Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 11,786
- 18,562
Unamfahamu?Huyo marehemu alikuwa maharage ya Mbeya sana, hao vijana wa kiume wasamehewe na kuachiwa mara moja.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unamfahamu?Huyo marehemu alikuwa maharage ya Mbeya sana, hao vijana wa kiume wasamehewe na kuachiwa mara moja.
Utaambiwa Ukosefu wa ajira ni tatizo la dunia nzima.Kweli katiba mpya ni muhimu ili ije na suluhisho la ajira kwa vijana, yani mil 1.7 saba unalipwa kuua mtu!!!? Jamani huyo ni mtu au mbwa kuchaa?
Wanaume, ni rahisi sana kutambua kuwa mwanamke ulienae hakupendi ila pesa yako kwanini umgharimikie? Nyie wanawake wenye tamaa za fisi kama humpendi mtu kwanini umkubalie? Siukatae tu ili uwe huru na maisha yako?
Hapana sheria ichukue mkondo wake. Angeachwa aendelee kuishi pengine angeweza kubadili mwenendo wa maisha yake.Huyo marehemu alikuwa maharage ya Mbeya sana, hao vijana wa kiume wasamehewe na kuachiwa mara moja.
Naona Kama ni ukichaa 1.7 mil. Uue mtu kweli ?Dunia imekwisha
Naona Kama ni ukichaa 1.7 mil. Uue mtu kweli ?
huyu mdada kumbe ndo tabia zake. Kisa mnene mweupe ndo akafanya watu madanga yake. Duh!! yani huku amepata kibano na huko kwa Mungu anakwenda kupambana na kibano kingine. Au kwa kibano walichompa huku Mungu atamsamehe?Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aitwaye Barke Rashid, aliyeuawa Januari Mosi, 2022, akiwa guest maeneo ya Tabata, ambapo mmoja amekiri kutekeleza unyama huo baada ya kuahidiwa shilingi milioni 1.7
Kuhusu mkasa wa mauaji, soma Dada zetu kuweni makini na madanga mnayopata sehemu za starehe
----
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata watu wawili wanaodaiwa kula njama ya kumuua mwanamke mmoja katika nyumba ya kulala wageni eneo la Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Barke Rashid (30) ameuawa Januari Mosi, 2022 baada ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake White kutoa malipo ya Sh1.7 milioni kwa Jonsiner Bounser ili kutekeleza mauaji.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo leo Jumanne Januari 25, 2022 imeeleza kuwa chanzo cha maauaji hayo ni mwanamke huyo kukabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya wageni.
“Inadaiwa mtuhumiwa wa kwanza alikodiwa na mtuhumiwa wa pili kwa malipo ya Sh1.7 milioni ili amtongoze na baadae aende kumuua mwanamke huyo kwa madai kuwa mtuhumiwa wa pili alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini ilidaiwa na mtuhumiwa wa pili kuwa mwanamke huyo ana wanaume wengine.
“Mtuhumiwa wa kwanza amekiri kupewa Sh1.2 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Sh500,000 kwa mtuhumiwa wa pili kwa mauaji ya mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo” imeeleza taarifa hiyo.
Habari zaidi...
=====
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Dar-es-salaam 25/01/2022
WATUHUMIWA WAWILI WAMEKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MWANAMKE MMOJA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata na kuwashikilia watu wawiwli wanaodaiwa kula njama na baadae kumuua mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid miaka 30 Mdigo mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam.
Tukio hilo limetokea tarehe 1.1.2022 huko eneo la tabata segerea kwenye Nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo mtuhumiwa wa kwanza jinsia Me @jonsiner bounser miaka 34, Mmakonde mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa mwenye jinsia Me White miaka 33 Mhehe mfanya biashara ya Lori la kuzolea taka mkazi wa Tabata Segerea.
Chanzo cha maauaji hayo ni Mwanamke huyo kukabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika Nyumba hiyo ya kulala wageni na inadaiwa na mtuhumiwa wa kwanza alikodiwa na mtuhumiwa wa pili @Whyite kwa malipo ya Tshs milioni moja na laki saba ili amtongoze na baadae aende kumuua mwana mke huyo kwa madai kuwa mtuhumiwa wa pili alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini ilidaiwa na mtuhumiwa wa pili kuwa mwanamke huyo ana wanaume wengine.
Mtuhumiwa wa kwanza amekiri kupewa Tshs milioni moja na laki mbili kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Tshs laki tano kwa mtuhumiwa wa pili kwa mauaji ya mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo
Tukio la pili linahusu kukamatwa kwa watu sita wote wanaodaiwa kuiba vitabu mbalimbali mali ya Taasisi ya Elimu Tanzania. Tukio hili limetokea tarehe 23.1.2022 saa saba mchana eneo la Mabibo External wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam.
Vitabu hivyo vilikuwa kwenye viroba 19 na tayari vilikwishapakiwa kwenye Magari yenye namba za usajili T 718 DXW aina ya Pro Box na T 931 DNG aina ya Noah, watuhumiwa hawa wanahojiwa kwa kina na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar essalaam linaendelea kuwashukuru Wananchi wema wanaoendelea kutoa taarifa za kweli zinazosaidia kufuatilia na kuwakamata wahalifu kabla au baada ya uhalifu.
Muliro J. Muliro– ACP
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam
We umelewa leo au mbona unachangia kiwaki sanaKama kaleta mambo ya kingese ufanyaje sasa? Unapangia mwanamke nyumba na kumpa kila kitu still analeta upuuzi😅?
Kwa hali ya sasa mie hata wakinipa 1M nakuondoa kichwa chapuNaona Kama ni ukichaa 1.7 mil. Uue mtu kweli ?
[emoji1787][emoji1787] nyie ndio mnafanya kazi yakuondoa watu ionekane kazi rahisi SanaKwa hali ya sasa mie hata wakinipa 1M nakuondoa kichwa chapu
Kitaa kigumu aisee[emoji1787][emoji1787] nyie ndio mnafanya kazi yakuondoa watu ionekane kazi rahisi Sana
wewe umeumbwa na nani?Alipangiwa kufa hivyo na nani?
Nimeumbwa na Munguwewe umeumbwa na nani?
Ile roho ya uuaji iliyoletwa na boss wa wasiojulikana still inatenda Kazi.Dunia imekwisha
Ujinga kuua mtu kisa mapenzi.Usaliti ktk mapenzi ni chanzo kikuu cha mauaji.
badilikeni .
Ngoja nkuelimishe kidogo mimi mwenyewe ni muuguzi unatolewaje figo bla kuacha alama kwenye mwili? Na ndugu walipewa ruhusa ya kukagua mwlMsitufanye wajinga, hapo kilichokuwa kinalengwa ni hiyo FIGO tu. Hayo mengine ni porojo za kusherehesha hadithi tu. Nilisema toka mwanzo, kwamba Figo ukiitoa bila utaalam ni useless, hivyo lazima surgeon mtaalam alikuwepo kuitoa kitalaam, which haiwezekani kwa guest house, hivyo baada ya mauaji na huo mwili kupelekwa mortuary, huko ndiko walipoitoa kitaalam.