Duuh! kumbe wewe somo la Jiogirafia limekupita pembeni, ukanda wa Pwani tangu lini ukawa na volkano?, Volcano ni uji wa mawe unaitwa magma ni ya moto na hutanguliwa na moshi wenye jivu jeupe kama vumbi, magma hiyo hutoka chini na moto wake ikifika ardhini hutiririka na kupoa na ndio hujenga milima ya volcano, kama Mt. Kilimanjoro, Mt. Meru na Oldonyo Lengai, kuna aina tatu za volcano, hai, pozo na mfu. Kilimanjaro ni mfu, Meru ni pozo na Oldonyo Lengai ndio hai. Mfu hailipuki tena, imekufa, pozo, imetulia siku ya siku ikifika, itacharuka, haini kule chini magma ya moto inaendelea kuchemka ila haijalipuka.
Hilo tope baridi sio la volcano, hilo ni la mitetemo tuu, kutokana vi tetemeko vya chini kwa chini!, japo mimi sio mjeolojia, lakini najua kwa kuliona tuu kwa macho, eneo hilo ni eneo la mkondo wa maji, tope hilo ni udongo wa mfinyanyanzi, ulio chini ya mkondo huo wa maji, ambao chini yake una mwamba uliokuwa semi permeable rocks, ambao siku zote unapitisha maji kwenda chini ardhini kwenye mkondo wa maji, sasa kutokana na mvua, water table ime raise, above ile semi permeable rock, hivyo kina cha maji huko chini ardhini kimepanda, sasa na kutoka juu kama chemchem, kutoka na mfinyanzi huo huko jini kuloa, umekuwa uji, hivyo sasa uji wa tope la chemchem, ndio linakuwa pushed juu na ile water table.
Water table ikija kushuka, yale maeneo ya ulipotoka huo mfinyanzi, kutakuwa na hollow pots, mvua ikinyesha na kupalowewesha udongo wa juu, utaporomoka, kama kuna nyumba zinapiga ufa hadi msingi!.
Nimeyajua haya kutokana na mimi kibanda changu pia nimejenga juu ya mkondo wa maji na chinikuna udongo wa mfinyanzi, fundi aliyenijengea, alishauri nijenge msingi wa jamvi la nondo kama msingi wa ghorofa, mimi nikamgomea, si unajua tena Wasukuma tulivyo wabishi, nikamwambia fundi, sijawahi kuona jamvi la nondo nyumba ambayo sio ya gharofa, nikalazimisha ajenga tuu, kikawaida. Fundi akajenga kwa shingo upande!. Nikahamia, mwaka uliofuta mvua za elninyo zikashuka!, kumbe kwangu ni water way, upande wa nyuma kwa jirani yangu, maji yamefika hadi dirishani, akaniomba nibomoe ukuta wangu ili kuyaruhusu yapite.
Kwa ubishi ule ule wa Kisukuma, nikamgomea, kuwa kila mtu kauziwa kiwanja kivyake, hivyo kila mtu atafute pa kuyapeleka maji yake!.
Within two days, maji ukuta jirani yamefika juu ya dirisha, kwa jirani wamehama kila kitu kimeloa, huku yamezuiwa na ukuta wangu!, Kumbe chini kunazidi kulowa na after two days, huku kwangu kukaibuka chemchemi ya matope pembeni ya ukuta wote, yale maji ya jirani yanazama jini ya ukuta na kuibukia kwangu.
Nikamuita fundi wangu, akasema lazima tubomoe ukuta kuyapa maji ya jirani njia, nikamgomea, ndipo akaniambia kutatokea mambo mawili.
1. Ukuta utaloa, utazidiwa nguvu, maji yatafunja huo ukuta, na kutoka na presha, ukuta ukianguka utabomoa nyuma na presha ya maji nyuma yangu itazolewa!.
2. Kwa sababu chini ni mfinyanzi, una very high water retaining capacity, utakuwa tepetepe, na nilijenga msingi bila nondo, nyumba itaanza kutitia na kupiga nyufa kwenye msingi, mwisho itabomoka!.
Ndipo nikakubali, tukabomoa ukuta wangu kujenga tundu la kupitishia hayo hayo maji, kiukweli hiyo pressure, ili fumua karibu ukuta wote, ule msala wa maji sasa ndio yakajaa kwangu, ikabidi na ukuta wa mbele kutoboa kuyaachia maji njia yake, yalikata hadi barabara!.
After two years nyumba ilipiga bonge la crack kwenye msingi, fundi akanionyesga, kweli nyumba ilikuwa inatitia!. Hivyo nikakubali matokeo!,
P
Pasco Mayalla Ndiye Mwana JF wa Kwanza, Kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM!