Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Dar: Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope, watakiwa kuhama

Duh, kumbe wewe somo la jiogirafia limekupita pembeni, ukanda wa pwani tangulini ukawa na volkano?, Volcano ni uji wa mawe unaitwa magma ni ya moto na hutanguliwa na moshi wenye jivu jeupe kama vumbi, magma hiyo hutoka chini na moto wake ikifika ardhini hutiririka na kupoa na ndio hujenga milima ya volcano, kama Mt. Kilimanjoro, Mt. Meru na Oldonyo Lengai, kuna aina tatu za volcano, hai, pozo na mfu. Kilimanjaro ni mfu, Meru ni pozo na Oldonyo Lengai ndio hai. Mfu hailipuki tena, imekufa, pozo, imetulia siku ya siku ikifika, itacharuka, haini kule chini magma ya moto inaendelea kuchemka ila haijalipuka.

Hilo tope baridi sio la volcano, hilo ni la mitetemo tuu, kutokana vi tetemeko vya chini kwa chini!, japo mimi sio mjeolojia, lakini najua kwa kuliona tuu kwa macho, eneo hilo ni eneo la mkondo wa maji, tope hilo ni udongo wa mfinyanyanzi, ulio chini ya mkondo huo wa maji, ambao chini yake una mwamba uliokuwa semi permeable rocks, ambao siku zote unapitisha maji kwenda chini ardhini kwenye mkondo wa maji, sasa kutokana na mvua, water table ime raise, above ile semi permeable rock, hivyo kina cha maji huko chini ardhini kimepanda, sasa na kutoka juu kama chemchem, kutoka na mfinyanzi huo huko jini kuloa, umekuwa uji, hivyo sasa uji wa tope la chemchem, ndio linakuwa pushed juu na ile water table.

Water table ikija kushuka, yale maeneo ya ulipotoka huo mfinyanzi, kutakuwa na hollow pots, mvua ikinyesha na kupalowewesha udongo wa juu, utaporomoka, kama kuna nyumba zinapiga ufa hadi msingi!.

Nimeyajua haya kutokana na mimi kibanda changu pia nimejenga juu ya mkondo wa maji na chinikuna udongo wa mfinyanzi, fundi aliyenijengea, alishauri nijenge msingi wa jamvi la nondo kama msingi wa ghorofa, mimi nikamgomea, si unajua tena Wasukuma tulivyo wabishi, nikamwambia fundi, sijawahi kuona jamvi la nondo nyumba ambayo sio ya gharofa, nikalazimisha ajenga tuu, kikawaida. Fundi akajenga kwa shingo upande!. Nikahamia, mwaka uliofuta mvua za elninyo zikashuka!, kumbe kwangu ni water way, upande wa nyuma kwa jirani yangu, maji yamefika hadi dirishani, akaniomba nibomoe ukuta wangu ili kuyaruhusu yapite.

Kwa ubishi ule ule wa Kisukuma, nikamgomea, kuwa kila mtu kauziwa kiwanja kivyake, hivyo kila mtu atafute pa kuyapeleka maji yake!.
Within two days, maji ukuta jirani yamefika juu ya dirisha, kwa jirani wamehama kila kitu kimeloa, huku yamezuiwa na ukuta wangu!, Kumbe chini kunazidi kulowa na after two days, huku kwangu kukaibuka chemchemi ya matope pembeni ya ukuta wote, yale maji ya jirani yanazama jini ya ukuta na kuibukia kwangu.

Nikamuita fundi wangu, akasema lazima tubomoe ukuta kuyapa maji ya jirani njia, nikamgomea, ndipo akaniambia kutatokea mambo mawili.
1. Ukuta utaloa, utazidiwa nguvu, maji yatafunja huo ukuta, na kutoka na presha, ukuta ukianguka utabomoa nyuma na presha ya maji nyuma yangu itazolewa!.
2. Kwa sababu chini ni mfinyanzi, una very high water retaining capacity, utakuwa tepetepe, na nilijenga msingi bila nondo, nyumba itaanza kutitia na kupiga nyufa kwenye msingi, mwisho itabomoka!.

Ndipo nikakubali, tukabomoa ukuta wangu kujenga tundu la kupitishia hayo hayo maji, kiukweli hiyo pressure, ili fumua karibu ukuta wote, ule msala wa maji sasa ndio yakajaa kwangu, ikabidi na ukuta wa mbele kutoboa kuyaachia maji njia yake, yalikata hadi barabara!.
After two years nyumba ilipiga bonge la crack kwenye msingi, fundi akanionyesga, kweli nyumba ilikuwa inatitia!. Hivyo nikakubali matokeo!,


P

Nimeongea kwa mujibu wa mwanaikolojia kutoka The Hill!
 
lava flow? volcano erupt? mud flow? au land slide? we jamaa kilaza sana
 
Nimeongea kwa mujibu wa mwanaikolojia kutoka The Hill!
Hawa wasomi wa vitabuni, hakuna kitu!, kule Oldonyo Lengai, kabla ya ule moshi wa majivu, wanyama wote wa porini waakwisha timka, wakabaki ngombe na mbuzi!, hao ma geologist, walikuwa wapi?.
Unakumbuka issue ya Tetemeko la Bukoba,


Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!
 
