Uchaguzi 2020 Dar: Watu 14 Wakamatwa kwa kushawishi maandamano yasiyo halali

Uchaguzi 2020 Dar: Watu 14 Wakamatwa kwa kushawishi maandamano yasiyo halali

Kwahiyo halima na zito wamejificha au wamekimbia😁😁😁
 
We ndo mjinga,
Huyu anashangaa polisi kumuwekea bail mtuhumiwa mmoja tu kati ya wengi walokamatwa, we unamuona hajasoma we ndo mwehi.
Hata mie nastaajabu hao polisi kwa upendeleo/uoga
Kukosa kwako elimu ndio kuna kusumbua, hujui police bail ni kitu gani?. Mipumbavu ndio mnashabikia upuuzi.
 
WATUHUMIWA 14 WAKAMATWA KUSHAWISHI MAANDAMANO YASIYO HALALI.

Dar es Salaam- 03Novemba, 2020

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na oparesheni kali ya kukamata watu wanaofanya mipango ya kuhamasisha maandamano bila kufuata sheria na kusababisha taharuki kwa wananchi sambamba na mipango ya kuharibu mali, miundombinu na kudhuru watu.

Hadi sasa Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam linawashikilia watu 14 kama ifuatavyo;

1. Freeman Mbowe - Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

2. Bonface Jacob aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo na mwanachama wa Chadema

3. Denis Vesta

4. Godfrey Seleman

5. Elisha Mbandamka

6. Shehebu Kiarus

7. Yohana Marco

8. Salehe Omary

9. Mohamed Omary

10. Tundu Antipas Lissu, aliyekuwa mgombea urais na makamu mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

11. Moses Fanuel Omary

12. Charles Renatus

13. Essau Charles Bwiru

14. Godbless Lema aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini

Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiliwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es salaam amesema jiji la Dsm liko shwari na wanasiasa waache tabia ya kuja kufanya fujo maeneo ambayo sio majimbo yao na hatimaye wafuate sheria ili kupeleka malalamiko yao tume ya uchaguzi na si kushawishi watu kufanya maandamano haramu, kuhatarisha maisha ya watu na mali zao pia kuleta taharuki kwa wananchi wasio na hatia.

Aidha watuhumiwa wengine wanaotafutwa ni pamoja na Halima Mdee ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha CHADEMA pamoja na Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT wazalendo) aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini.

Pia Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linawataka wajisalimishe mara moja ili kuendelea na mahojiano kwa tuhuma zinazowakabili.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAM.
Ipo haja ya kuanza kuitumia ile njia waliyoitumia watu wa Lindi kuwakataa hawa wabunge wamagufuli
 
Act of hooliganism by the head of state. You steal votes, you change the election results, then you turn everything (wrong doing) to the opposition that they printed fake votes.

Unprecedent act of hooliganism which was done only by Hitler and happened in imperial japan in the last century; also qin dynasty when fraud was the order of the day.

All these hooligans used security forces to suppress opposition
Mhhh what a lecture from an academician,,, Hooligans!! hooligans using security forces mhh you better go back to school on hooliganism lessons,, Hitler was not a hooligan but a great leader and what about the Belgian King Leopold who killed more than 15 million Congolese more than twice of Hitler,s mess,, has your godfathers mentioned about???
 
Mbona wamewapa kesi nusu!?
Ikitakiwa iwe hivi"Kuhamasisha maandamano haram na kutaka kuchoma vituo vya mafuta"
 
Maandamano ni HAKI yetu ya KIKATIBA.
Mnashambuliana wenyewe na angalia kujichanganya kwenu,,mguu aliopigwa risasi Lissu ulitakiwa kuwa wa dereva,,,mguu wa kulia,, Lissu angepigwa mguu wa kushoto kama alikuwa anaendeshwa akiwa amekaa mbele na dereva wake,, je umeuona mlango wa gari uliopigwa risasi?? kajiridhishe gari bado liko polisi
 
Kisa Chadema imekosa wabunge na imekufa kifo cha mende?
Kuua CHADEMA kifo cha mende, haitoshi kukupa amani, otherwise usingeendelea kubwabwaja hapa! Unashindanaje na CHADEMA iliyokufa kifo cha mende, kama hampo sehemu moja, (huko kifoni kwa mende)????!!!
 
Freeman Al Baghdad Mbowe, mzee wa bendera nyeusi, maandishi meupe na majambia mawili😀
 
Hata Nyerere aliwahi shitakiwa na wakoloni kwa kuandamana.

Mandela pia aliitwa gaidi.
Nyerere ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa mminya haki za binadamu.
Nenda field, maandamano ya kwenye simu yana matokeo madogo sana kamanda salary
 
So sad kwa kinachofanywa na hili jeshi dhalimu!
Halafu kuna mtu ataniambia niwe mzalendo,aah wapi!Akija adui na lengo likawa nikuwatarget hawa wadhalimu,walahi nawaunga mkono!
Nawashauri watz waanze sasa kukutarget na wewe wasisubiri mpaka adui aje TZ wewe ni adui wa watz kuanzia sasa hivi.
 
Act of hooliganism by the head of state. You steal votes, you change the election results, then you turn everything (wrong doing) to the opposition that they printed fake votes.

Unprecedent act of hooliganism which was done only by Hitler and happened in imperial japan in the last century; also qin dynasty when fraud was the order of the day.

All these hooligans used security forces to suppress opposition
Kama kwenye kifo cha Aquelina, waligeuziwa kibao wao.
Kwa TL napo walisema wamempiga risasi wanachama wenzake.
Yani ni mwendo wa kubadilishiana kibao tu.
 
Natamani agizo litoke ".....Harooo IGP, waagize vinaja wako kuelekea kuapishwa kwangu futeni kesi za kisiasa zote ,warudi makwao wamejifunza, ...napigiwa kelele sana mabalozi kupitia kwa Kabudi na wasaidizi wangu...." IGP sawa mkuu tunateleza mara moja..."
 
Back
Top Bottom