Dar: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Shaban Mkwanywe kwasababu ya uzembe kazini

Dar: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Shaban Mkwanywe kwasababu ya uzembe kazini

Na kwa taarifa tu, ndg Waziri huyo meneja inaonekana amekula sana pesa za madawa ya kusafisha maji.

Rafiki yangu mmoja jana kanisimukia mkasa wa kwenda kazini huko Dar bila kuoga, kisa maji yanafanana na chai ya maziwa kwa takribani week nzima ''anasema"

Inakuwaje matanki yanayopokea maji yasiwekewe dawa au kuchuja maji kabla ya kuwafikia wateja?.

Kwani mapato mnayokusanya kwa wateja pamoja na bajeti mnayopewa na serikali haitumiki ipasavyo?.
 
Mamlaka ya uteuzi ilikosea sana kumtoa Eng. Luhemeja hapo Dawasa alifanya kazi kubwa sana, hizi changamoto ni matokeo ya kumtoa
 
NIMESHANGAA sana kuwa makao makuu ya Dawasa yapo ubungo halafu wilaya ya ubungo ndiyo wilaya pekee mkoa wa Dar es salaam ambao haijaungwa na huduma ya maji.Huko misumi,mpiji, mbezi msakuzi ,makabe n.k hakuna hata bomba Moja la Dawasa.Halafu Kuna wapuuzi wanasema mama anaupiga mwingi.wananchi wa wilaya ya ubungo kunyweshwa maji ya mabowser ya magari yaliyochotwa mtoni ndiyo kuupiga mwingi?
Jiulize hao watendaji wa dawasa qameshindwa kuwafikishia watu maji kwa ajili ya mama hakuwatimizia mahitaji yao au ni uzembe wao wenyewe?
 
AWESO AIPANGUA DAWASA, AIWEKA CHINI YA UANGALIZI MAALUM

View attachment 3030087
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiula Kingu akae pembeni kwa muda, pia amemsimamisha kazi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji-DAWASA, Shaban Mkwanywe na kuanzia leo June 30,2024 ameiweka DAWASA chini ya uangalizi Wizara ili kuboresha utendaji wake kufuatia uzembe uliopelekea visima kukosa maji na kufanya Wakazi wa Dar es salaam kukosa maji.

Aweso ametangaza uamuzi huo leo baada ya kufanya ziara ya kimkakati na ya kushtukiza katika Ofisi za DAWASA zilizopo Ubungo Dar es salaam ili kupata maelezo ya Watendaji ya sababu za Watu kukosa maji na baada ya kushindwa kuridhishwa na majibu aliamua kuzungukia matanki ya maji katika maeneo manne tofauti ikiwemo la Ardhi UDSM na Kibamba huku akituma Timu nyingine kwenda kukagua matanki ya Kigamboni ambapo matanki hayana maji huku mengine yakiwa na maji kidogo ukilinganisha na mahitaji ya Wananchi huku Watendaji wa DAWASA wakishindwa kueleza sababu iliyopelekea uhaba huo wa maji.

Aweso amesema “Mwanzoni kulipokuwa kunakosekana maji tulikuwa tunasema shida ni vyanzo vya maji vimekauka hakuna maji, TANESCO umeme hamna lakini leo vyanzo vyote vina maji, umeme upo, niambieni kwanini hatuna maji kwenye matenki?, kwanini Wananchi wanateseka, wanalalamika wanapiga kelele kwenye Serikali?”

Ziara ya Aweso leo imekuja baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa Maji aliyoifanya kwa siku mbili kujionea utendaji kazi wa DAWASA na hali ya upatikanaji wa maji ambapo amebaini uzembe aliouwasilisha kwa Waziri Aweso leo ikiwemo miundombinu ya maji kuwa chakavu, maji kupotea bila usimamizi, Watendaji wa DAWASA wa ngazi za chini kutopewa stahiki zao muhimu na kupelekea kufanya kazi bila hamasa nzuri na hata kupelekea kuwajibu vibaya Wateja, ziara hiyo ya Aweso na Katibu Mkuu itaendelea katika maeneo mbalimbali ya Nchi ili kuboresha upatikanaji wa maji.

Pia soma;

1. KERO - Wakazi wa Tegeta Azania (Kwenye Nyaya za Umeme wa Zanzibar) hatuna Maji kwa Muda Sasa, DAWASA shida ni nini?

2. KERO - DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

3. KERO - DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani

4. KERO - Waziri Juma Aweso atoke hadharani na kusema kwanini Ubungo mpaka Kimara maji ni shida

5. KERO - Waziri Aweso, Jiji la Dar Sasa wanakunywa na kuoga maji ya kwenye mifereji. DAWASA pakavu

6. KERO - Kinyerezi kuna shida kubwa ya maji, group la DAWASA WhatsApp halifanyi chochote kutatua kero hii

7. KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

8. DAWASA kwanini mvua ni nyingi lakini tunakosa maji?

9. KERO - DAWASA kuna rushwa kwenye ufungaji wa maji

10. KERO - DAWASA maji ya makazi mapya Mbezi Beach yana udongo mwezi sasa, nini shida?

11. KERO - Maji ya DAWASA yana harufu na ladha ya Dawa kali sana, ni salama kweli?

12. Mnyika: DAWASA mnataka tufanye maandamano ya Maji DSM ndio mtoe majibu?

13. Hivi DAWASA haina msimamiz?

14. Dar: Maeneo ya Segerea hadi Kinyerezi hakuna Maji

15. DOKEZO - Tabata Bonyokwa hatujaona tone la maji wiki ya tano sasa, DAWASA mnatuona manyani?

16. DOKEZO - DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!

17. ACT Wazalendo: Kutofanyiwa kazi matatizo ya upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam; Tunamtaka Waziri wa Maji kuiwajibisha DAWASA
Hii inakaaje kobaaz kumsimamisha Kobaaz mwenzake ndugu yake katika imani?

