WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Dar es Salaam kuaga miili ya waliofariki kutokana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la Ghorofa eneo la mtaa wa Congo na Mchikichi kata ya Agrey Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam lililoanguka tarehe 16 Novemba, 2023.
Tukio la ibada maalum ya kuwaombea na kuaga miili ya marehemu hao limefanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja Dar es Salaam.