ALEX_ANDER
JF-Expert Member
- Jul 8, 2014
- 570
- 816
Nimeongea kwa mujibu wa mwanaikolojia kutoka The Hill!
Kamati ya amani au ya matapeli ya dini?Natoa wito kwa kamati ya amani mkoa wa Dsm inayoongozwa na alhad Mussa Salum dua zao zisiishie kwa wanasiasa tu bali wazielekeze kwa jamii nzima.
Kunduchi mtongani kuna tishio la makanisa takribani matano kuzolewa na tope baridi la volcano.
Makanisa hayo ni KKKT, Anglican, Katoliki, Sabato na Pentecoste yaliyo karibu karibu katika eneo linalonyemelewa na tope maji la volcano.
Ninajua shehe alhad Salum na msaidizi wako askofu Gamanywa mnapita hapa Jf, Tafadhali sana kamati yenu izuru eneo la maafa hapo kunduchi mtongani kwa diwani Urio.
Maendeleo hayana vyama!
Huko sahihi mkuuHakuna volcano hapo, ni kuhamisha mijadala ya mambo ya kitaifa
Wizi wa kura
Mauaji Zanzibar
Kibano cha kimataifa
etc
Eti wataalamu wapige kambi kapige mwenyewe nyumba zinazama unataka na wataalamu wetu wazame hapo kwenye kambi?baadhi ya nyumba zimezama na nyingine zinabomoka. Wataalamu wanaonekana kutoa maelezo ya nadhalia badala ya kupiga kambi eneo hilo na kufanya uchunguzi wa kina.
Polisi wa bongo huwa wanajiona wanafit kila mahali
Huwa wanajidai wanajua kila kitu wakati wengine Ni mbumbumbu tu kwenye Mambo ya kitaaluma
Waache kuingilia fani za watu
Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Udsm hakuna kituKuwahamisha waliopo kwenye mkondo huo si suluhisho wakati haujui nini kinaendelea chini ya ardhi eneo hilo, ni sawa na kikitoboa kipele cha jipu ukadhani umepata suluhisho kumbe jipu linakua kwa ndani. Mimi nina uhakika hapo wataalamu wa UDSM hawana uwezo na hii ni baada ya kumsikia mmoja wao akitoa maelezo ya darasani! Wakati hawaj as piga kambi hapo na kufanya uchunguzi chini ya ardhi, inawezekana lile tetemeko limesababisha hilo.
Usijitoe ufahamu.Eti wataalamu wapige kambi kapige mwenyewe nyumba zinazama unataka na wataalamu wetu wazame hapo kwenye kambi?
Yaani wewe ulipoona kupiga kambi ukajua wanatakiwa wakajenge mahema waishi hapo!!??Eti wataalamu wapige kambi kapige mwenyewe nyumba zinazama unataka na wataalamu wetu wazame hapo kwenye kambi?
Kwani kupiga kambi maana yake nini wanakaa hewani au?Yaani wewe ulipoona kupiga kambi ukajua wanatakiwa wakajenge mahema waishi hapo!!??
Unanimalizaga Sana bwana PaskaliiHawa wasomi wa vitabuni, hakuna kitu!, kule Oldonyo Lengai, kabla ya ule moshi wa majivu, wanyama wote wa porini waakwisha timka, wakabaki ngombe na mbuzi!, hao ma geologist, walikuwa wapi?.
Unakumbuka issue ya Tetemeko la Bukoba,
Taarifa Rasmi ya Tetemeko la Ardhi Tanzania Kwenye Web ya Geological Survey of Tanzania! .
Wanabodi, Update. Hatimaye leo 12/09/2016, siku tatu baada ya kutokea tetemeko la Bukoba, GST nao ndio wametoa taarifa rasmi!.- Taarifa kwa Umma ya Tukio la Tetetemeko la Ardhi Mkoa wa Kagera WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA YA TUKIO LA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA 1 Tukio...www.jamiiforums.com PSomo Kutoka Tetemeko la Bukoba: Japo Halitabiriki na Halizuiliki Lakini Linalocetika!. Tujiandae!.
Wanabodi, Utangulizi Kwanza niungane na Watanzania wenzangu kutoa pole kwa Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko hili, kuwatakia uponaji wa haraka wa majeruhi na kuunganisha nguvu zetu kama taifa kuwasaidia kwa hali na mali wahanga wa tukio hilo ambapo kesho asubuhi, naamini...www.jamiiforums.com
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!