adriz hydroxo Adiosamigo Webabu incharge Jagina green rajab
 
MWANGALIENI USON ANASUTWA. HUYU WAZIR NI MWIZI NA MSANII NA TAPELI. KUNA MREJESHO ALIUTAKA HUKU DAWAS HAKUPEWA NDIO MAANA ANAJIDAI KUSHUGHULIKIA WATENDAJI
Nakuunga mkono, yeye ndiye mwenye shida anakaa ofisini watu wamepiga kelele. Kuna watu miezi 6 hawana maji. Aliziba masikio, akawa chura kiziwi mdogo. Hiyo wizara imemshinda.
 
Hii inakaaje kobaaz kumsimamisha Kobaaz mwenzake ndugu yake katika imani?

adriz hydroxo Adiosamigo Webabu incharge Jagina green rajab
Hahaha inahusika nini wakiwa wana majina ya kislamu, mimi mbona Magu nilikuwa nampenda kuliko maraisi wote wa Tanzania, lakini alikuwa anawasumbua sana marafiki zangu, na hao marafiki zangu walikuwa wananichukia mimi eti namsifia dictator.

Haya Makondo mzee wa kazi namsifia na yeye ni Mkristo, we akili zako unadhani mimi nachukia wakristo, mbona wengi tu tulikuwa tunasoma nao mpaa leo ni marafiki zangu, wengine mpaa tulikuwa tunakula nao ugali majumbani kwao.

Mimi wananijua wazi sina matatizo nao, lakini sikubaliani nao kifrika na vitabu vyaa kuhusu Yesu, wao wanasema Yesu ni Mungu au Mtoto wa Mungu hapo ndio tunapishana.

Kuhusu hio issue ya maji hata awe ndugu yangu wa tumbo moja, akiwa kakosa ni lazima nimkosoe tu.

Wangemrudisha Luhemeja alifanya kazi nzuri, kwani ukiwa mkristo au muislam ndio nini.

Mchapa kazi haendi na dini anaenda na mawazo yake.

Kuna lingine.
 
Hahaha noted mkuu
 
Jamaa anaonekana ana kiburi alikuwa anatafuna Jojo Waziri akiongea naye.
 
Ungewafukukuza mbali kabisa na utumishi wa.umma. dsm ndio jiji linaloongiza kwa mapato halafu maji hakuna.

Wahuni hawa wananufaika na wauza maji ya malori.
 
Hakuna Logic ya kumfuta kazi mkurugenzi suala la ukosefu wa maji nchi hii ni suala la kufeli Kwa serikali iliyopo madarakani, pamoja na waziri wake
Lini umesikia Marekani waziri wa maji amemfuta kazi Mkurugenzi, haya mambo ni hayo hayo mambo ya aweso anajua Mkurugenzi sio mtu wake na amemzidi mshahara hivyo anamtafutia zengwe Ili aweke mtu wake, kama alivyoweka Mkurugenzi wa muwasa Moshi asiye na vigezo taratibu za vyeo zinataka Mkurugenzi awe na masters ya mambo hayo ya maji na degree juu, ila tunaendelea kuvunia katiba . Tunajua hata huyo mtu wako utakayemuweka matatizo hayataisha, kwasababu haya ni matatizo ya serikali, hivyo uonevu ni kawaida ya wanasiasa.

Nchini hii Ina matatizo makubwa ya kiutawala yaliyochangiwa na umaskini wa nchi hii pia.
 
Kila nchi ina taratibu zake.

Marekani wana taratibu zao na Tanzania ina taratibu zake.

Kwa taratibu za Tanzania waziri wa maji ana nguvu ya kumfukuza mkurugenzi wa maji.. maana waziri wa maji ndio bosi wa watu wote wanaodili na maji.

Kama maji hayatoki na Mkurugenzi amezembea acha atimuliwe tu
 
Hakuna Logic ya kumfuta kazi mkurugenzi suala la ukosefu wa maji nchi hii ni suala la kufeli Kwa serikali iliyopo madarakani, pamoja na waziri wake
Lini umesikia Marekani waziri wa maji amemfuta kazi Mkurugenzi, haya mambo ni hayo hayo mambo ya aweso anajua Mkurugenzi sio mtu wake na amemzidi mshahara hivyo anamtafutia zengwe Ili aweke mtu wake, kama alivyoweka Mkurugenzi wa muwasa Moshi asiye na vigezo taratibu za vyeo zinataka Mkurugenzi awe na masters ya mambo hayo ya maji na degree juu, ila tunaendelea kuvunia katiba . Tunajua hata huyo mtu wako utakayemuweka matatizo hayataisha, kwasababu haya ni matatizo ya serikali, hivyo uonevu ni kawaida ya wanasiasa.

Nchini hii Ina matatizo makubwa ya kiutawala yaliyochangiwa na umaskini wa nchi hii pia.
Mods ungamisha huu Uzi.

Aweso fukuza hao vilaza
 
Back
Top Bottom