Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Nimeongea kwa mujibu wa mwanaikolojia kutoka The Hill!
 
lava flow? volcano erupt? mud flow? au land slide? we jamaa kilaza sana
 
Nimeongea kwa mujibu wa mwanaikolojia kutoka The Hill!
Hawa wasomi wa vitabuni, hakuna kitu!, kule Oldonyo Lengai, kabla ya ule moshi wa majivu, wanyama wote wa porini waakwisha timka, wakabaki ngombe na mbuzi!, hao ma geologist, walikuwa wapi?.
Unakumbuka issue ya Tetemeko la Bukoba,


Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!
 
Wananchi wameamliwa kuhama na eneo lote lenye tope litazungushiwa utepe mwekundu!
Kwa vile hawajui chanzo cha tope hilo, ni muhimu kuchukua tahadhari zote, ila hawa wa jeologia wetu, hakuna kitu kabisa!.
Kitu cha kwanza, sio kukimbilia kuhamisha watu hapo, hapo hilotope linapotokea ni upenyo tuu kama ilivyo chemchem, eneo lenye hatari ni kwenye mkondo wa maji ambalo ndio hilo tope linakotokea, kwa lugha nyingine huko chini ardhini kuna njia za maji, ardhi oevu, water table na mito ya maji tope ya chini kwa chini kama stalactite na stalagmite katika mapango ambayo ni semi permeable rocks za mapango ya chini kwa chini ni njia za mito ya chini kwa chini, hii mito inatabia ya kuhama hama, na kuacha njia ya awali inayogeuka pango. Huko udongo tope unakotokea ndiko kwenye hatari kuliko hapo unapoibukia, kule ndiko mapande ya udongo yataporomoka kuziba nafasi, kutengeneza mabonde ya ufa. Mfano hapo kwangu, kwa juu ni udongo wa kawaida ila hadi uchimbe sana ndio unakutana na huo mfinyanzi tena udongo msafi wa kijivu. Udongo tope huo una rutuba balaa kutokana na kitu kinachoitwa siltation, ukiuchukua ni kama mbolea super!.

P
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!.
 
Ahsante kwa elimu nzuri mkuu!
 
Congo imewahi kulipuka volcano magari,nyumba na mimea iliharibika
Volcano za milima ya Congo DRC unitia wasiwasi sana, siku moja panaweza kutokea majanga kama yaliyo ikumba Italy miaka ya zamani sana baada ya mlima/mji wa Pompeii kulipuka na kuua/unguza wakazi wote wa mji huo na mali zao zote including nyumba
 
Volcano za milima ya Congo DRC unitia wasiwasi sana, siku moja panaweza kutokea majanga kama yaliyo ikumba Italy miaka ya zamani sana baada ya mlima/mji wa Pompeii kulipuka na kuua/unguza wakazi wote wa mji huo na mali zao zote including nyumba.

mkuu 2003 ilitokea hadi ndege ziliungua, ila haikuwa deadly kama hiyo unayosema ya Italy ambayo sijawahi kuisikia kabla ngoja nikatafute huko youtube najua wenzetu lazima wali record
 

We have scientists who can tell us the nature of the problem and the solution. So far mkuu wa mkoa yuko sahihi
 

Hiyo sehemu siku za mbele inaweza kutitia au kutengeneza shimo.... Hao raia wenye makazi hapo Ni heri waondoke kabla ya majanga ikitokea....
 
Yawezekana eneo hilo kuna akiba ya gesi/mafuta hivyo yanalazimisha kupandisha tope zito litoke nje kwanza.
Wataalamu wetu wafanye utafiti ikiwezekana drilling ya mita kama 300 chini kubaini layers za chini zikoje.
Hii inawezekana sababu eneo lenyewe liko karibu kutoka usawa wa Bahari na ni eneo chepe chepe/chem chem.
 
Elimu ya Tanzania ingekuwa ni bora hadi hivi sasa tungepata Majibu wa Kitaalam, ila tatizo ni kwamba Watanzania wengi tunasoma kupata GPA tu.
 
... Let's wait for Geological Survey of America achana na wawinda teuzi Chief.
Hii kali ya mwaka - tukimbilie tena mabeberu kupatiwa taarifa ya geological survey - mkuu hiyo itakuwa ngumu kwa kuwa hapakutoea seismic shock wave yakuwa registered by Ritcher au Kainamori sensors/transducers, hivyo si raisi Uncle SAM kubaini kilicho tokea Kunduchi - my opinion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…