Dar: We’re committed to bulk buying of petroleum. Ruswa tupu!

Dar: We’re committed to bulk buying of petroleum. Ruswa tupu!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Serikali kujihusisha na biashara za mafuta ni nia ya viongozi kutafuta rushwa badala ya kujali wananchi. Serikali inashidwa kutatua tatizo la umeme la kununua Generator lakini badala yake inataka kujiingiza kwenye biashara za rushwa kwa kukataza na kuchagua ni nani alete mafuta Tanzania. Je ni lini viongozi wetu wataanza kujali watanzania badala ya matumbo yao, ni lini tutakuwa na viongozi wazalendo. Nani kasema kwamba tu kampuni zikijiunga zitaleta mafuta kwa bei rahisi wakati tanzania inatumia 0.0002% ya mafuta !!. Serikali ijitoe kwenye biashara na hao mawaziri hasa wa nishati hawajui biashara wala wanachofanya bali wanawasikiliza hao wanawapa rushwa wanavyowaambia. Mimi niko hapa Houston, TX kwenye kiini cha kampuni zote za biashara za mafuta duniani na nasema hii ni rushwa na si ukweli kwamba utapunguza bei kwa kuchagua kampuni moja kuleta mafuta!!!
 
Kamundu,

..mwanzo walisema TPDC ndiyo watapewa jukumu la kuagiza in bulk.

..baadaye wakaona watakosa ulaji kwa hiyo Ngeleja akatangaza kwamba itachaguliwa kampuni binafsi!!
 
Njeleja ni mlarushwa na mfisadi mkubwa sana na mbinafsi wa ajabu!!!. Tanesco serikali imeshidwa sasa wanajiingiza kwenye biashara za mafuta!!!. Kwanini wasiachie kampuni binafsi!!
 
Uagizaji mafuta kwa pamoja ni jambo muhimu na limnamafaa makubwa kwa taifa:
  1. Ukununua kitu kwa ujumla lazima uapate unafuu wa bei
  2. serikali itakuwa na takwimu sahii za mafuta yaloagizwa na itaweza kuzibiti ukepaji wa kodi
  3. utaratibu huu utachangia kupunguza uchakachuaji wa mafuta
Kwa hill Ngeleja anastahili pongezi mnyonge mnyongeni lakini haki yake apaewe.
 
Ninachofahamu ni kwamba bei ya juu ya mafuta inachangiwa na ushuru mkubwa na kodi ya mafuta ambayo TRA inatoza. Kwa mfano, Import duty ya Petrol kwa litre ni Shs 537. Hapo haujaweka VAT ambayo inapitishwa kwa mlaji pamoja na gharama za usafirishaji etc. Kodi peke yake ni zaidi ya Shs 800 kwa litre sasa bei itashuka vipi? kuna faida na hasara za bulk purchase system. Hasara moja wapo ni kwamba kama kampuni mojawapo ya zilizopo TZ zilizo na kampuni mama huko nje zitapewa kununua mafuta, kuna hatari ya masuala ya "transefer pricing" kuingia ndani na hivyo kuongeza gharama zaidi. Niishie hapo kwa leo!
 
Nadhani hili swala ni la kupingwa kabisa hawa jama wanataka kuturudisha enzi za National milling eti lazima watu wote tununue kwa mtu mmoja..kuna risk kubwa sana kwa kutoa tender kwa mtu mmoja na nchi zote zinakumbatia rushwa ndizo zinaendeleza mambo kama hayo wazo langu ni moja waendelee kuruhusiwa watuwengi tu walete mafuta ila serikali ibaki kupanga Bei ndiyo masuala ya kumpta mtu wizara wakati hata elimu ake haihusiani na ile wizara )))
 
Joblube unayosema si kweli kabisa

Mafuta yanauzwa kama commodities kwenye soko la dunia na muuzaji mkubwa ni Opec. Hatakama Tanzania ikinunua mafuta kwa ujumla hamna punguzo lolote watakalopata kwasababu mbili (a) Kiwango wanacho nunua ni kidogo sana 0.0002% hivyo kwanini wapewe punguzo? (b) Mafuta hayauzwi kibinafsi yanauzwa kwenye soko na yakipanda bei haiyajali kama wewe unanunua zaidi au la!. Tanzania na Marekani na China wananunua mafuta kwa bei moja kwenye soko la dunia lakini tofauti ni kodi.
Vilevile ukifanya kampuni moja inunue hakutakuwa na mashindano hivyo bei itakuwa juu kwani hakuna ushindani. Hivyo wazo lako ni nzuri lakini si kwa mafuta mafuta hayauzwi kama machungwa na hii ni rushwa kubwa tu kupeana deal na kukataza wafanyabiashara wadogo. Non SENSE!!
 
Back
Top Bottom