Wananchi wameamliwa kuhama na eneo lote lenye tope litazungushiwa utepe mwekundu!
Kwa vile hawajui chanzo cha tope hilo, ni muhimu kuchukua tahadhari zote, ila hawa wa jeologia wetu, hakuna kitu kabisa!.
Kitu cha kwanza, sio kukimbilia kuhamisha watu hapo, hapo hilotope linapotokea ni upenyo tuu kama ilivyo chemchem, eneo lenye hatari ni kwenye mkondo wa maji ambalo ndio hilo tope linakotokea, kwa lugha nyingine huko chini ardhini kuna njia za maji, ardhi oevu, water table na mito ya maji tope ya chini kwa chini kama stalactite na stalagmite katika mapango ambayo ni semi permeable rocks za mapango ya chini kwa chini ni njia za mito ya chini kwa chini, hii mito inatabia ya kuhama hama, na kuacha njia ya awali inayogeuka pango. Huko udongo tope unakotokea ndiko kwenye hatari kuliko hapo unapoibukia, kule ndiko mapande ya udongo yataporomoka kuziba nafasi, kutengeneza mabonde ya ufa. Mfano hapo kwangu, kwa juu ni udongo wa kawaida ila hadi uchimbe sana ndio unakutana na huo mfinyanzi tena udongo msafi wa kijivu. Udongo tope huo una rutuba balaa kutokana na kitu kinachoitwa siltation, ukiuchukua ni kama mbolea super!.

P
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!.
 
Kwa vile hawajui chanzo cha tope hilo, ni muhimu kuchukua tahadhari zote, ila hawa wa jeologia wetu, hakuna kitu kabisa!.
Kitu cha kwanza, sio kukimbilia kuhamisha watu hapo, hapo hilotope linapotokea ni upenyo tuu kama ilivyo chemchem, eneo lenye hatari ni kwenye mkondo wa maji ambalo ndio hilo tope linakotokea, kwa lugha nyingine huko chini ardhini kuna njia za maji, ardhi oevu, water table na mito ya maji tope ya chini kwa chini kama stalginite na stalactites katika mapango, mapango ya chini kwa chini ni njia za mito ya chini kwa chini, hii mito inatabia ya kuhama hama, na kuacha njia ya awali inayogeuka pango. Huko udongo tope unakotokea ndiko kwenye hatari kuliko hapo unapoibukia, kule ndiko mapande ya udongo yataporomoka kuziba nafasi, kutengeneza mabonde ya ufa. Mfano hapo kwangu, kwa juu ni udongo wa kawaida ila hadi uchimbe sana ndio unakutana na huo mfinyanzi tena udongo msafi wa kijivu. Udongo tope huo una rutuba balaa kutokana na kitu kinachoitwa siltation, ukiuchukua ni kama mbolea super!.

P
Ahsante kwa elimu nzuri mkuu!
 
Congo imewahi kulipuka volcano magari,nyumba na mimea iliharibika
Volcano za milima ya Congo DRC unitia wasiwasi sana, siku moja panaweza kutokea majanga kama yaliyo ikumba Italy miaka ya zamani sana baada ya mlima/mji wa Pompeii kulipuka na kuua/unguza wakazi wote wa mji huo na mali zao zote including nyumba
 
Volcano za milima ya Congo DRC unitia wasiwasi sana, siku moja panaweza kutokea majanga kama yaliyo ikumba Italy miaka ya zamani sana baada ya mlima/mji wa Pompeii kulipuka na kuua/unguza wakazi wote wa mji huo na mali zao zote including nyumba.

mkuu 2003 ilitokea hadi ndege ziliungua, ila haikuwa deadly kama hiyo unayosema ya Italy ambayo sijawahi kuisikia kabla ngoja nikatafute huko youtube najua wenzetu lazima wali record
 
RC wa Mkoa wa Dar Es Salaam Aboubakar Kunenge awataka baadhi ya wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimeathiriwa na uji wa tope la volcano kuhama katika eneo hilo.

Chanzo ITV

My take: Hiki ni kitu gani au ndio dalili ya volcano na madhara yake ni nini?

We have scientists who can tell us the nature of the problem and the solution. So far mkuu wa mkoa yuko sahihi
 
Ni kawaida ya wasomi wetu ila mi ninavyofahamu lile eneo kwa wenyeji ni eneo ambalo linaonyesha lina maji mengi sana na ndio mana zile nyumba za pale bemaco zimetitia na hata ukienda mpaka eneo la kanisa la kkkt kile kidogo kilititia kabla la hilo kubwa kujenga na hata nyumba zilizopo maeneo ya kuanzia pale kwa Mwalimu dachi zote zinaonyesha kumezwa ila kwa Volcano sijui japo nilikuta maneno ya watu wanasema hivyo ila swali langu linabaki vile vile inamana Volcano mtu akizama ukimtoa haungui kumbe

Hiyo sehemu siku za mbele inaweza kutitia au kutengeneza shimo.... Hao raia wenye makazi hapo Ni heri waondoke kabla ya majanga ikitokea....
 
Yawezekana eneo hilo kuna akiba ya gesi/mafuta hivyo yanalazimisha kupandisha tope zito litoke nje kwanza.
Wataalamu wetu wafanye utafiti ikiwezekana drilling ya mita kama 300 chini kubaini layers za chini zikoje.
Hii inawezekana sababu eneo lenyewe liko karibu kutoka usawa wa Bahari na ni eneo chepe chepe/chem chem.
 
Elimu ya Tanzania ingekuwa ni bora hadi hivi sasa tungepata Majibu wa Kitaalam, ila tatizo ni kwamba Watanzania wengi tunasoma kupata GPA tu.
 
... Let's wait for Geological Survey of America achana na wawinda teuzi Chief.
Hii kali ya mwaka - tukimbilie tena mabeberu kupatiwa taarifa ya geological survey - mkuu hiyo itakuwa ngumu kwa kuwa hapakutoea seismic shock wave yakuwa registered by Ritcher au Kainamori sensors/transducers, hivyo si raisi Uncle SAM kubaini kilicho tokea Kunduchi - my opinion.
 
Back
Top Bottom