Dar: Washindwa kula nyama krisimasi bei imepanda Kg Sh 11000. Chalamila hajaliona hili?

Dar: Washindwa kula nyama krisimasi bei imepanda Kg Sh 11000. Chalamila hajaliona hili?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813

Nilikuja hapa kununua nyama leo sikukuu watoto wakale lakini nimekuta bei zimebadilika hadi elfu 11 kwa kilo, naomba serikali itusaidie udhibiti wa bei ambazo zinapanda mara kwa mara.”- Dickson Kitanda, Mkazi wa Mwananyamala
 
Nyama ni 10k maeneo mengi, kama ongezeko la buku limefanya wasile nyama bas hawapo serious na sherehe, btw, bei itashuka after sikukuu
 
Watu wa Dar walalamishi sana ka yatima,mimi huku liwale nanunua nyama kilo 1 sh 10,000 Napo hadi niifate kwa nauli ya sh 10,000 kwenda na kurudi,na wala silalamiki,wewe wa 11,000 kelele mingi!!

Watu wa Dar bure kabisa
 
Poleni Sana ,watu wadaslama hapo nikula mchicha , unajua ongezeko la buku moja ni kubwa Sana ikiwa unakula nyama Sana.
 
Watu wa Dar walalamishi sana ka yatima,mimi huku liwale nanunua nyama kilo 1 sh 10,000 Napo hadi niifate kwa nauli ya sh 10,000 kwenda na kurudi,na wala silalamiki,wewe wa 11,000 kelele mingi!!

Watu wa Dar bure kabisa
Hili nalo wakalitazame.
 
Ongezeko la 1000 ndo lifanye mtu ale matembele sikukuu!?, January ada za watoto na ela za school bus zitaongezeka, mjiandae kisaikolojia.
 
20231225_172309.jpg
 
Hao wanaolalamika ni chadema,mbona sisi Wana CCM tunanunua kwa bei ndogo sana
 
View attachment 2852661
Nilikuja hapa kununua nyama leo sikukuu watoto wakale lakini nimekuta bei zimebadilika hadi elfu 11 kwa kilo, naomba serikali itusaidie udhibiti wa bei ambazo zinapanda mara kwa mara.”- Dickson Kitanda, Mkazi wa Mwananyamala
Pole mkuu; lakini ndo sikukuu inapita hivyo. Wewe ungependekeza nyama iuzwe Kg. 1 kwa Tshs ngapi?? Katika pendekezo lako zingatia yafuatayo:
1. Nauli ya Usafirishaji wa mnyama(ng'ombe au Mbuzi) kutoka huku mikoani hadi Dar.
2.Vijana waswagaji mifugo kutoka maporini huko hadi mahali pa kupakia (Rump)
3. Tajiri Mnunuzi wa ng'ombe au mbuzi anahitaji kupata chochote a.k.a faida
4. Bucha(Fremu ya kuuzia) inalipiwa (kodi ya pango)
5. Kila kg.moja unayouza unalipa Tozo Serikalini- ref mashine za EFD.
6. Zipo Risks njiani e.g. Ng'mbe anaweza kufa kwa kukanyagwa na wenzake au kukosa hewa au kuugua ghafla(tena broo;Bila kusahau wale jamaa wavaa kofia barabarani).
7.Usiwasahau Wachunaji na usafirishaji kutoka machinjioni hadi Buchani.
Karibu tujadili.
BTW:
Mimi sijihusishi na biashara ya nyama wala biashara ya mifugo minadani ila nafahamu madhila wanayopitia wenye biashara hiyo.
 
Watu wa Dar walalamishi sana ka yatima,mimi huku liwale nanunua nyama kilo 1 sh 10,000 Napo hadi niifate kwa nauli ya sh 10,000 kwenda na kurudi,na wala silalamiki,wewe wa 11,000 kelele mingi!!

Watu wa Dar bure kabisa
Wewe akili zako zimeshafubazwa na mahaba ya chama chako.
 
Back
Top Bottom