Wahamie wapi?Leo mkuu wa mkoa tyr ametoa maelekezo kuwa wananchi wa maeneo hayo wanatakiwa kuhama haraka
Hawajamtaja Halima Mdee kwenye Hilo sakata?Lipo kwenye taarifa za habari, magazeti yetu yamejikita kwenye siasa hili yanaona halina dili.
Ndiyo ,mliwapola waathilika michango yao iliyotolewa na mataifafa ,mashirika na watu wenyeupendo waliojitolea kuwasaidia.Hawa wasomi wa vitabuni, hakuna kitu!, kule Oldonyo Lengai, kabla ya ule moshi wa majivu, wanyama wote wa porini waakwisha timka, wakabaki ngombe na mbuzi!, hao ma geologist, walikuwa wapi?.
Unakumbuka issue ya Tetemeko la Bukoba,
Taarifa Rasmi ya Tetemeko la Ardhi Tanzania Kwenye Web ya Geological Survey of Tanzania! .
Wanabodi, Update. Hatimaye leo 12/09/2016, siku tatu baada ya kutokea tetemeko la Bukoba, GST nao ndio wametoa taarifa rasmi!.- Taarifa kwa Umma ya Tukio la Tetetemeko la Ardhi Mkoa wa Kagera WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA YA TUKIO LA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA 1 Tukio...www.jamiiforums.com PSomo Kutoka Tetemeko la Bukoba: Japo Halitabiriki na Halizuiliki Lakini Linalocetika!. Tujiandae!.
Wanabodi, Utangulizi Kwanza niungane na Watanzania wenzangu kutoa pole kwa Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko hili, kuwatakia uponaji wa haraka wa majeruhi na kuunganisha nguvu zetu kama taifa kuwasaidia kwa hali na mali wahanga wa tukio hilo ambapo kesho asubuhi, naamini...www.jamiiforums.com
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!
Mkuu P nahisi awamu hii msukuma mwenzio lazima akupe teuzi ,nakuomba unikumbuke kwenye ufalme wako wakati utakapokua unakula keki ya TaifaDuuh! kumbe wewe somo la Jiogirafia limekupita pembeni, ukanda wa Pwani tangu lini ukawa na volkano?, Volcano ni uji wa mawe unaitwa magma ni ya moto na hutanguliwa na moshi wenye jivu jeupe kama vumbi, magma hiyo hutoka chini na moto wake ikifika ardhini hutiririka na kupoa na ndio hujenga milima ya volcano, kama Mt. Kilimanjoro, Mt. Meru na Oldonyo Lengai, kuna aina tatu za volcano, hai, pozo na mfu. Kilimanjaro ni mfu, Meru ni pozo na Oldonyo Lengai ndio hai. Mfu hailipuki tena, imekufa, pozo, imetulia siku ya siku ikifika, itacharuka, haini kule chini magma ya moto inaendelea kuchemka ila haijalipuka.
Hilo tope baridi sio la volcano, hilo ni la mitetemo tuu, kutokana vi tetemeko vya chini kwa chini!, japo mimi sio mjeolojia, lakini najua kwa kuliona tuu kwa macho, eneo hilo ni eneo la mkondo wa maji, tope hilo ni udongo wa mfinyanyanzi, ulio chini ya mkondo huo wa maji, ambao chini yake una mwamba uliokuwa semi permeable rocks, ambao siku zote unapitisha maji kwenda chini ardhini kwenye mkondo wa maji, sasa kutokana na mvua, water table ime raise, above ile semi permeable rock, hivyo kina cha maji huko chini ardhini kimepanda, sasa na kutoka juu kama chemchem, kutoka na mfinyanzi huo huko jini kuloa, umekuwa uji, hivyo sasa uji wa tope la chemchem, ndio linakuwa pushed juu na ile water table.
Water table ikija kushuka, yale maeneo ya ulipotoka huo mfinyanzi, kutakuwa na hollow pots, mvua ikinyesha na kupalowewesha udongo wa juu, utaporomoka, kama kuna nyumba zinapiga ufa hadi msingi!.
Nimeyajua haya kutokana na mimi kibanda changu pia nimejenga juu ya mkondo wa maji na chinikuna udongo wa mfinyanzi, fundi aliyenijengea, alishauri nijenge msingi wa jamvi la nondo kama msingi wa ghorofa, mimi nikamgomea, si unajua tena Wasukuma tulivyo wabishi, nikamwambia fundi, sijawahi kuona jamvi la nondo nyumba ambayo sio ya gharofa, nikalazimisha ajenga tuu, kikawaida. Fundi akajenga kwa shingo upande!. Nikahamia, mwaka uliofuta mvua za elninyo zikashuka!, kumbe kwangu ni water way, upande wa nyuma kwa jirani yangu, maji yamefika hadi dirishani, akaniomba nibomoe ukuta wangu ili kuyaruhusu yapite.
Kwa ubishi ule ule wa Kisukuma, nikamgomea, kuwa kila mtu kauziwa kiwanja kivyake, hivyo kila mtu atafute pa kuyapeleka maji yake!.
Within two days, maji ukuta jirani yamefika juu ya dirisha, kwa jirani wamehama kila kitu kimeloa, huku yamezuiwa na ukuta wangu!, Kumbe chini kunazidi kulowa na after two days, huku kwangu kukaibuka chemchemi ya matope pembeni ya ukuta wote, yale maji ya jirani yanazama jini ya ukuta na kuibukia kwangu.
Nikamuita fundi wangu, akasema lazima tubomoe ukuta kuyapa maji ya jirani njia, nikamgomea, ndipo akaniambia kutatokea mambo mawili.
1. Ukuta utaloa, utazidiwa nguvu, maji yatafunja huo ukuta, na kutoka na presha, ukuta ukianguka utabomoa nyuma na presha ya maji nyuma yangu itazolewa!.
2. Kwa sababu chini ni mfinyanzi, una very high water retaining capacity, utakuwa tepetepe, na nilijenga msingi bila nondo, nyumba itaanza kutitia na kupiga nyufa kwenye msingi, mwisho itabomoka!.
Ndipo nikakubali, tukabomoa ukuta wangu kujenga tundu la kupitishia hayo hayo maji, kiukweli hiyo pressure, ili fumua karibu ukuta wote, ule msala wa maji sasa ndio yakajaa kwangu, ikabidi na ukuta wa mbele kutoboa kuyaachia maji njia yake, yalikata hadi barabara!.
After two years nyumba ilipiga bonge la crack kwenye msingi, fundi akanionyesga, kweli nyumba ilikuwa inatitia!. Hivyo nikakubali matokeo!,
P
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!
Kwa utaalam gani ulio nao juu ya miamba? Nani kakudanganya kuwa hiyo m dalili ya volkeno?Nimekagua eneo la tukio bwashee!
We nawe, ndio wale wale, jangwani ni mahali pakame hakuna mvua, nimejenga kwenye mkondo wa maji, ni njia ya maji ya iliyopo chini ya ardhi. Hizi njia ni kama mito, sometimes mito huwa inahama, na kuibukia pengine sometimes inapotea njia na kusambaa.Mbwembwe zote kumbe umejenga jangwani??
Jangwa la wapi bwashee?Mbwembwe zote kumbe umejenga jangwani??
Kuna mtaalam mmoja wa jiolojia yuko serikali alipigia simu na ITV habar akasema hilo tope halina shida watu waendelee na shughuli zao, sasa Leo nasikia mkuu wa mkoa kaagiza watu wahamishwe, mbona wanajichanganyaKuwahamisha waliopo kwenye mkondo huo si suluhisho wakati haujui nini kinaendelea chini ya ardhi eneo hilo, ni sawa na kikitoboa kipele cha jipu ukadhani umepata suluhisho kumbe jipu linakua kwa ndani. Mimi nina uhakika hapo wataalamu wa UDSM hawana uwezo na hii ni baada ya kumsikia mmoja wao akitoa maelezo ya darasani! Wakati hawaj as piga kambi hapo na kufanya uchunguzi chini ya ardhi, inawezekana lile tetemeko limesababisha hilo.
ni kweli hii inshu inawahusu kikosi cha zima moto na uokoaji.Tanzania kipo kikosi rasmi cha uokoaji ambacho kinatakiwa kusimamia majanga yanayotokea, tangu kuzuke tope linalotoka aridhini jeshi la polisi limekuwa mbele kutoa maelezo! Hilo jukumu ni la wataalamu wa jiolojia na kikosi cha uokoaji kusimamia usalama wa raia, hapa hakuna uhalifu. Sakata hilo ni kuwa na linahitaji hatua za haraka sana kujua nini kinaendelea chini ya ardhi eneo hilo badala ya kufanya siasa, baadhi ya nyumba zimezama na nyingine zinabomoka. Wataalamu wanaonekana kutoa maelezo ya nadhalia badala ya kupiga kambi eneo hilo na kufanya uchunguzi wa kina.