuambia hata kuongea kwake ni kwa shida, tunaomba serikali isimamie jambo hili kusudi hawa wanaofanya uhalifu huu wadhibitiwe,” alisema.

Shuhuda mwingine Sofia Hamisi, alisema alikuwa anaelekea nyumbani na kuvamiwa na vijana hao ambao walimpora simu na kutishia kumchoma kisu.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi wamedai kuhofia kutoka nje, huku wakiliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi kutokana na kuongeza kwa matukio ya uhalifu.

Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Willium Mponda, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa askari wanawasaka waliohusika na wanawashikilia watu kadhaa.

Source: Nipashe
 
Hiyo grocery ya Shooters wanakaa watu wachovu TU...hao vijana hawajui kutageti hela
Wana silaha za jadi. Utavamia wenye hela na silaha za jadi?
 
Hali ya maisha imekuwa ngumu sana kwa kweli ndio matokeo haya. Ila nashauri, hao vijana inatakiwa wauliwe angalau watano tu watapunguza hizo tabia

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hilo sio suluhisho.Utaua bado watajitokeza wengine ambao wala hawatajali historia.ndo maana matukio ya uhalifu hayajawai kuisha duniani kwasababu kila mtu ana sababu yake yakufanya uhalifu.Matukio ya uhalifu wakupora mali yatapunguzwa zaidi kwakuboresha maisha ya watu sio zaidi ya hapo.
 
Waje hapa ibungu mabibo ni karibu hawa walevi wanapiga kelele usiku kucha.
 
  • Kicheko
Reactions: Cyn
Poleni wakazi wa mzizima.

Dar bila mishe maisha ni magumu sana.
Hao vijana kazi hawana, bodaboda sasa hivi nayo kuipata mpaka connection.
Ajira ngumu kwakweli.
 
yaanii vyuma vimekazaa hadi unatamani 24hrs kuwe mchana wa jua/mbalamweziii manake usiku nao unatishaa
 
Uko

Sahihi

Wanunuzi wa Simu za mkononi wajiandae kudakwa kama ndio wahusika wa tukio

Usinunue simu ya mkononi kama hutaki shida maishani

Ukidakwa wewe ndie mkata mapanga
Wajanja wanauza spea tu siku hizi, bodi wanzitupa
 
Poleni wakazi wa mzizima.

Dar bila mishe maisha ni magumu sana.
Hao vijana kazi hawana, bodaboda sasa hivi nayo kuipata mpaka connection.
Ajira ngumu kwakweli.
Mimi huwa nawashangaa kama dar hawana kazi za kueleweka si warudi makwao
 
WATU watano wamejeruhiwa huku mmoja akiwa mahututi baada ya kundi la vijana kuvamia mtaa wa Tagusako, Tabata jijini Dar es Salaam, kupora mali na fedha taslimu."

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, mashuhuda na viongozi wa mtaa huo, walisema vijana hao wakiwa na silaha za jadi waliwakata kwa mapanga waendesha bodaboda watatu na wananchi wawili, huku wengine wakikatwa vidole.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, Peter Joakimu, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 28, mwaka huu, majira ya saa tano usiku na kundi hilo la vijana lililokuwa limebeba silaha kama visu na mapanga.

Alisema wanamshikilia mtu mmoja ambaye alionekana na watuhumiwa hao.

"Kweli vijana hao walifanya uhalifu huo, waliwaumiza wananchi watatu pamoja na vijana wawili wa bodaboda ambao kati yao mmoja anafahamika kwa jina la Nelson Aruya (30), ambaye mpaka sasa hali yake sio nzuri amelazwa Hospitali ya Amana,” alisema Joakimu.

Mwenyekiti huyo alisema kundi hilo la wahalifu lilivamia maduka na kupora fedha na kuwanyang’anya simu za kiganjani wananchi.

"Wahalifu hao walivamia wateja waliokuwa kwenye baa ya Shooters Pub, na kuanza kuwakata mapanga kichwani na kuwakatakata viungo vya mwili wateja waliokuwapo na kuwaamuru walale chini,” alisimulia.

Alisema walishirikiana na Kituo cha Polisi Tabata na kumpata mhusika mmoja ambaye majira ya mchana siku ya tukio, alionekana na watuhumiwa wengine nyumbani kwake.

Hata hivyo, alipofikishwa kituoni alibainika kuwa sio mkazi wa eneo hilo.

Mjumbe wa eneo hilo, Saida Mashine (60), alisema vijana hao walivamia eneo hilo mapema wakati baadhi ya wananchi wakiwa hawajafunga biashara zao.

"Nilikuwa nipo ndani nikasikia kelele nje nilipotoka nikamkuta kijana mmoja wa bodaboda anatoka damu nyingi kichwani na mkononi, huku akiwa anapiga kelele anakimbia ikanilazimu nifanye utaratibu apelekwe hospitali huku nikiwa nimeishikilia pikipiki yake,” alisema Mashine.

Tukio hilo alidai limeathiri uchumi wa eneo hilo baada ya kuwapora wananchi fedha na mali zilizokuwa kwenye biashara zao.

Mmoja wa majeruhi, aliyekatwa mapanga kichwani na kukatwa kidole cha mkono Abduli Salum Maketa (35), alisema vijana hao walimvamia akiwa anashusha abiria na kupora simu na fedha alizokuwa nazo.

"Nilikuwa nimesimama nasubiri abiria anilipe pesa nikaona kundi la watu linakuja nikidhani ni ulinzi shirikishi waliponikaribia wakatoa mapanga wakaniambia nitoe simu pamoja na pesa nilizokuwa nazo hapo tayari wamenipiga panga la kichwa nikawa sijitambui nikakimbizwa hospitali,” alisema Maketa.

Naye dada wa majeruhi, Sara Aruya, alisema hali ya mdogo wake sio nzuri anaendelea na matibabu Hospitali ya Amana.

"Nelson hali yake sio nzuri alikatwa mapanga mawili kichwani vile vile alikatwa kidole cha mkono ninavyokuambia hata kuongea kwake ni kwa shida, tunaomba serikali isimamie jambo hili kusudi hawa wanaofanya uhalifu huu wadhibitiwe,” alisema.

Shuhuda mwingine Sofia Hamisi, alisema alikuwa anaelekea nyumbani na kuvamiwa na vijana hao ambao walimpora simu na kutishia kumchoma kisu.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi wamedai kuhofia kutoka nje, huku wakiliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi kutokana na kuongeza kwa matukio ya uhalifu.

Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Willium Mponda, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa askari wanawasaka waliohusika na wanawashikilia watu kadhaa.

Source: Nipashe
Wameamua kula kwa urefu wa kamba. Ili mradi wasivimbewe. Sasa wao wale wapi jamaniiii
 
Back
Top Bottom