Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
WATUHUMIWA 14 WAKAMATWA KUSHAWISHI MAANDAMANO YASIYO HALALI.
Dar es Salaam- 03Novemba, 2020
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na oparesheni kali ya kukamata watu wanaofanya mipango ya kuhamasisha maandamano bila kufuata sheria na kusababisha taharuki kwa wananchi sambamba na mipango ya kuharibu mali, miundombinu na kudhuru watu.
Hadi sasa Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam linawashikilia watu 14 kama ifuatavyo;
1. Freeman Mbowe - Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
2. Bonface Jacob aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo na mwanachama wa Chadema
3. Denis Vesta
4. Godfrey Seleman
5. Elisha Mbandamka
6. Shehebu Kiarus
7. Yohana Marco
8. Salehe Omary
9. Mohamed Omary
10. Tundu Antipas Lissu, aliyekuwa mgombea urais na makamu mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
11. Moses Fanuel Omary
12. Charles Renatus
13. Essau Charles Bwiru
14. Godbless Lema aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini
Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiliwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serikali kwa hatua zaidi za kisheria.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es salaam amesema jiji la Dsm liko shwari na wanasiasa waache tabia ya kuja kufanya fujo maeneo ambayo sio majimbo yao na hatimaye wafuate sheria ili kupeleka malalamiko yao tume ya uchaguzi na si kushawishi watu kufanya maandamano haramu, kuhatarisha maisha ya watu na mali zao pia kuleta taharuki kwa wananchi wasio na hatia.
Aidha watuhumiwa wengine wanaotafutwa ni pamoja na Halima Mdee ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha CHADEMA pamoja na Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT wazalendo) aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini.
Pia Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linawataka wajisalimishe mara moja ili kuendelea na mahojiano kwa tuhuma zinazowakabili.
LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.