Uchaguzi 2020 Dar: Watu 14 Wakamatwa kwa kushawishi maandamano yasiyo halali

Uchaguzi 2020 Dar: Watu 14 Wakamatwa kwa kushawishi maandamano yasiyo halali

Atakupataje huku JF na ID yao bandia? Wanawatafuta vingunguri wanaoshinda mashimoni, porini & misituni wakila udongo na mchwa na kunywa umande. Wewe ambaye hata huo mkono wako lainiii unajeruhiwa na kiibodi yako hiyo hawakutaki kabisa hata kwa ushauri tu.
 
WATUHUMIWA 14 WAKAMATWA KUSHAWISHI MAANDAMANO YASIYO HALALI.

Dar es Salaam- 03Novemba, 2020

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na oparesheni kali ya kukamata watu wanaofanya mipango ya kuhamasisha maandamano bila kufuata sheria na kusababisha taharuki kwa wananchi sambamba na mipango ya kuharibu mali, miundombinu na kudhuru watu.

Hadi sasa Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam linawashikilia watu 14 kama ifuatavyo;

1. Freeman Mbowe - Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

2. Bonface Jacob aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo na mwanachama wa Chadema

3. Denis Vesta

4. Godfrey Seleman

5. Elisha Mbandamka

6. Shehebu Kiarus

7. Yohana Marco

8. Salehe Omary

9. Mohamed Omary

10. Tundu Antipas Lissu, aliyekuwa mgombea urais na makamu mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

11. Moses Fanuel Omary

12. Charles Renatus

13. Essau Charles Bwiru

14. Godbless Lema aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini

Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiliwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es salaam amesema jiji la Dsm liko shwari na wanasiasa waache tabia ya kuja kufanya fujo maeneo ambayo sio majimbo yao na hatimaye wafuate sheria ili kupeleka malalamiko yao tume ya uchaguzi na si kushawishi watu kufanya maandamano haramu, kuhatarisha maisha ya watu na mali zao pia kuleta taharuki kwa wananchi wasio na hatia.

Aidha watuhumiwa wengine wanaotafutwa ni pamoja na Halima Mdee ambaye alikuwa mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha CHADEMA pamoja na Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT wazalendo) aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini.

Pia Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linawataka wajisalimishe mara moja ili kuendelea na mahojiano kwa tuhuma zinazowakabili.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAM.
Wakuu,
Nchi yetu inapoenda ni pabaya. Polisi kuwemo ndani ya siasa sio mwelekeo mzuri.
Kama ni kuonyesha umahiri wa kiintelijensia, nguvu ya polisi, na hata kuhakikishia usalama wa raia, basi wangeanza huko kusini kwenye magaidi wa kweli. Sijasikia polisi wakija kusema oh kuna taarifa ya magaidi wanataka kuua watanzania, tumewakamata walikuwa wanafanya mikutano huko kusini.
Najiuliza maswali mengi

Waziri wa Kiraia, tunapelekwa kipolisi polisi?
Kwani mandamano ni uhalifu? kwanini iwemo kwenye sheria za nchi? Kwanini isiwe tu Maandamo kushnei?
Watoe evidence, waende kwa nani yule aarrrgh enhe musiba, inawezekana akatusaidia kuonyesha huo uhalifu wa hao viongozi wa kisiasa

...zaidi ya hapo atakuja kuelewa kuwa ile nembo anayovaa inasema usalama wa raia. na sio chama.
nimejaa jazba
 
Back
Top Bottom